Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CHADEMA azidi kupoteza kura toka kwa wananchi

CCM kama mlishindwa kuitumia gesi ya mtwara kutuondolea kero ya umeme ,msilaghai wananchi kwa huo mradi wa kifisadi wa Stigler's gorge
 
Ndio upuuzi ambao Lissu anawadanganya? Subiri mwakani uanze kupikia umeme.
 
Kama wahenga wanavyosema unapokuwa unaongea na watu unatakiwa uwe mwangalifu maana kauli yako inaweza kukuponza. Na hiki ndicho kinachotokea kwa mgombea wa Chadema. Mdomo na kauli zake zinazidi kumponza na sasa kura zake zinazidi kupungua. Maana atleast watu walikadiria angepata hata kura laki mbili na nusu lakini sasa huenda akaambulia kura laki na nusu.

Mtu mwenye busara zako ambae unasaka kura kwa wananchi huwezi kusema kuwa mradi kama JNHPP hauna manufaa kwa wananchi. Na unaongea na mwandishi wa habari na kuanza kutoa takwimu za kutafuta kwenye mitandao eti gharama za kujenga mradi huo ni Usd bil 11wakati sio kweli.

Hivi ni mtanzania gani ambae hajui umuhimu wa huu mradi? Ni mtanzania gani ambae hajui kuwa gharama za huu mradi ni tril 6.5 ambazo ni sawa na Usd bil 3.3 kwa kukadilia. Kauli ya Tundu Lissu imewatia hofu watanzania sababu inaonyesha wazi hana nia ya kuwaondolea watanzania kero ya gharama kubwa za umeme kwa sasa.Sababu huu mradi utapokamilika ni wazi kuwa gharama za umeme zitakuwa chini.

Nimeshangazwa kusikia Tundu Lissu akisema eti serikali ya awamu ya tano haijafanya jitihada zozote kulinda rasilimali za nchi. Hivi Lissu amesahau kuwa madini kama Tanzanite na dhahabu yalikuwa yanatoroshwa kama nyanya na kwenda kuuzwa nchi za jirani? Lissu amesahau kuwa kuna ukuta umezungushwa Mererani na sasa Tanzanite haitoroshwi tena na mapato ya serikali yameongezeka?
Dhahabu nayo haitoroshwi hovyo na hii ni baada ya kuanzishwa kwa masoko rasmi ya dhahabu. Na masoko haya yamechangia kupata mapato makubwa kwa serikali.

Pia ameshangaza watanzania kwa kusema eti serikali ya awamu ya tano imewanyima haki za kunufaika na rasilimali zao wananchi wanaoishi jirani na migodi mikubwa. Hivi Lissu anashindwa kutambua kuwa awamu ya tano ilivyoingia wachimbaji wadogo wameruhusiwa kufanya shughuli zao bila bugudha. Walikuwa wanafukuzwa maeneo kama Mwakitolyo, Shinyanga lakini serikali ya awamu ya tano ikawaruhusu na kunyag'anya wawekezaji ambao walikuwa hawayaendelezi na kuwanyanyasa wakazi wa maeneo hayo.

Kwa ufupi huyu mgombea wa Chadema ni kama anajiabisha kuzunguka nchi nzima akipinga mambo ambayo hata kwa macho tu mtu mwenye busara huwezi kuyapinga. Na hii ndio inazidi kumpunguzia kura ambazo angezipata kama kifuta machozi kwa kuzunguka Tanzania.

Umemaliza kuandika? Haya kavute kipisi cha bangi ulichokiacha!
 
Nyie CCM hebu acheni kuomba ushindi wa mezani hamuoni aibu? Rudisheni wagombea wote kama nyie vidume kweli ili mpambane na hao mnaowaita wamekufa kwenye sanduku la kura.

Miaka 5 mnaongea peke yenu...sasa kuomba ushindi wa mezani wa nini??
 
Kosa sio la Ccm usiwalaumu. Mliokota wagombea ambao hawako makini. A wanaandika Q. Hii ni kwa sababu wananchi wengi waligombea kupitia Ccm baada ya kuona imekuwa tamu.
 
Nyie CCM hebu acheni kuomba ushindi wa mezani hamuoni aibu? Rudisheni wagombea wote kama nyie vidume kweli ili mpambane na hao mnaowaita wamekufa kwenye sanduku la kura.

Miaka 5 mnaongea peke yenu...sasa kuomba ushindi wa mezani wa nini??
Wagombea wanarudishwa kwa mujibu wa taratibu na sheria za uchaguzi na sio kwa maneno au msukumo wa wafuasi wa chama.
 
Hamna cha taratibu wala nini...hii ni aibu kubwa sana!! Ushindi wa mezani kweli? Yaani CCM kuomba ushindi wa mezani looh!!
 
Kama wahenga wanavyosema unapokuwa unaongea na watu unatakiwa uwe mwangalifu maana kauli yako inaweza kukuponza. Na hiki ndicho kinachotokea kwa mgombea wa Chadema. Mdomo na kauli zake zinazidi kumponza na sasa kura zake zinazidi kupungua. Maana atleast watu walikadiria angepata hata kura laki mbili na nusu lakini sasa huenda akaambulia kura laki na nusu.

Mtu mwenye busara zako ambae unasaka kura kwa wananchi huwezi kusema kuwa mradi kama JNHPP hauna manufaa kwa wananchi. Na unaongea na mwandishi wa habari na kuanza kutoa takwimu za kutafuta kwenye mitandao eti gharama za kujenga mradi huo ni Usd bil 11wakati sio kweli.

Hivi ni mtanzania gani ambae hajui umuhimu wa huu mradi? Ni mtanzania gani ambae hajui kuwa gharama za huu mradi ni tril 6.5 ambazo ni sawa na Usd bil 3.3 kwa kukadilia. Kauli ya Tundu Lissu imewatia hofu watanzania sababu inaonyesha wazi hana nia ya kuwaondolea watanzania kero ya gharama kubwa za umeme kwa sasa.Sababu huu mradi utapokamilika ni wazi kuwa gharama za umeme zitakuwa chini.

Nimeshangazwa kusikia Tundu Lissu akisema eti serikali ya awamu ya tano haijafanya jitihada zozote kulinda rasilimali za nchi. Hivi Lissu amesahau kuwa madini kama Tanzanite na dhahabu yalikuwa yanatoroshwa kama nyanya na kwenda kuuzwa nchi za jirani? Lissu amesahau kuwa kuna ukuta umezungushwa Mererani na sasa Tanzanite haitoroshwi tena na mapato ya serikali yameongezeka?
Dhahabu nayo haitoroshwi hovyo na hii ni baada ya kuanzishwa kwa masoko rasmi ya dhahabu. Na masoko haya yamechangia kupata mapato makubwa kwa serikali.

Pia ameshangaza watanzania kwa kusema eti serikali ya awamu ya tano imewanyima haki za kunufaika na rasilimali zao wananchi wanaoishi jirani na migodi mikubwa. Hivi Lissu anashindwa kutambua kuwa awamu ya tano ilivyoingia wachimbaji wadogo wameruhusiwa kufanya shughuli zao bila bugudha. Walikuwa wanafukuzwa maeneo kama Mwakitolyo, Shinyanga lakini serikali ya awamu ya tano ikawaruhusu na kunyag'anya wawekezaji ambao walikuwa hawayaendelezi na kuwanyanyasa wakazi wa maeneo hayo.

Kwa ufupi huyu mgombea wa Chadema ni kama anajiabisha kuzunguka nchi nzima akipinga mambo ambayo hata kwa macho tu mtu mwenye busara huwezi kuyapinga. Na hii ndio inazidi kumpunguzia kura ambazo angezipata kama kifuta machozi kwa kuzunguka Tanzania.
Anazidi kuipotezea kura chama Cha m.kiti.
 
Ni Magufuli tena
2453634_IMG_20200712_083708.jpg
 
Sina uhakika mwaka 2012 ulikuwa na umri gani wakati wa ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara-Dar es salaam. Kama ulikuwa na umri wa kujitambua bila shaka utakuwa unakumbuka jinsi mradi huo ulivyopata ukinzani mkubwa sana kutoka kwa jamii ya watu wa kusini mpaka serikali ikapeleka kikosi cha kutuliza ghasia na watu walichezea kipigo kweli kweli.

(Kumbuka kauli iliyotolewa kwamba mtu yeyote atakaye jitokeza kuzuia au kukwamisha huo mradi hata kama ana mapembe tutayakata)

Sisi wananchi kwa umoja wetu tuliaminishwa kwamba mradi huo ni mkombozi, na tatizo letu la umeme lililodumu tangu uhuru litabaki kuwa historia, maana umeme utakaozalisha utatosheleza kwa mahitaji yetu na tutapata ziada.

Pili tuliambiwa kwamba gharama za kuzalisha umeme kwa njia ya gesi ni nafuu sana ukilinganisha na umeme mwingine wowote ukiwemo wa maji, upepo, jua au mafuta.

Je ni kweli tatizo la umeme limeisha Tanzania kwa baada ya huo mradi?

Je gharama za umeme zimepungua kama tulivyokuwa tumeaminishwa?

Je vipi kuhusu gesi tunayotumia majumbani gharama zake zikoje?

Lakini cha ajabu huo mradi mpaka sasa hakuna mtu yeyote kutoka serikalini anayeupigia chapuo tena kama ilivyokuwa hapo awali wakati wa kuanzishwa kwake.

Sasa hivi hadithi inayobamba ni hiyo ya stiglers gourge(JKNHPP)

Kwa kurejea mradi wa gesi ulivyokuwa unapigiwa promo na sasa ni kama umetelekezwa maana nguvu kubwa tumehamishia huko JKNHPP.

Katika mazingira hayo unadhani serikali itaaminika vipi kuwa inachotaka kukifanya ni kweli kina manufaa kama inavyoelezwa?

Kubwa kuliko yote, gharama za ujenzi wa hii miradi ni kiasi gani? Na je mikataba yake ikoje?

Kwanini inafanywa kuwa siri, nini kinafichwa?

Usiri huo ni kwa faida ya nani?

Kama nchi hauwezi kuyafikia maendeleo ya kweli kama kila kitu tutakifanya kuwa siri. Binafsi naona suala usiri ni kichaka cha upigaji. Kwanini tufanye siri hata kwenye mambo ambayo hayahusiani kabisa na usalama wa nchi?

Yaani tunafanya mambo kwa ajili ya wananchi lakini hatutaki wajue mikataba tunayoingia kwa niaba yao.

Tuna safari ndefu.
 
Back
Top Bottom