Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CHADEMA azidi kupoteza kura toka kwa wananchi

CCM kama mlishindwa kuitumia gesi ya mtwara kutuondolea kero ya umeme ,msilaghai wananchi kwa huo mradi wa kifisadi wa Stigler's gorge
 
CCM kama mlishindwa kuitumia gesi ya mtwara kutuondolea kero ya umeme ,msilaghai wananchi kwa huo mradi wa kifisadi wa Stigler's gorge
Ndio upuuzi ambao Lissu anawadanganya? Subiri mwakani uanze kupikia umeme.
 
Umemaliza kuandika? Haya kavute kipisi cha bangi ulichokiacha!
 
Nyie CCM hebu acheni kuomba ushindi wa mezani hamuoni aibu? Rudisheni wagombea wote kama nyie vidume kweli ili mpambane na hao mnaowaita wamekufa kwenye sanduku la kura.

Miaka 5 mnaongea peke yenu...sasa kuomba ushindi wa mezani wa nini??
 
Kosa sio la Ccm usiwalaumu. Mliokota wagombea ambao hawako makini. A wanaandika Q. Hii ni kwa sababu wananchi wengi waligombea kupitia Ccm baada ya kuona imekuwa tamu.
 
Nyie CCM hebu acheni kuomba ushindi wa mezani hamuoni aibu? Rudisheni wagombea wote kama nyie vidume kweli ili mpambane na hao mnaowaita wamekufa kwenye sanduku la kura.

Miaka 5 mnaongea peke yenu...sasa kuomba ushindi wa mezani wa nini??
Wagombea wanarudishwa kwa mujibu wa taratibu na sheria za uchaguzi na sio kwa maneno au msukumo wa wafuasi wa chama.
 
Wagombea wanarudishwa kwa mujibu wa taratibu na sheria za uchaguzi na sio kwa maneno au msukumo wa wafuasi wa chama.
Hamna cha taratibu wala nini...hii ni aibu kubwa sana!! Ushindi wa mezani kweli? Yaani CCM kuomba ushindi wa mezani looh!!
 
Anazidi kuipotezea kura chama Cha m.kiti.
 
Sina uhakika mwaka 2012 ulikuwa na umri gani wakati wa ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara-Dar es salaam. Kama ulikuwa na umri wa kujitambua bila shaka utakuwa unakumbuka jinsi mradi huo ulivyopata ukinzani mkubwa sana kutoka kwa jamii ya watu wa kusini mpaka serikali ikapeleka kikosi cha kutuliza ghasia na watu walichezea kipigo kweli kweli.

(Kumbuka kauli iliyotolewa kwamba mtu yeyote atakaye jitokeza kuzuia au kukwamisha huo mradi hata kama ana mapembe tutayakata)

Sisi wananchi kwa umoja wetu tuliaminishwa kwamba mradi huo ni mkombozi, na tatizo letu la umeme lililodumu tangu uhuru litabaki kuwa historia, maana umeme utakaozalisha utatosheleza kwa mahitaji yetu na tutapata ziada.

Pili tuliambiwa kwamba gharama za kuzalisha umeme kwa njia ya gesi ni nafuu sana ukilinganisha na umeme mwingine wowote ukiwemo wa maji, upepo, jua au mafuta.

Je ni kweli tatizo la umeme limeisha Tanzania kwa baada ya huo mradi?

Je gharama za umeme zimepungua kama tulivyokuwa tumeaminishwa?

Je vipi kuhusu gesi tunayotumia majumbani gharama zake zikoje?

Lakini cha ajabu huo mradi mpaka sasa hakuna mtu yeyote kutoka serikalini anayeupigia chapuo tena kama ilivyokuwa hapo awali wakati wa kuanzishwa kwake.

Sasa hivi hadithi inayobamba ni hiyo ya stiglers gourge(JKNHPP)

Kwa kurejea mradi wa gesi ulivyokuwa unapigiwa promo na sasa ni kama umetelekezwa maana nguvu kubwa tumehamishia huko JKNHPP.

Katika mazingira hayo unadhani serikali itaaminika vipi kuwa inachotaka kukifanya ni kweli kina manufaa kama inavyoelezwa?

Kubwa kuliko yote, gharama za ujenzi wa hii miradi ni kiasi gani? Na je mikataba yake ikoje?

Kwanini inafanywa kuwa siri, nini kinafichwa?

Usiri huo ni kwa faida ya nani?

Kama nchi hauwezi kuyafikia maendeleo ya kweli kama kila kitu tutakifanya kuwa siri. Binafsi naona suala usiri ni kichaka cha upigaji. Kwanini tufanye siri hata kwenye mambo ambayo hayahusiani kabisa na usalama wa nchi?

Yaani tunafanya mambo kwa ajili ya wananchi lakini hatutaki wajue mikataba tunayoingia kwa niaba yao.

Tuna safari ndefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…