Chama cha Democratic Party (DP) kimemsimamisha uachamaa Makamu Mwenyekiti Zanzibar Peter Agaton Magwira pamoja na wanachama wengine saba kwa tuhuma za kumuunga mkono mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Alhaji Dk. Husein Ally Mwinyi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho ambae pia ni mgombea wa Urais wa chama cha DP, Juma Mluya wakati akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Kahama mkoani Shinyanga, baada ya kuahirisha mkutano wake kufuatia kuwa na vikao mbalimbali kwa njia ya mtandao kutokana na kauli za makamu mwenyekiti zenye lengo la kuvuruga msimamo wa chama hicho.
"Viongozi wasio wadilifu hatuwezi kuwavumilia wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti ambae sio msemaji wa chama kwa mujibu wa katiba yetu, Mwenyekiti ndio msemaji ambae ndio mimi, hivyo nimemuagiza Katibu mkuu kuwaandikia barua ya kuwasimamisha uongozi wakiwemo wajumbe na wanachama walioshiriki kwenye kikao hicho, "Amesema Juma Mluya.
“Katiba ya chama chetu ibara ya 13 (2) inasema Mwenyekiti wa chama ndio mlinzi wa Katiba na Msemaji wa chama hivyo taarifa ya Makamu huyu ipuuzwe kwani sio msimamo wa chama na nimepata mshtuko wa moyo hivyo ninaahirisha ziara katika mkoa huu" ameongeza Juma Mluya.
Waliosimamishwa uachama ni pamoja na Peter Agaton Magwira ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama Zanzibar, Zainabu Juma Khamisi, Mkude John Mkude, Salma Mateo Petro, Juma Ramadhani Kidawa, Mariam Brash Maseka, Makame Omani Makame, Leonard Damiani Mkoga, kuwa hapo ni wajumbe wa sekretariet na baadhi ya wanachama.
Aidha kufuatia kauli hiyo amelazimika kuahirisha ziara katika mkoa wa shinyanga ili aweze kupumzika kwani jambo hilo limemuathiri kiafya na baada ya mapumziko ya siku mbili kuanzia sasa ataendelea na ziara zake kwa mujibu wa ratiba ya tume ya uchaguzi nchini