GE2025 Mgombea Urais wa NCCR-Mageuzi, Haji Ambar Khamis aahidi Katiba mpya ndani ya siku 100

GE2025 Mgombea Urais wa NCCR-Mageuzi, Haji Ambar Khamis aahidi Katiba mpya ndani ya siku 100

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama NCCR- Mageuzi, Haji Ambar Khamis akiwa ameambatana na Mgombea mwenza, Everylin Munisi, amechukua fomu ya Urais katika Tume Huru ya Uchaguzi Jijini Dodoma leo August 15, 2025 huku akiahidi kuwa endapo Watanzania watamchagua kuwa Rais atahakikisha ndani ya siku 100 tangu kuapishwa kwake Tanzania inapata Katiba mpya.

Akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu, Haji amesema “Kama mnavyofahamu nchi nzima inazungumzia Katiba mpya na karibuni tu mlisikia CCM imeunga mkono kuhuisha Katiba mpya, NCCR ndio Waanzilishi wa mchakato wa Katiba hata Chama chetu kilivyoundwa lengo lilikuwa ni Katiba mpya, hao wengine wamedandia tu, NCCR ndio chimbuko la Katiba mpya”

“Jambo la kwanza tutakalolishughulikia tukiingia madarakani ni Katiba mpya na tunawaahidi Wananchi ndani ya siku 100 tutakuwa tumeshuka na Katiba mpya, Katiba pendekezwa ya Jaji Warioba tutaifanyia marekebisho ndani ya siku 100 tutahakikisha jambo la Katiba mpya limekubalika”

 
Back
Top Bottom