Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kumbe vijana wengi tunachelewa kuoa kwa sababu ya mahari? Lakini tukipewa mahari ndio inatosha? Vipi kutunza familia?
===============
Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK) David Mwaijojele amesema iwapo atapata ridhaa ya kuwa Rais, Serikali ya chama hicho itahakikisha inasimamia Mikopo kwa Vijana na kuondoa mikopo ya kausha damu pamoja na kuwatolea mahari Vijana wanaotaka Kuoa.
Mwaijojele akizungumza wakati wa kampeni zilizofanyika mkoani Mbeya ameomba kura kwa wananchi na kudai kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza nchi serikali yake itatoa mikopo kwa kila mtanzania,atawalipia mahari vijana wanaotaka kuoa na kupeleka gari la wagonjwa kila mtaa ili kubeba wajawazito.