Uncle Rukus
JF-Expert Member
- Jun 16, 2010
- 2,415
- 398
- Thread starter
-
- #21
mbona hiyo habari kwenye mwananchi sijaiona? mwananchi ya leo sio?
Msanii kuna ukweli fulani katika maelezo yako! Lakini kumbuka viongozi wa siasa karibu wote Afrika wako kwa ajili ya maslahi yao. Hata mtu akae miaka 20 kwenye chama sio qurantee kuwa anaamini falsafa na sera za chama. Mambo yalivyo sasa ni kama kurusha shilingi... hujui inaangukia wapi! Afrika itaendelea kuteseka hadi hapo sisi wenyewe tutakapokubali kubadilika!!Niliwahi kusema hapa kwamba KOSA ambalo chadema wanalifanya ni kuwaamini wanaojiunga na chama hicho ktk kipindi cha lala salama ya uchaguzi. Walipaswa kumpokea na kuanza kummezesha maji yenye sabuni za chadema awe msafi kisha apewe jimbo.
Tusikimbilie madaraka tukidhani ndo suluhisho la mwisho.
Dawa ni kujipanga na kuamini timu uliyo nayo haitakuangusha.
Poleni chadema
naona mkuu unamwaga mchele kwenye kuku wengi.
Kikwete amewaambia kwamba uchaguzi ni sawa na vita, kwenye vita kama inavyojulikana si lazima utumie mbinu halali hata mbinu haramu zinarushusiwa. Hiyo ndo Tz yetu
Watu walioendelea hata vitani wanapigana kwa sheria, ndiyo maana kuna Geneva Convention. Sasa kama unataka kutuambia Kikwete ni barbarian ambaye haelewi hili, sawa.
Great Post!
Kama, na kama habari hii yote ni ya kweli, basi sheria ya uchaguzi iangaliwe upya. Kwani jambo hili kutokea linaonesha mapungufu mengi katika kusimamia demokrasia ya kweli.
Kuhama chama ni jambo la kawaida, maana watu hubadilisha misimano na malengo yao kulingana na yale wanayoamini, misimamo yao na yale wanayo kukutana nayo ndani ya chama. Lakini si hoja kubwa kulinganisha na uvurugaji wa sheria kama zipo kulinda uhamiaji wa kiholela wa wagombea. Ni mithili ya transfer window kwenye league za ulaya; wachezaji wanaweza kuhama wapendavyo ndani ya kipindi kilicho idhinishwa, muda ukipita transfer zote zinasimamishwa.
Katika hili, mimi nadhani sheria iweke ku-limit kipindi ambacho mgombea anaweza kuhama toka chama kimoja hadi kingine pale kampeni zinapoanza. Na pale zinapoisha, mgombea huyo kama amesha utwaa ubunge akihama, uchaguzi mdogo wa jimbo unafatia. Ili kuruhusu watu kuchagua mtu na chama wapendacho kulingana na sera zilizopo na maono yao.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba, sheria zetu bado haziruhusu wagombea binafsi, na mgombea mmoja kuhama wakati wa kipindi cha kampeni ambapo kura za maoni zimeshapita na kipindi cha kupitisha wa wakilishaji wa chama kimefungwa, kunaweka disadvantage kwa chama pinzani na demokrasia kiujumla.
Nionavyo hili ni sawasawa na swala lile la kupita bila kupingwa. Kwani itatokea watu wanafanya makusudi kuhamia chama kimoja wakati wakiwa wamekula njama na chama fulani, ili pale kipindi cha kuteua wawakilishi wa chama kinapofungwa, basi mgombea huyo anahama chama kwenda kingine na kukiacha kingine bila mwakilishi.
you can say that again... its not over yet!!! watu walimshukia rev. lakini relevance iko palepaleNilisema hapa CHADEMA wasichukue makapi ya CCM, yatawatokea puani. Watu wakasema ooooh, aaaah.
Sasa mnayaona. Na bora hata huyu karudi CCM kabla ya uchaguzi, kuna wengine watabaki upinzani na kuuhujumu upinzani huu huu bungeni.
Steve-Dii
hivi vyama vya upinzani vilitakiwa vizingatie suala hilo mapema sana. Vili gamble na imeanza kula kwao.
tunaambiwa kuwa zitto kabwe yeye binafsi alienda kuwaomba hao 'walio onewa' kwenye ccm, kujiunga na chadema na baadae kuwapa nafasi ya kugombea majimbo.
Hii mimi inanionyesha dhahiri kuwa hao wahamiaji kwenye vyama vya upinzani hawajahamia kwa kupenda sera au muongozo wa upinzani bali kama njia ya kuikomoa ccm.
Wakipewa pesa ndio haooo wanaondoka bila ya kutizama nyuma kwa kuwa mapenzi tokea hapo mwanzo hayapo.
Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, kwa tiketi ya Chadema Elisha Nkhambaku amerudi tena CCM baada ya kufatwa na uongozi wa juu wa CCM ukimsihi arudi CCM ambako alijiengua baada ya kushinda kwenye kura za maoni na NEC kumuengua kwenye kinyanganyiro hicho.Elisha ambaye alikuwa amejiunga na Chadema ili kugombea kwenye Jimbo hilo la Singida Magharibi amejitoa Chadema baada ya kupewa million 60 na kuahidiwa u-DC kwenye jimbo jipya...
Source: Zimetoka kwa mtu wakaribu sana ambaye alikuwa ni mmoja ya watu waliomfuata Elisha.