Great Post!
Kama, na kama habari hii yote ni ya kweli, basi sheria ya uchaguzi iangaliwe upya. Kwani jambo hili kutokea linaonesha mapungufu mengi katika kusimamia demokrasia ya kweli.
Kuhama chama ni jambo la kawaida, maana watu hubadilisha misimano na malengo yao kulingana na yale wanayoamini, misimamo yao na yale wanayo kukutana nayo ndani ya chama. Lakini si hoja kubwa kulinganisha na uvurugaji wa sheria kama zipo kulinda uhamiaji wa kiholela wa wagombea. Ni mithili ya transfer window kwenye league za ulaya; wachezaji wanaweza kuhama wapendavyo ndani ya kipindi kilicho idhinishwa, muda ukipita transfer zote zinasimamishwa.
Katika hili, mimi nadhani sheria iweke ku-limit kipindi ambacho mgombea anaweza kuhama toka chama kimoja hadi kingine pale kampeni zinapoanza. Na pale zinapoisha, mgombea huyo kama amesha utwaa ubunge akihama, uchaguzi mdogo wa jimbo unafatia. Ili kuruhusu watu kuchagua mtu na chama wapendacho kulingana na sera zilizopo na maono yao.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba, sheria zetu bado haziruhusu wagombea binafsi, na mgombea mmoja kuhama wakati wa kipindi cha kampeni ambapo kura za maoni zimeshapita na kipindi cha kupitisha wa wakilishaji wa chama kimefungwa, kunaweka disadvantage kwa chama pinzani na demokrasia kiujumla.
Nionavyo hili ni sawasawa na swala lile la kupita bila kupingwa. Kwani itatokea watu wanafanya makusudi kuhamia chama kimoja wakati wakiwa wamekula njama na chama fulani, ili pale kipindi cha kuteua wawakilishi wa chama kinapofungwa, basi mgombea huyo anahama chama kwenda kingine na kukiacha kingine bila mwakilishi.