Yaani hii habari si ya kufurahia upande wowote, iwe ni CCM au Chadema, CCM watafurahia tu kwa sababu uhalisia nia yao sio kuwatumikia wananchi ila kutumikia maslahi yao.CHADEMA tukiwapa nchi watauza hadifamilia zetu,mfano mzuri ni kwa wagombea wao kununulika kirahisi namna ile.
Chadema ni ya kuuzunishwa kwa sababu wamepoteza jimbo kirahisi, ila sio kirahisi kama itakavyodhaniwa, chezea nguvu ya pesa.
Unajua shida kuna watu hawaamini ka kura yao inaweza ikaondoa udhalimu wa ccm. Kati ya hao wapo haya ambao ni viongozi wa chadema. Ila mi hainishtui maana haijaanza kwao. Wana Israel wakiwa wanakaribia nchi ya ahadi, waliwatuma watu kwenda kuipeleleza ile nchi, walivyorudi asilimia kubwa walirudi na na taarifa ya kutisha kua wale watu ni mijitu minene, na mirefu, wana silaha za kutosha sisi kwao hatuonekani ka ni watu. Akatokea Joshua akasema wale watu ni wadogo sana, Mungu wetu ni mkubwa kuliko wao .wale wengine walifia njiani hawakufika nchi ya ahadi. Ndivyo ilivyo hata sasa kuna watu wanaiona kama haiwezi kuondka kwa sababu wana Police, wana Tume ya uchaguzi, usalama wapi nyuma yao. Lakini wanasahau kua Mungu wa wanyonge ni mkubwa kuliko ccm. Wanachadema tusikatishwe na tamaa na hao wanaoondoka ila tujifunze kutoka kwao na kuchukua hatua zaidi. Hii safari sio wote lazima wafike, Nguvu ya Umma inaguvu mno kuliko police, NEC nk.wache hao CCM wafurahie kwa sababu walishazoea kutoa rushwa