Wanabodi,
Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye kipindi kirefu nyuma, ambaye nahisi ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama mmja wa makatibu wa CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously kuwa eti imeishaamuliwa (sitaji imeamuliwa na nani), kuwa mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!
Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi kweli ni sababu za msingi na ziko justifiable kwa any reasonable man, sababu nyingine alizonitajia sio tuu ni unreasonable, bali pia ni unjustifiable! na hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!.
, then nitaziweka hadharani hizo sababu za kwa nini CCM imeamua mgombea wake wa urais kwa uchaguzi wa 2015 lazima awe ni John Pombe Magufuli tuu na sio mtu mwingine yoyote!, na kiukweli mkizisikia hizo sababu nilizotajiwa, naamini hata nyinyi sio tuu mtashangaa, bali mtakubaliana na mimi kwanini mtu huyu asiwe!.
Hili la kuamua ni Magufuli, limenistua kidogo kwa sababu kwa sisi tunaomjua asili yake halisi na tuliomfuatilia utendaji kazi wake kwa kauli na matendo tangu akiwa waziri, japo kiukweli ni mchapa kazi, yaani hili ni jembe kazi la ukweli, lakini mtu huyu ameonyesha wazi sio mzuri sana in terms of stability in decision making!, amefanya baadhi ya maamuzi mengi tuu kwa jazba, pupa, papara na kukurupuka kwa mtindo wa nimeamua mimi na liwalo liwe!, mwisho wa siku baadhi ya maamuzi yake ambayo mengine ni very rational yanakuja kutu cost sisi kama taifa,
Paskali