Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Wanabodi,

Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi, ambaye ni mtu wa kuaminika na ni kada wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi pia zimenihuzunisha, kunisikitisha na kunisononesha!, kuwa eti imeishaamuliwa mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!.

Kilichonistua, kunihuzunisha, kunisikitisha na kunisononesha, ni the reasons behind alizonitajia ambazo ndizo zimepelekea CCM kuamua why ni lazima awe Magufuli tuu, and no one else!.

Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi ni justifiable na nyingine sio tuu ni unjustifiable!, bali hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!. Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia from a single source, nahitaji kwanza kufanya collaborative verification na kupata attribution ili nijiridhishe kuwa ni za kweli na kuthibitisha kuwa hivyo ndivyo CCM inavyoweza kufikia maamuzi based on hayo niliyoyasikia!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za CCM on Why ni Magufuli!.

Kwa kawaida sisi waandishi, ukipata taarifa kama hii, huwa inaitwa "news tip", haukimbilii kuiandika mbio mbio mpaka kwanza uifanyie verification kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe, lakini kwa vile sasa tunaishi kwenye "the world of information age", nimeamua kuileta hii "news tip" humu jf, hivi hivi ikiwa kwenye hatua ya "tip" kabla hata ya verification, ili wewe kama mwana jf, uipate ile advantage ya jf, "be the first to know!", hivyo nawaombeni tuu sasa mkae mkijua, "Mgombea wa CCM 2015 ni John Pombe Magufuli!"

Nikiisha "confirm" neno "tetesi" litaondolewa na kuwa replaced na neno "confirmed!", na nitaziweka hizo sababu ila sasa ndio zijadiliwe!, na nawahakikishia wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mkizisikia hizo sababu za CCM!, na nyinyi pia zitawashtua, kuwahuzunisha, kuwasikitisha na kuwasononesha!. Naomba nisiwatajie jina la huyo source wangu chini ya kinga ya kihabari inayoitwa "The Confidentiality of the source".

NB. Sio kila thread ni lazima ichangiwe, saa nyingine itoshe kujisomea tuu na kujipitia bila kuchangia chochote!. Hii ni just a news tip, kwa vile nimewaahidi naifanyia verification kuithibitisha, nawaombeni msiniulize swali lolote at this stage, kwa sababu sitajibu chochote!, and if possible nawashauri na nyingi msome FYE only na sio lazime mchangie kwa sasa na badala yake mvute subira kusubiria verification.
Sababu ya kuiwahisha humu jf kabla ya verification ni ili tuu wewe kama mwana jf to be the first to know!. Information is power!, if you are the first to know, then you'll have the powers to make good things happen or not to happen if they are bad things!.


Asante.
Pasco.
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.
 
Mbona hata raisi wa sasa huwa analalamikiwa kuwa hashauriki?

Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.

Mkuu umri wa kuongozwa na Rais mwanamke Tz bado sana, may b miaka 30 ijayo! Huo ndo ukweli hata kama unauma
 
Pasco muulize huyo mtoa taarifa wako walikuwa wanajadili nini huko songea kwao na aliyekuwa naibu katibu mkuu John ndunguru walipokuwa wameenda kuhan msiba wa marehem mama yake John ndunguru...kikao walichofanya pale kilikuwa na madhumuni gani na sehem ya msiba ikawa ndio sehem ya kuwakutanisha mameneja karibu wote tanroad nchini ....pia muulize nini hasa kilifanya huyo bwana nduguru aondolewe kwenye wadhifa alfajiri siku moja baada ya makatibu na manaibu katibu wakuu wapya kutangazwa alikuwa keshaoga tayari kuelekea kazin mara akapokea taarifa ya kuondolewa katika nafasi hiyo.... akikujibu pia muulize swali la nyongeza mtoa taarifa wako nini huyo magufuli aliambiwa akiwa pamoja na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bwana nchimbi...waliambiwa nini na wale wazee 12 wa taifa hili...
Mbona wewe ndiye umetuacha na maswali zaidi? Umesahau kuwa hapa JF is where we dare talk openly? Funguka basi.
 
Hahahahaha lol!!!! Sijui siye Watanzania tulimkosea nini Mungu mpaka tupate watu wa ajabu ajabu ambao hawana hata sifa moja ya uongozi kuliongoza Taifa letu.

kama aliwambia.wananchi wa kigamboni wapige mbizi.unategemea akiwa rais atawambia nini watanzania? jibu jaza hapa { }
 
..Magufuli ni mropokaji.

..hana kabisa breki ya mdomo.

..pia inaonekana hajatulia kimawazo, na Uraisi hauhitaji mtu wa namna hiyo.
Au wewe ni mhanga wa magufuli? maana jamaa ameumiza wengi,ukianzia waliojimilikisha magari ya umma,njoo kwa wezi wa viwanja, malizia na samaki alizozikamata na meli ikazama.
Kimsingi tunamhitaji heri alaumiwe kama nyerere lkn nchi isonge mbele
 
Kitabu cha siri ndani ya CCM kinasema " ni haramu kafiri (mkristo) kuwa mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM. Mi sishangahi kuona Magufuli ndo mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM ila watambue kuwa nchi hii haina dini, kabila, wala kanda.Nchi ni yawote...
Jiulize je! Katika historia ya Tanzania kashatokea mgombea uraisi mkristo kwa tiketi ya CCM?
Waache ujinga tuijenge nchi.

Hee hilo nalo jipya! Kumbe kuna kitabu cha siri!
 
Au wewe ni mhanga wa magufuli? maana jamaa ameumiza wengi,ukianzia waliojimilikisha magari ya umma,njoo kwa wezi wa viwanja, malizia na samaki alizozikamata na meli ikazama.
Kimsingi tunamhitaji heri alaumiwe kama nyerere lkn nchi isonge mbele

Kwa kweli kila mtu ana mabaya na mazuri yake! Watu wanamponda kwa mabaya tu bila kuangalia upande wa pili!
 
RAIS wa segerea au ukonga gerezanu!!! maana cdm tunachukua nchi rais slaa lazma atafunga jela wezi wote
 
........., ni the reasons behind alizonitajia ambazo ndizo zimepelekea CCM kuamua why ni lazima awe Magufuli tuu, and no one else!.

Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi ni justifiable na nyingine sio tuu ni unjustifiable!, bali hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!. Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia from a single source, nahitaji kwanza kufanya collaborative verification na kupata attribution ili nijiridhishe kuwa ni za kweli na kuthibitisha kuwa hivyo ndivyo CCM inavyoweza kufikia maamuzi based on hayo niliyoyasikia!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za CCM on Why ni Magufuli!.

.................., na nitaziweka hizo sababu ila sasa ndio zijadiliwe!, na nawahakikishia wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mkizisikia hizo sababu za CCM!, na nyinyi pia zitawashtua, kuwahuzunisha, kuwasikitisha na kuwasononesha!. Naomba nisiwatajie jina la huyo source wangu chini ya kinga ya kihabari inayoitwa "The Confidentiality of the source".

......

Hapa umenichanganya...unasema ....sababu kwa sasa huziweki hadharani....lakini unatutaka tuzijadili....hizo hizo sababu...!!! Tutajadilije sababu ...ambazo bado hujaziweka hadhari...!??

Ebu niweke sawa hapo...Mkuu Pasco wa JF.
 
ajabu :A S-eek:, mi najua mwakani CCm wanang'olewa na ukawa mwaka 2015.. maana ndivo juzi walivo tangaza na nikajua baada ya ccm kukutana na azama hii ya kutaka kung'olewa na wababe wa ukawa wataweza kutafuta jembe.... wameamua kumuweka mtu anaye panic na anafanya maamuzi ambayo hayajulikani wapi yanatoka? nape hawezi ​KUKUBALI.
 
Mkuu Pasco unaweza kuwa karibu na ukweli halisi hasa ukizingatia harakati za Bwana Pombe mara kaja na daraja la Kigamboni kashalitembelea na kulikagua mara tatu,akaja na swaga nyingine bandari ya nchi kavu Ruvu nikajisemea tangu lini kawa waziri wa uchukuzi kabla hali ya hewa haijakaa sawa katembelea vivuko sijui vya wapi vile nikajisemea huyu si bure nikadhani sasa atatulia kumbe wapi kaja na barabara za juu sijui zinaitwa flyover kazitolea ufafanuzi kwamba foleni Dar itakuwa historia duh.

Mpaka hapo ndugu mwanaJF mwenzangu uhitaji kuambiwa na Pasco huyu ndio mgombea wa CCM hapana tumia akili yako kiduchu utagundua Pombe safari hii kaamua haswa haogopi magazeti ya Rostitamu wala mifedha ya Laigwanani wa Monduli jogoo awike asiwike lazima kutakucha tu.Nafasi ya Pombe safari hii ni wazi kwasababu pia Vasco Dagama asingependa Rais ajae atoke nje ya baraza lake la mawaziri ukitamza baraza lake sasa hakuna waziri anayemkaribia Pombe kwa vituko nasema vituko si kwa bahati mbaya la hasha Bwana Pombe ni waziri wa kukariri barabara na kilometa,ni waziri mropokaji kuliko mawaziri wote wa Vasco labda unaweza kumlinganisha na aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Bwana Makamba hana akili hajui aseme nini wapi na wakati gani kwa hakika Tanzania itakuwa na Rais wa hovyo kuliko marais wate tangu tupate uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Tena ni fisadi mkubwa, alikuwa mstari wa mbele akishirikiana na fisadi Mkapa katika ukwapuzi wa nyumba zenye thamani zaidi ya trillion za Serikali....Hafai kabisa huyu fisadi.


Ilithibitika kuwa Pombe Magufuli alimuhonga kimada wake nyumba ya serikali hivyo fastahili kuwa mpangaji wa Magogoni atahonga nchi!!
 
Mie siyajui mazuri yake kama wewe unayajua yaweke, mapungufu haya si madogo na hayastahili kudharauliwa katika kumtathmini huyu kama ana sifa ya kuliongoza Taifa. Haya madudu kayafanya akiwa Waziri, akiingia Ikulu si ndiyo itakuwa msalie mtume na MACCM hata mtu pale IKULU akivurunda namna gani wana utamaduni wao wa kuachiana mpaka amalize awamu zake mbili za miaka mitano mitano.

Umeandika mapungufu peke yake! Tuwekee na mazuri pia aliyotufanyia ili tulinganishe. Moja ya mazuri ni pamoja na kuuzuia uwanja wa Nyamagana usipewe muwekezaji ili watu wa Mwanza waendelee kupumua kwenye uwanja wao wa kiistoria. Weka na mazuri unayoyafahamu
 
Hilo ni kweli kabisa Mkuu Ndinani alihonga nyumba, lakini watu wanataka kuyafukia madudu yake na kudai jamaa ni "jembe" ukiwaambia waweke yale mazuri yake wanang'aa macho. Huyu fisadi naye hafai kabisa kuingia Ikulu makosa yaliyofanyika 1995 na 2005 tusiyarudie tena.

Ilithibitika kuwa Pombe Magufuli alimuhonga kimada wake nyumba ya serikali hivyo fastahili kuwa mpangaji wa Magogoni atahonga nchi!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom