Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.
 
Mbona hata raisi wa sasa huwa analalamikiwa kuwa hashauriki?

Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.
 

Mkuu umri wa kuongozwa na Rais mwanamke Tz bado sana, may b miaka 30 ijayo! Huo ndo ukweli hata kama unauma
 
Mbona wewe ndiye umetuacha na maswali zaidi? Umesahau kuwa hapa JF is where we dare talk openly? Funguka basi.
 
Hahahahaha lol!!!! Sijui siye Watanzania tulimkosea nini Mungu mpaka tupate watu wa ajabu ajabu ambao hawana hata sifa moja ya uongozi kuliongoza Taifa letu.

kama aliwambia.wananchi wa kigamboni wapige mbizi.unategemea akiwa rais atawambia nini watanzania? jibu jaza hapa { }
 
..Magufuli ni mropokaji.

..hana kabisa breki ya mdomo.

..pia inaonekana hajatulia kimawazo, na Uraisi hauhitaji mtu wa namna hiyo.
Au wewe ni mhanga wa magufuli? maana jamaa ameumiza wengi,ukianzia waliojimilikisha magari ya umma,njoo kwa wezi wa viwanja, malizia na samaki alizozikamata na meli ikazama.
Kimsingi tunamhitaji heri alaumiwe kama nyerere lkn nchi isonge mbele
 

Hee hilo nalo jipya! Kumbe kuna kitabu cha siri!
 
Au wewe ni mhanga wa magufuli? maana jamaa ameumiza wengi,ukianzia waliojimilikisha magari ya umma,njoo kwa wezi wa viwanja, malizia na samaki alizozikamata na meli ikazama.
Kimsingi tunamhitaji heri alaumiwe kama nyerere lkn nchi isonge mbele

Kwa kweli kila mtu ana mabaya na mazuri yake! Watu wanamponda kwa mabaya tu bila kuangalia upande wa pili!
 
RAIS wa segerea au ukonga gerezanu!!! maana cdm tunachukua nchi rais slaa lazma atafunga jela wezi wote
 

Hapa umenichanganya...unasema ....sababu kwa sasa huziweki hadharani....lakini unatutaka tuzijadili....hizo hizo sababu...!!! Tutajadilije sababu ...ambazo bado hujaziweka hadhari...!??

Ebu niweke sawa hapo...Mkuu Pasco wa JF.
 
ajabu :A S-eek:, mi najua mwakani CCm wanang'olewa na ukawa mwaka 2015.. maana ndivo juzi walivo tangaza na nikajua baada ya ccm kukutana na azama hii ya kutaka kung'olewa na wababe wa ukawa wataweza kutafuta jembe.... wameamua kumuweka mtu anaye panic na anafanya maamuzi ambayo hayajulikani wapi yanatoka? nape hawezi ​KUKUBALI.
 
Mkuu Pasco unaweza kuwa karibu na ukweli halisi hasa ukizingatia harakati za Bwana Pombe mara kaja na daraja la Kigamboni kashalitembelea na kulikagua mara tatu,akaja na swaga nyingine bandari ya nchi kavu Ruvu nikajisemea tangu lini kawa waziri wa uchukuzi kabla hali ya hewa haijakaa sawa katembelea vivuko sijui vya wapi vile nikajisemea huyu si bure nikadhani sasa atatulia kumbe wapi kaja na barabara za juu sijui zinaitwa flyover kazitolea ufafanuzi kwamba foleni Dar itakuwa historia duh.

Mpaka hapo ndugu mwanaJF mwenzangu uhitaji kuambiwa na Pasco huyu ndio mgombea wa CCM hapana tumia akili yako kiduchu utagundua Pombe safari hii kaamua haswa haogopi magazeti ya Rostitamu wala mifedha ya Laigwanani wa Monduli jogoo awike asiwike lazima kutakucha tu.Nafasi ya Pombe safari hii ni wazi kwasababu pia Vasco Dagama asingependa Rais ajae atoke nje ya baraza lake la mawaziri ukitamza baraza lake sasa hakuna waziri anayemkaribia Pombe kwa vituko nasema vituko si kwa bahati mbaya la hasha Bwana Pombe ni waziri wa kukariri barabara na kilometa,ni waziri mropokaji kuliko mawaziri wote wa Vasco labda unaweza kumlinganisha na aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Bwana Makamba hana akili hajui aseme nini wapi na wakati gani kwa hakika Tanzania itakuwa na Rais wa hovyo kuliko marais wate tangu tupate uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Tena ni fisadi mkubwa, alikuwa mstari wa mbele akishirikiana na fisadi Mkapa katika ukwapuzi wa nyumba zenye thamani zaidi ya trillion za Serikali....Hafai kabisa huyu fisadi.


Ilithibitika kuwa Pombe Magufuli alimuhonga kimada wake nyumba ya serikali hivyo fastahili kuwa mpangaji wa Magogoni atahonga nchi!!
 
Mie siyajui mazuri yake kama wewe unayajua yaweke, mapungufu haya si madogo na hayastahili kudharauliwa katika kumtathmini huyu kama ana sifa ya kuliongoza Taifa. Haya madudu kayafanya akiwa Waziri, akiingia Ikulu si ndiyo itakuwa msalie mtume na MACCM hata mtu pale IKULU akivurunda namna gani wana utamaduni wao wa kuachiana mpaka amalize awamu zake mbili za miaka mitano mitano.

 
Hilo ni kweli kabisa Mkuu Ndinani alihonga nyumba, lakini watu wanataka kuyafukia madudu yake na kudai jamaa ni "jembe" ukiwaambia waweke yale mazuri yake wanang'aa macho. Huyu fisadi naye hafai kabisa kuingia Ikulu makosa yaliyofanyika 1995 na 2005 tusiyarudie tena.

Ilithibitika kuwa Pombe Magufuli alimuhonga kimada wake nyumba ya serikali hivyo fastahili kuwa mpangaji wa Magogoni atahonga nchi!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…