Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Pasco unazingua tumwagie sababu, sisi wagalatia tunataka kuzijua
Hivyo hizo sababu kwa nini ni Magufuli na ni nani walioamua ni Magufuli, nilitajiwa, ila mimi mwenyewe siamini kuwa huo ndio ukweli wenyewe!, ndio maana nikashauri, amini kuwa nilisema ni Magufuli na kweli ikatokea tuu kuwa ni kweli ni Magufuli, just a coincidentally!.

Pasco
 
Wajameni uzi wangu huu bado uko valid kwa sababu zile sababu nilizo zisikia za why mgombea wa CCM ni Magufuli sijazitaja kwa sababu siziamini!. Kama kuna yeyote humu anayejua ilikuwaje akawa ni Magufuli naomba atudokeze vinginevyo itanilazimu nizitaje, na ikitokea zikawa ni kweli, then Magufuli atakuwa hatufai kabisa ni mtu wa kumuogopa kama ukoma!.
Pasco

Ha ha ha ha..."then Magufuli atakuwa hatufai kabisa ni mtu wa kumuogopa kama ukoma"

Mkuu Pasco, bado unashikilia hii kauli yako?
 
Kipindi kile niliwahi kutabili kama hivi kijiwe fulani...kidogo wanakijiwe waniweke kaa la moto mdomoni...!!!
 
Aisee

Mimi naweza nikataja baadhi ya sababu ulizoambiwa.
Mosi, anatoka kanda ya ziwa ambako inadaiwa kuwa ni kanda iliyoikimbia ccm 2010. Hata majimbo waliyonayo mengi waliyachakachua.
Ile hoja ya kitoto ya kidini inaweza kuwa imejificha humo
Umachachari wake inaweza kuwa sababu mojawapo
Inaweza kuwa ni mtu muhimu kuwasaidia akina nani hili kumdhibiti mtu kwa kuwa kanda ya ziwa ina watu wengi. Nawaza tu shemeji yangu pasco
 
..i am not.

..watu walikuwa hawa pay attention kwa mambo aliyokuwa akifanya.

..hata kashfa ya kuuza nyumba za serikali wapinzani wangeifuatilia na kuundiwa tume bila shaka ingemuondoa ktk uongozi.
 
Mussolin5,

..umesema mimi ni legend but i am not.

..watu walikuwa hawa pay attention kwa mambo aliyokuwa akifanya.

..hivi sifa alizokuwa akimpa JK ktk mikutano ya hadhara mlikua hamuoni kwamba ni mtu wa ajabu kidogo?

..hata kashfa ya kuuza nyumba za serikali wapinzani wangeifuatilia na kuundiwa tume bila shaka ingemuondoa ktk uongozi.
 
Asilimia 90 ya id zilizochangia huu uzi wakati huo zote zilikua Mpya na zimepotea hadi leo
 
Tunahitaji rais kama magufuli,nchi hii imechoshwa na siasa na sasa inataka utendaji na vitu vionekane kwa mipango,watu wanafanya nchi kama idara ya zimamoto, nchi imekuwa na slogani nyingi,mara ari mpya,maisha bora,kilimo kwanza, big result now,mabilioni ya kikwete...magufuli hana upuuzi huo,yeye anafanya kazi japo ana mapungufu, mapungufu hayo yanafunikwa na utendaji,usimamiaji.KAMA HAMTAMPA WA MUUNGANO,NI BORA TANGANYIKA IRUDI TUTAMPA URAIS WA HUKU
Njoo tena urudie kusoma hii post yako
 
magufuli ni mchapakazi lakini hafai kuwa kwa rais kwa sababu zifuatazo
1. intellectual arrogance - anadhan kua anajua kila kitu na akishaamua basi hakuna wazo jipya litakalokuja kuimprove alichoamua ni lazima kifanyike ivyo ivyo au hakuna wazo jipya litalomfanya abadili maamuz kwamba hicho anachokitaka kinawez kisiwe sahihi kwa mfano alivyokua anavunjia watu ovyo mpaka aliposhinwa ile kesi mahakamani wakat yy alikua anang'ang'ania kua anatimiza sheria.

2. hana uvumilivu - kiongoz bora yoyote lazima awe mvumilivu hasa anapokosolewa kwa mfano anapandoisha jazba kwa mambo madogo aliwambia watu wasioweza lipa nauli mpya ya kivuko wapige mbizi wakat kiongoz mzuri angekaa kimya tu.

3. anafata sheria kisabato - sheria hata kama ipo mda mwingine busara itumike kwa mfano anapong'ang'ania kuvunjia watu hata sehem zisizo na tija bila huruma nadhan akipewa lungu la urais watu watasaga meno kwa kigezo cha kufata sheria. ndo mana hata jesus aliuliza its ok usifanye kazi jmosi lakini ngombe wako akidumbukia mtoni hutamtoa busara ya bwana magufuli ni kwamba sitamtoa acha afe!!!

4. atakua haeshim judiciary - kitendo chake cha kujitafisira sheria anavyojua na kuzitekeleza kitamcost na kitasumbua watu akiwa rais, mara zaid ya 2 mahakama ndio imetoa nishai kwa kutengua maamuz yake ambayo yy alikua anadai anafata sheria nk

magufuli ni mtendaji mzuri nadhan kwa nafasi ya urais unaitaji caliber ya juu kidogo zaidi ya utendaji ambayo bwana magufuli hana nampenda kwa uchapa kazi wake lakini kwa urais hapana the maximum he can go up ni kua prime minister si zaid ya apo.

the ultimate glory i honestly fee should go to Dk. Harrison mwakyembe, he is composed, mchapa kazi na sheria anazijua vizur and he got the caliber kuwa mvumilivu!!!

sitta is simply lacking some know how and smartness, and he has already passed his sell by date!!!
Hii post iishi miaka 10...
 
Hii post iishi miaka 10...
Vigezo hivi ndivyo vilipaswa kuzingatiwa na wana Usalama wa Taifa katika kumshauri Rais aliyekuwa madarakani wakati ule juu ya harakati za kumtafuta mrithi wa JK. Kwa bahati mbaya nchi haina mfumo wa serious vetting haswa kwa wagombea toka CCM! Kuna siku nchi itatawaliwa na mzungu wa unga au chizi atakayeiangamiza nchi!
 
Back
Top Bottom