Wanabodi,
Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi, ambaye ni mtu wa kuaminika na ni kada wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha, zimenisikitisha, kunihuzunisha, kuniogopesha na kunisononesha!, kuwa eti imeishaamuliwa (situation na nani), mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!.
Kilichonistua, kunitisha, kunihuzunisha, kunisikitisha, kunisononesha na kunigopesha, ni the reasons behind alizonitajia ambazo ndizo zimepelekea CCM kuamua why mgombea wake ni lazima awe John Pombe Magufuli tuu, and no one else!.
Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi kweli ni justifiable na nyingine sio tuu ni unjustifiable!, bali hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!. Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza hizo sababu, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia from a single source, nahitaji kwanza kufanya a double check, na cross check ikiwemo kupata a collaborative verification na attribution ya third parties ili nijiridhishe kuwa hii ni habari za kweli na kuthibitisha kuwa kumbe hivyo ndivyo the inner core ya CCM inavyoweza kufikia maamuzi ya mgombea wake based on sababu nilizo tajiwa!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za kwa nini CCM imeamua mgombea wake lazima awe ni Magufuli tuu!, na kiukweli mkizisikia hata nyinyi mtashangaa!.
Kwa kawaida sisi waandishi, ukipata taarifa kama hii, huwa inaitwa "a news tip", haukimbilii kuiandika mbio mbio mpaka kwanza uifanyie verification kwa kui double check na kui cross check ili kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe, baada ya kuthibitisha na kujiridhisha ndipo unaiandika.
Lakini kwa vile sasa tunaishi kwenye "the world of information age", nimeamua kuileta hii "news tip" humu jf, hivi hivi ikiwa kwenye hatua ya "tip" kabla hata ya verification, ili wewe kama mwana JF, uipate ile JF advantage ya "be the first to know!", hivyo nawaombeni tuu sasa mkae mkijua, "Mgombea wa urais wa CCM kwa mwaka 2015 ni John Pombe Magufuli!. Hili la kuamua ni Magufuli, limenistua kidogo kwa sababu kwa tuliomfuatilia Magufuli kwa kauli zake na matendo, huyu sio mtu mzima sana, anafanya baadhi ya maamuzi ya papara na kukurupuka mtindo wa liwalo liwe , hivyo akipita, ana chance ya kuja kuwa the worst dictator this nation has ever had.
Nikiisha "confirm" neno "tetesi" litaondolewa na kuwa replaced na neno "confirmed!", na nitaziweka hizo sababu ila sasa ndio zijadiliwe!, na nawahakikishia wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mkizisikia hizo sababu za CCM kwa nini ni Magufuli!, na nyinyi pia zitawashitua, zitawatisha, zitawaogopesha, kuwahuzunisha, kuwasikitisha na kuwasononesha!.
Naomba nisiwatajie jina la huyo source wangu chini ya kinga ya kihabari kwa ma source inayoitwa "The Confidentiality of the source", na hapa wakati naileta taarifa hii humu jf, kwa vile zoezi la kumteua mgombea wa CCM bado liko mbali hadi mwaka ujao, unaweza kukuta hata Magufuli mwenyewe bado hajui kuwa ni yeye ndie atakuwa mgombea wa CCM, kwa sababu walio amua kuwa ni Magufuli sio kikao chochote halali ndani ya CCM bali ni "The Inner Circle" hivyo hii ni tip kutoka kwa "the inner circle", na bahati mbaya sana, Magufuli mwenyewe hayuko kwenye hiyo "the inner circle!".
NB. Sio kila thread ni lazima ichangiwe, saa nyingine itoshe kujisomea tuu na kujipitia bila kuchangia chochote!. Hii ni just a news tip, kwa vile nimewaahidi naifanyia verification kuithibitisha, nawaombeni msiniulize swali lolote at this stage, kwa sababu sitajibu chochote!, and if possible nawashauri na nyingi msome FYE only na sio lazime mchangie kwa sasa na badala yake mvute subira kusubiria verification.
Sababu ya kuiwahisha humu JF kabla ya verification ni ili tuu wewe kama mwana JF to be the first to know!. Information is power!, if you are the first to know, then you'll have the powers to make good things happen or not to happen if they are bad things!.
Asante.
Paskali
Update: 12/07/2015
Leo hili limetimia ni kweli aliyepita ni Magufuli, nimezitafakari sababu nilizotajiwa ile siku napewa tetesi hii, na kuzipima na hiki kilichotokea, nimejikuta nimelazimika kutoziamini kuwa zile nilizosikia ndizo sababu zenyewe halisi.
Kwa sisi waandishi tuna kanuni, ukilisikia jambo, kama huliamini, then usiliseme wala kuliandika, hivyo hizo sababu nilizopewa siku hiyo, on why ni Magufuli, mimi siziamini, naomba nisiziseme kabisa, hivyo naomba tuchukulie kupitishwa kwa jina la John Pombe Magufuli kumetokea tuu naturally, by chance, bila any pre meditated moves, na hili bandiko lichukuliwe tuu kama just a coincidence, kuwa nilisema mgombea wa CCM atakuwa ni Magufuli na kweli ikatokea tuu coincidentally, mgombea wa CCM kweli ni Magufuli.
Kwa mtakaonielewa asanteni kwa kunielewa, na kwa msio nielewa samahanini sana!.
Hongera sana John Pombe Joseph Magufuli kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM.
Paskali