Usafiri wa daladala umeanza kurejea katika baadhi ya maeneo, ikiwemo njia za Kabwe–Iyunga na Kabwe–Mjini/Uhindini, ingawa idadi ya daladala bado ni ndogo.
Baadhi ya madereva wameendelea kushinikiza wenzao waliokamatwa waachiliwe huru ili waweze kurejesha huduma.
Your browser is not able to display this video.
Usafiri wa bajaji bado haujarejea barabarani, madereva wanataka utaratibu wa zamani wa kutumia barabara kuu urejeshwe.
Kutokana na hali hiyo, nauli za usafiri ndani ya mji zimepanda hadi kati ya Tsh. 5,000 - 8,000, kutegemea aina ya usafiri unaopatikana. Baadhi ya wafanyakazi walilazimika kulala ofisini kutokana na kukosa usafiri wa kurejea nyumbani.