Mgomo na uasi wa Jeshi nchini mwaka 1964

Mgomo na uasi wa Jeshi nchini mwaka 1964

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,491
350px-Zanzibar%2C_12_Jan._2004%2C_celebration_of_40_years%27_Revolution.JPG


Mwaka 1919 Uingereza ilikabidhiwa utawala juu ya Tanganyika na Shirikisho la Kimataifa. Waingereza walipanusha mfumo wa King's African Rifle waliowahi kuanzishwa Kenya hadi Tanganyika. Jeshi la Kings African Rifles ilikuwa na vikosi (battalions) 6 ambazo viwili vilikuwepo Kenya, vitatu Tanganyika na kimoja huko Uganda. Katika kikosi cha sita cha King's African Rifles kilichoanzishwa mwaka 1917 kwa kuajiri askari kutoka Tanganyika walikuwepo pia askari wa awali wa jeshi la Kijerumani la Schutztruppe waliowahi kukamatwa kama wafungwa na kukubali kuendelea upande wa Waingereza.


Baada ya uhuru mwaka 1961 vikosi vya Kings African Rifles katika Tanganyika vilibadilishwa jina na kuwa Tanganyika Rifle (TR). Pamoja na kubadilika jina Tanganyika Rifles ilikuwa na muundo sawa na Kings African Rifles (KAR). Maafisa wenye mamlaka bado walikuwa Waingereza, pamoja na Waafrika watano waliopandishwa cheo wakati wa uhuru na kupokea mafunzo katika vyuo vya kijeshi vya Kiingereza. Jeshi jipya lilipangwa katika vikosi viwili vyenye makao makuu huko Dar es salaam na Tabora. Afisa mkuu alikuwa Brigedia Jenerali Patrick Sholto Douglas.
Kwa jumla kulikuwa na hali ya kutoridhika kati ya askari wa Tanganyika Rifle(TR). Sababu yake ilikuwa matumaini ya kwamba uhuru ungeleta mabadiliko makubwa zaidi na nafasi za kupanda cheo baada ya kuondoka kwa maafisa wazungu.

Lakini maafisa Waingereza waliendelea kuajiriwa na serikali ya Nyerere na tofauti kubwa katika mapato na hali ya makazi ya Wazungu na Waafrika ziliendelea. Hata kinyume askari waliowahi kuwa na mshahara wa juu kulingana na watumishi Waafrika wengine ya serikali waliona ya kwamba mapato yao hayakupanda ilhali mishahara kwa jumla iliongezeka zaidi. Zaidi ya hapo, serikali ya TANU ilituma vijana kutoka Umoja wa Vijana wa TANU kwa mafunzo ya kijeshi huko Israel na baada ya kurudi walipewa ajira jeshini na wengine wao kupandishwa vyeo kupitia askari waliowahi kuhudumia miaka mingi.

Katika Januari 1964 matokeo mawili yalijadiliwa sana kati ya askari moja ilikuwa tangazo la Nyerere alikotamka mwisho wa siasa ya "Africanization" katika utumishi wa serikali.Tangazo hili lilisababisha viongozi wa umoja wa wafanyakazi kulalamika. Tukio lingine likawa habari za mapinduzi ya zanzibar yaliyoanza tar. 12 Januari 1964.

Tarehe 20 Januari 1964, bado wakati wa usiku, kikosi cha kwanza cha TR kwenye kambi la Colito Barracks mjini Dar es Salaam kiliasi na kujipatia silaha kutoka ghala. Maafisa Waingereza walikamatwa na kufungwa lakini mkuu Douglas aliweza kujificha. Waasi walivamia kituo cha redio, uwanja wa ndege, ikulu na ofisi ya posta na simu. Maafisa Waingereza na Waafrika wasioshiriki na waasi walisafirishwa Kenya. Rais Nyerere alienda mafichoni katika kanisa moja la kikatoliki ng'ambo ya bandari akamwachia waziri Oskar Kambona kazi ya kuwasiliana na wanajeshi. Madai ya wanajeshi yalikuwa kuachishwa kwa maafisa Waingereza na kupandishwa kwa mishahara. Siku za kwanza ya mgomo wa jeshi ilifuatwa na vipindi vya fujo mjini vilivyobadilika na vipindi vya kimya, mashambulizi dhidi ya maduka ya Wahindi na kukamatwa kwa Wazungu wachache. Hata mbalozi wa Uingereza alikamatwa kwa kipindi kifupi.

Waziri Kambona alianza kujadiliana na wanajeshi na kuwaahidi ongezeko la mapato na kutoa vyeo vya juu kwa Waafrika kadhaa. Nyerere alirekodi hotuba iliyotangazwa redioni alipokosoa wanajeshi na kudai utulivu. Askari walirudi kwenye kambi lakini kurudi mjini siku iliyofuata. Pia huko Nairobi na Kampala ulitokea uasi wa wanajeshi -wote askari wa KAR wa awali. Maraisi Milton Obote na Jomo Kenyatta hawakusita kuomba vikosi wa jeshi la Uingereza vilivyokuwa bado na vituo kwa kuzimisha ghasia. Hatimaye Nyerere alianza mawasiliano na Uingereza iliyotuma manowari na wanajeshi kutoka Aden kuelekea Daressalaam.Polisi ya siri ya Tanzania ilianza kupata habari ya kwamba pia kati ya askari ya Field Force unit majadiliano yalikuwa yameanza kuunga mkono na juhudi za wanajeshi, pia harakati kati ya wafanyakazi bandarini na hofu ilikuwa ya kwamba sehemu ya viongozi wa umoja wa wafanyakazi walikuwa na mipango ya kujiunga nao.

Tarehe 24 Januari serikali ya Tanzania iliomba rasmi Uingereza kuingia kati na kuzimisha uasi. Asubuhi ya 25 Januari kikosi kidogo cha wanajeshi wa Kiingereza waliondoka kwa njia ya helikopta kwenye meli iliyokaa baharini karibu na Dar es Salaam wakavamia kambi la Colito Barracks. Jenerali Douglas alihotubia askati kwa kipazia sauti akadai wanajeshi wajisalimishe. Mwanzoni walikataa lakini baada ya mashambulio mafupi ya Wingereza walio wengi walijisalimisha wengine wakakimbia na viongozi walikamatwa. Vilevile askari wa Dodoma na Nachingwea waliowahi kujiunga na uasi walijisalimisha bila upinzani baada ya kufika kwa askari Waingereza wachache.

Wakazi wengine wa Daressalaam walikuwa na hofu ya kwamba Uingereza ulikuwa umerudi ili kurudisha ukoloni lakini baada ya kusita masaa machache Nyerere alieleza kwa njia ya redio ya kwamba kuingilia kwa Uingereza ulifuata ombi la serikali yake.

Watu wengi walikamatwa baada ya matukio haya na kufanyiwa utafiti kama walikuwa na uhusiano na uasi.

Askari Waingereza waliondoka kwenye Aprili 1964 na nafasi yao ilichukuliwa na kikosi kutoka Nigeria iliyofika kwa niaba ya Umoja wa Afrika kufuatana na ombi la serikali ya Tanganyika.

Kuanzisha jeshi jipya la wananchi (Jeshi la Wanainchi wa Tanzania -JWTZ)
Baada ya uasi, jeshi la Tanganyika Rifle(TR) lilivunjwa. Askari wote waliachishwa. Sehemu ya askari wa Dodoma waliajiriwa tena katika jeshi jipya lakini hao wa Dar es Salaam hawakurudishwa. Maafisa Waafrika ambao kwa jumla walisimama upande wa serikali na kutoshiriki katika uasi waliajiriwa tena.

Jeshi jipya lilijengwa kwa kuajiri hasa wanachama wa umoja wa vijana wa TANU likapewa jina la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Jeshi hili jipya liliwekwa chini ya usimamizi ya chama cha TANU (baadaye CCM) kwa kufuata mtindo wa nchi kama Urusi na China. Kamanda wa kwanza alikuwa Mrisho Sarakikya aliyewahi kusimama upande wa serikali wakati wa uasi akapandishwa cheo kutoka luteni hadi kanali, baadaye kuwa jenerali.

Mwanzoni JWTZ ilikuwa jeshi ndogo lenye askari chache kuliko TR lakini hadi 1967 lilipanushwa kuwa na vikosi 4. Mnamo 1972 JWTZ lilikadiriwa kuwa na askari 10,000 katika vikosi vinne pamoja na vifaa vya vifaru 20 aina ya Kifaru T-59, 14 Kifaru T-62, mizinga ya Kirusi na Kichina. Vipuli vilikuwa haba na sehemu ya vifaa haikuweza kutengenezwa.
 
Story yako haijakamilika bila ya kumtaja Elisha Kavana, graduate wa The Royal Military Academy Sandhurst
 
jazia nyama za kutosha mkuu.... kama vile kuna gape nyingi, nadhani hivo tuuu kwa uelewa wangu
 
Colito Barracks ndiyo Lugalo kwa sasa kwa wale wageni.
 
mkuuu yaani unielekeze
kama kunijuza laaabda kiongozi wa majaribio haya na kabineti yake.
Story inajieleza vizuri tu....Elisha Kavana ambaye kwa wakati huo alikuwa msomi mzuri na cheo cha Luteni akiwa na wasomi wengine kama Sarakikya aliyepangiwa batallion ya Tabora na Nyirenda aliyepandisja Mwenge mlima kilimanjaro siku ya Uhuru.Huyu Luteni Elisha Kavana alifanya ziara katika nchi za Kenya na Uganda na inasemekana alifanya ushawishi ktk majeshi wakati huo ya hizi nchi kugoma na kuasi ili kuboresha huduma za majeshi kwasababu kulikuwa hakuna tofauti ya maisha kabla na baada ya uhuru.Kwa mfano vitanda katika barrack vilijengwa na cement na unapewa blanketi mbili, moja kama godoro na lingine la kujifunika.

Hapo Colito Barracks ambayo ndiyo Lugalo ya sasa jina lililotokana na vita kali na Mjerumani Chifu Mkwawa huko Iringa ndipo uasi ulipoanzia kwa kuwa arrest baadhi ya raia na maofisa wa jeshi wazungu kwa wakati huo.Pamoja na kuwa majina ya maofisa waliofanya uasi yamewekwa ktk kumbukumbu za siri sana lakini ndipo Sarakikya alipoteuliwa kuwa mkuu jeshi la Tanganyika Rifles kabla ya kuundwa kwa JWTZ akihofiwa kuwa asije kuwa ameanzisha uasi huko Tabora ktk Batallion na hata Elisha Kavani kupandishwa cheo kutoka Luten kuwa Meja na haya yalifanywa na Oscar Kambona kushirikiana na Nyerere.
 
Back
Top Bottom