Mgomo UDSM waota mbawa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Ule mgomo uliokuwa ukinukia na kutangazwa mitandaoni kuwa ungetokea UDSM umeota mbawa.Ilielezwa kuwa mgomo huo ungekuwa usio na kikomo na ulilenga kupinga kucheleweshwa kwa malipo ya fedha za kujikimu za wanafunzi wa UDSM. Ulipangwa kuanzia eno maarufu kama 'Revolutionary Square' na kusambaa sehemu mbalimbali za chuo na Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Nikiwa UDSM leo,nimeshuhudia hali ikiwa ni ya utulivu na kila mwanachuo akiendelea na ratiba yake ipasavyo. Kitivoni Sheria, uchaguzi wa Viongozi wa Jamii ya Wanafunzi wa Sheria UDSM (UDLS-University of Dar es Salaam Law Society) ulikuwa ukiendelea.

Taarifa zinaonesha kuwa wanachuo wote waliokwisha saini malipo ya pesa zao tangu Jumatatu,Jumanne na Jumatano wameanza kulipwa.Taratibu nyingine za malipo hayo zinaendelea. Katika viunga vya Revolutionary Square,hali ni tulivu kabisa na hakuna hata dalili ya mahali hapo kutumika kwa hivi karibuni. Nyasi ndefu zimeshuhudiwa mahali pa kusimama viiongozi pamoja na madimbwi ya maji mahali ambapo wanapaswa kusimama wasikilizaji.

Hakuna tena mgomo UDSM na masomo yanaendelea kama kawaida.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Hakuna mgomo uliofanikiwa tz. Wanaojua mgomo ni wakenya.
 
2006 -2010... hichi kipindi daah.. sitasahau..

2006/2007 mgomo wa 60% na boom kutoka 3500-5000..mwezi mmoja nyumbani
2008/2009... means test... huu ni noma..zaid miezi zaidi ya miwili nyumbani..na vitisho juu
sijui kama kuna mgomo mwingine mkubwa zaidi ya hii hapo mlimani.. ambayo imetokea baadae ya 2010 mpaka sasa nijuzeni...

na yote tulifanikiwa.. maisha yote niliyoishi hapo niliona hii ndio best approach ya kudeal na watawala na uongozi wa chuo.. kwa mafanikio...pongezi kwa mtatiro ... na jamaa wote wapambanaji kipindi hicho ....
 
2010-2013 mgomo uliomtetemesha shukuru kawambwa eneo la swimming pool udsm kudai kulipwa 10000 badala ya 5000 wakatupatia 7500 na ffu kupigwa mawe sana chini ya wanaharakati baada ya uongozi wa daruso kuwa vibaraka wa watawala mkuruma hall ilionekana kuwa ndogo ndipo ushauri wa wanaharakati kuongoza msafara kwenda uwanja mkubwa wa mpira udsm ili watu wote wapate nafasi ya kumsikiliza waziri aliyesemekana kuwa wa elimu mpaka sasa.Alitetemeka na kupatwa na kigugumizi maana alikuwa amezungukwa na wanafunzi kila pande wakimtaka ataje 10000 tu na si kitu kingine.
 

Hivi ushawahi kujionea hii Makitu? Kwa kweli Chama chako kimetupeleka kuzimu

http://www.youtube.com/watch?feature=player_detailpage&v=QjvV8HGGXvI
 

sitakaa kusahau baada ya pale sisi wanaharakati wachache tuliitwa na kupewa barua za kusimamishwa masomo na baadae kufukuzwa chuo.......
 

Yumkini nimesoma na wewe na tumepitia hilo sekeseke umenikumbusha mbali mkuu
 
Yumkini nimesoma na wewe na tumepitia hilo sekeseke umenikumbusha mbali mkuu

Itakuwa tu kamanda ndio nyakati zetu za kina mtatiro na silinde owawa bwana mdogo nassari..na wengine wengi hasa wale wababe wa COET..
 
Itakuwa tu kamanda ndio nyakati zetu za kina mtatiro na silinde owawa bwana mdogo nassari..na wengine wengi hasa wale wababe wa COET..

Unaikumbuka re-admission? Unaenda kwa mwenyekiti wa mtaa, mtendaji, bomani kwa mkuu wa wilaya na malipo juu, acha bwana migomo ilikua those days.
 
Unaikumbuka re-admission? Unaenda kwa mwenyekiti wa mtaa, mtendaji, bomani kwa mkuu wa wilaya na malipo juu, acha bwana migomo ilikua those days.

Hahaha umenikumbusha kitu yaani yale mafomu ..mimi mwenyekiti wa mtaa alizingua eti anijui ikabidi ni mtoe daah acha re admission geti maji ndio unaingia na polisi wa kutosha ..
Unakumbuka UCLAS/ARDHI..? huu mgomo..walikaa zaidi ya semista nyumbani 2008/2009 ilikuwa balaa
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…