VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Ule mgomo uliokuwa ukinukia na kutangazwa mitandaoni kuwa ungetokea UDSM umeota mbawa.Ilielezwa kuwa mgomo huo ungekuwa usio na kikomo na ulilenga kupinga kucheleweshwa kwa malipo ya fedha za kujikimu za wanafunzi wa UDSM. Ulipangwa kuanzia eno maarufu kama 'Revolutionary Square' na kusambaa sehemu mbalimbali za chuo na Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Nikiwa UDSM leo,nimeshuhudia hali ikiwa ni ya utulivu na kila mwanachuo akiendelea na ratiba yake ipasavyo. Kitivoni Sheria, uchaguzi wa Viongozi wa Jamii ya Wanafunzi wa Sheria UDSM (UDLS-University of Dar es Salaam Law Society) ulikuwa ukiendelea.
Taarifa zinaonesha kuwa wanachuo wote waliokwisha saini malipo ya pesa zao tangu Jumatatu,Jumanne na Jumatano wameanza kulipwa.Taratibu nyingine za malipo hayo zinaendelea. Katika viunga vya Revolutionary Square,hali ni tulivu kabisa na hakuna hata dalili ya mahali hapo kutumika kwa hivi karibuni. Nyasi ndefu zimeshuhudiwa mahali pa kusimama viiongozi pamoja na madimbwi ya maji mahali ambapo wanapaswa kusimama wasikilizaji.
Hakuna tena mgomo UDSM na masomo yanaendelea kama kawaida.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam