Wanafunzi wa Chuo Kikuu huria cha Tanzania Makao Makuu, Kinondoni Dar es salaam, wameziba mlango wa kutokea wa block D, ambayo yaonekana ndilo jengo la utawala wanadai mikopo, wanasema hawaondoki mlangoni mpaka kieleweke. Viongozi wanaohusika na jambo hilo wamefika kuongea nao lakini walikuwa wanatoa majibu mepesi, hivyo wanafunzi wapo kimtazamo wa kuanzisha timbwili. Nimeondoka pale walio karibu waendelee kutujuza. Ila hadi naondoka FFU hawakuwepo ila mgambo wa Chuo walikuwa wanalinda viongozi.