Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,209
- 4,769
Naweza kusema kwamba, tunahatua kubwa sana kujifunza kutoka kwa majirani zetu Kenya! Kodi na ama ongezeko lolote la kikodi litokanazo na bidhaa, humlenga moja kwa moja mlaji na siyo mfanya biashara!
Kwa upande mwingine, maandamano ya majirani zetu, ni sahihi na siyo haya ya wafanyabiashara wa Kariakoo!
Kwa kawaida, mfanyabiashara huwa halipi kodi! Kwa sababu, asipouza hawezi kudaiwa kodi
Anapouza ndio hulazimika kulipa kodi, maana yake, anayekuja kununua ndiye anayelipa kodi zote, na mfanyabiashara kazi yake ni kupeleka kodi iliyotokana na njaa ya mlaji, kazi ya mfanyabishara, hufanya hesabu kabla ya kuanza kuuza bidhaa zake ili apate ya kodi ya pango, TRA, na gharama zoote ili abakiwe na faida yake
Nadhani hesabu zinawavuruga hawa wafanyabiashara, badala ya kukaa, kisha kuona ni kwanamna ipi itawalazimu kuongeza bei kwenye kila bidhaa ili wao wabaki na faida zao na maumivu ya kodi hizo anabaki nazo mlaji wao wanaweka mgomo, huo mgomo hauwahusu hata chembe
Huo mgomo iliwapasa watumia bidhaa (Walaji) ndiyo waandamane na ama kugomaa kula ili iwe sawa siyo kwa mfanyabishara kugoma, huo ni upuuzi na kuchelewesha wajinga kupata akili, wananchi wakionja joto ya jiwe ndo wataamua wao kugoma na ama wavumilie maumivu ya sera mbovu za viongozi wao mafisadi wa CCM
Nikimuuliza mfanya biashara anachogomea ni kipi, hana jibu kulingana na kwamba, yeye ni wakili tu wa serikali kuwasilisha kodi kwauaminifu kutoka kwa watumiaji bidhaa
Fungueni maduka na mpandishe bidhaa ili kama yupo wa kuandamana, aandamane mwananchi mtumiaji bidhaa