Mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo ni fedheha kwa Serikali

Mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo ni fedheha kwa Serikali

Kichwamoto

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Posts
3,403
Reaction score
4,692
Hii aibu ya huu mgomo ni kubwa sana na inafikirisha sana, je, hayo madeni ya Kodi ni bambikizi, ni penalty, na fitina ni nini hasa?

DG wa TRA yupo, Waziri wa Fedha yupo, Waziri wa Biashara yupo, kwanini haya madeni? Yapi halali na yapi haramu? Je, hii italeta mazoea ya kukwepa Kodi au mazoea ya kubambikia Kodi, au itakatisha tamaa? TRA wataonekana ni chombo uchwara.

Kama ni funika kombe mwanaharamu apite, kuponya majeraha, tugange yajayo, yote haya ifahamike.

Biashara ni nguzo, biashara ni uchumi, biashara ni Maisha, mlishe ng'ombe akupe maziwa tarajiwa, weka mazingiara rafiki ili upate kodi, weka kodi rafiki nchi iende mbele.

Usipogaagaa na upwa wali mkavu hupati.

Tuendelee na Imani.

Kichwamoto nimerejea.
 
Back
Top Bottom