Mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo umewafumbua macho Watanzania. Mnatakiwa kugoma kwa uonevu wa CCM unaoendelea sasa

Mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo umewafumbua macho Watanzania. Mnatakiwa kugoma kwa uonevu wa CCM unaoendelea sasa

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Wafanyakazi mnateseka sana isee. Mshahara ukitoka tu tar 23 baada ya wiki mnahaha kukopa madukani na kwenye baa.

Mnatakiwa kupinga kodi na tozo za hovyo kwa kugoma ili serikali iwasikilizie kama wafanyabiashara wa kariakoo.

Wafanyabiashara nyie ndio mnaumia kila siku. Tozo na kodi kibao. Mbaya zaidi pesa zinaliwa na wanaCCM wachache.

Watanzania kwa ujumla wanatakiwa wagome. Maana migomo ndio suluhu ya serikali fisadi na kandamizi.
 
Umekatisha usingizi Wako kwa Andiko La Kipuuzi Na Hivyo Kama Hili?

Rudi Usingizini Halafu Watu Wengine Ni Wa Hovyo Sana Yaan Kitendo Cha Kumiliki Smartphone Unajiona Unajua Kila Kitu. Shame!

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Wagome bila sababu??? Njia pekee ya watZ na binadamu kwa ujumla kugoma ni kugusa 'mifuko' yao basi
..
 
Unagoma huna sababu za msingi? Halafu wafanyakazi mianya mingi sana ya malupulupu sasa ugome yanini?
 
Migomo kuna wakati haisaidii kitu kwa sababu za "intimidation or divide and rule" hivyo wadhulimiwa kujikuta wamegawanyika na kukosa msimamo mmoja. Suluhisho ni kuwa na katiba mpya ambayo itawaweka watu wote katika fursa na adha zinazofanana.

Ni lazima masuala yote ya makato ya kodi, mafao, malupulupu n.k. yaainishwe kupitia sheria moja isiyokuwa na ubaguzi kati ya watawala na watawaliwa. Haiwezekani viongozi wawe na sheria yao maalum katika masuala ya utumishi wao wa umma ambayo haiendani na wafanyakazi wengine.

Mathalani, huwezi kuacha kuwatoza kodi eti kwa kuwa wao ni viongozi tu hali wakilipwa mishahara mikubwa na yenye malupulupu kibao, ama kuwa na utaratibu wa kuwalipa mafao makubwa vipindi vyao vifupi vya mikataba yao ya kazi kumalizika, ama kuwalipa posho za vikao pale wakiwa katika majukumu yao, n.k. Kama suala la kikokotoo liwe moja kwa watumishi wote, kama kujilipa posho kwa vikao vya kazi iwe kwa watumishi wote, la sivyo ondoa hii kitu mara moja.

Ni jambo la ajabu sana hili la kuwa "double standard & treatments" katika masuala yahusuyo "statutory payments". Viongozi wala hawaoni aibu ya kuishi maisha ya anasa na huku wakijiwekea sheria za kuwawezesha kukwepa kulipa kodi, kujipa malupulupu yenye kufuru kubwa huku wafanyakazi wengine wengi wakiishi katika lindi kubwa la ufukara!
 
Wafanyakazi mnateseka sana isee. Mshahara ukitoka tu tar 23 baada ya wiki mnahaha kukopa madukani na kwenye baa.

Mnatakiwa kupinga kodi na tozo za hovyo kwa kugoma ili serikali iwasikilizie kama wafanyabiashara wa kariakoo.

Wafanyabiashara nyie ndio mnaumia kila siku. Tozo na kodi kibao. Mbaya zaidi pesa zinaliwa na wanaCCM wachache.

Watanzania kwa ujumla wanatakiwa wagome. Maana migomo ndio suluhu ya serikali fisadi na kandamizi.
Sawa kamanda mchomvu,tuko pamoja,sawa waongoze na unaona unafaa kuwatetea leo,ila miaka yote ya awm5 hukuona ilifaa kuwatetea🤔
 
Back
Top Bottom