Migomo kuna wakati haisaidii kitu kwa sababu za "intimidation or divide and rule" hivyo wadhulimiwa kujikuta wamegawanyika na kukosa msimamo mmoja. Suluhisho ni kuwa na katiba mpya ambayo itawaweka watu wote katika fursa na adha zinazofanana.
Ni lazima masuala yote ya makato ya kodi, mafao, malupulupu n.k. yaainishwe kupitia sheria moja isiyokuwa na ubaguzi kati ya watawala na watawaliwa. Haiwezekani viongozi wawe na sheria yao maalum katika masuala ya utumishi wao wa umma ambayo haiendani na wafanyakazi wengine.
Mathalani, huwezi kuacha kuwatoza kodi eti kwa kuwa wao ni viongozi tu hali wakilipwa mishahara mikubwa na yenye malupulupu kibao, ama kuwa na utaratibu wa kuwalipa mafao makubwa vipindi vyao vifupi vya mikataba yao ya kazi kumalizika, ama kuwalipa posho za vikao pale wakiwa katika majukumu yao, n.k. Kama suala la kikokotoo liwe moja kwa watumishi wote, kama kujilipa posho kwa vikao vya kazi iwe kwa watumishi wote, la sivyo ondoa hii kitu mara moja.
Ni jambo la ajabu sana hili la kuwa "double standard & treatments" katika masuala yahusuyo "statutory payments". Viongozi wala hawaoni aibu ya kuishi maisha ya anasa na huku wakijiwekea sheria za kuwawezesha kukwepa kulipa kodi, kujipa malupulupu yenye kufuru kubwa huku wafanyakazi wengine wengi wakiishi katika lindi kubwa la ufukara!