Hii ishu iko ki mkakati sana tofauti na watu wengi wanavyodhani.
Sasa hivi dunia yote ni ya moto, ukienda Kenya maandamano, ukija bongo mgomo,ukiangalia pale kati yukrein pamewaka, ukichunguza kidogo unamuona putin yupo na kiduku mpaka wanaendeshana kwenye limousine ,ukimcheki mchina anaitaka Taiwan 🇹🇼 huku siasa za chuki zinahubiriwa kuhusu muungano.
Muda huu majasusi wengi wapo kazini, hii ni vita ya dunia ndio inapiganwa tactically , haya mambo hayatokei kwa bahati mbaya, sijui mapinduzi Burkina 🇧🇫 sio kwamba yametokea bahati mbaya, kuna watu wamekaa wanacheza na dunia kama vile wanacheza draft.
Ni kama vile Russia 🇷🇺 labda huwaambia nato,mkimpa yukrein silaha mie natengeneza machafuko kwa nchi washirika wako halafu ninawapa options za kuja kujiunga upande wangu.
Ndio maana mnaona dunia imechangamka kama mdomo uliokula pilipili, hakuna sehemu inapoa, leo huku hivi kesho kule vile.
Hawa jamaa wanazicheza vita zao kwenye nchi zetu(kama watu anavyocheza draft) na ni kitu rahisi sana kwao.
Wanajua na minds zetu,wanajua watanzania kwa maandamano ni wagumu, hawa tunawapa bomb la muungano very complicated.