Mgomo wa wafanyakazi na wananchi utakuwaje?

Mgomo wa wafanyakazi na wananchi utakuwaje?

Bando la wiki

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2023
Posts
911
Reaction score
3,017
Nawaza endapo wafanyakazi na wananchi kwa ujumla watajoini mgomo wa wafanyabishara unaoendelea hivi sasa nchini hali itakuwaje!!?

Madai ya wafanyakazi;
1.Kupinga kanuni za kikokotoo cha mafao yao.
2. Kupinga kanuni za PAYE zinazokota mishahara yao moja kwa moja huku makato hayo kuto reflect hali zao za mishahara.
Kupinga mishahara kiduchu
3. Kupinga mifumo mingi kama PEPMIS inayolazimishwa kwa watumishi pasipo semina elekezi namna ya kutumia mifumo hiyo.

Madai ya wananchi;
1. Kupinga mfumuko wa bei kwa bidhaa muhimu
2. Kupinga tozo kila eneo hasa kwenye miamala ya simu huku wabunge wao wakituma pesa bure kabisa.
3. Kupinga serikali kutowawajibisha wezi wa mali za umma kwa ushahidi wa ripoti za CAG.
4. Kupinga suala la muungano ambapo hivi sasa watanganyika wanataka muungano huo kujadiliwa upya.
5. Kupinga serikali kuchelewesha upatikanaji wa katiba mpya ili hali mali na rasilimali za nchi zinaendelea kuibiwa na kakikundi kadogo huko juu.

Nadhani kutachimbika nchi hii
 
Back
Top Bottom