Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

Najua si wote, ni mamluki wachache wanaowachafua wapiganaji wa UDOM walioko nasi.

Poleni sana, hizo ni changamoto zinazoikabili hii nchi karibu kila chuo. Jitahidi ujumbe ufike kwa watanzania wote.

Ila kwenu hapo, inabidi huo moto muendelee nao ikiwezekana hao wasaliti wenu wanaojipendekeza CCM wapeni onyo.

Mapambano yaendeleee vijana hakuna kurudi nyuma!! Mapinduzi halisi yeyote yale katika nchi yeyote ile, HUANZIA VYUO VIKUU.
 
Wamemgomea nani.....??? JK waliyemchangia kuchukuwa fomu au .......... au ................. au ......... mi siwaelewi.....ni bora ile milioni mgewapa hao waleta maji ili wawaletee maji....................thatha mtakunywa na kuoga jeuri yenu
 
Salaam wana JF,
kweli nimekubali mfamaji haachi kutapata, sasa watawala wa Udom na serikali wanaitaja na kuisingizia CHADEMA kwamba ndio wanachochea migomo chuoni Udom na hususani mgomo huu wa wanataaluma wa chuoni hapo.

makamu mwenyekiti wa UDOMASA (chama cha wanataaluma Udom) ametumiwa jumbe mbali mbali za kuonyesha kwamba wanatumiwa na Chadema na kwamba hawana madai ya msingi (uongo uliokithiri). Na mwanataaluma huyo alisoma hiyo sms mbele ya wantaaluma wenzake.

soma moja ya sms hii . " tunajua mnatumiwa na Chadema kufanya hayo mnayofanya". Hii ni ajabu kabisa kutapatapa badala ya kushughulikia madai yao ya msingi. M/mweyekiti huyo alisema atawapeleka mahakamani wote waliomtumia jumbe hizo na atawashitaki wathibitishe madai yao kama yanaukweli.

Sasa kila muv ya kudai haki tanzania chadema wanahusishwa hata kama hawapo kabisa kwa nini? Bt nafurahi sana kwa sababu ccm bila kujua wanaipa umaarufu Chadema kwamba hakuna haki tanzania bila Chadema.

my take,
uongozi na serikali acheni zengwe shughulikieni madai ya msingi ya wananchi acheni kuisingizia upinzani hususani Chadema.
 
Sisiyemu washanyea kambi.., njia pekee ya kuisafisha Sisiyemu ni kupelea almost nusu ya top layer ya uongozi Segerea mkulu akiwa ndani..,
Ni mtazamo tu wajameni, msinipige mawe :tongue::tongue:
 
CCM ni sawa na timu ya mpira wa miguu ambao wakifungwa siku zote makosa huwa si ya kwao.

Watasema alikuwa ameotea, au refa kawapa goli, au wamechezesha vijeba, sisi hatuna uzoefu, wao ni profeshenoz na sababu lukuki.

Ukiona haya yanatokea Tambua saa na wakati wa Ukombozi umekaribia.
 
Nafurahi kweli kuona kila kitu ni chadema.
Maana kuna siku waziri kombani alisema eti chadema ndio wanacheleweshea maendeleo wananchi, nikawaza chadema ndo wana rimoti control ya na ccm wanasubiri waambiwe cha kufanya na CDM.

ANANGALAU UDOM MMEANZA KUKUA MAANA MEMBE ALIWAAIDI KUWA HATAKI KUONA HOJA YA MIKOPO INAFANYWA AJENDA NA WAVAA MAGWANDA MKASHANGILIA.
 
Namshauri huyo m/mwenyekiti akifungua kesi kuhusu hilo jambo awataarifu uongozi wa Chadema nao wafungue kesi ya kusingiziwa na kudhalilishwa.
 
It's useless for the sheep to pass resolutions in favour of vegetarians while the wolf remains of a different opinion. Anonynous
 

ndg yangu ni kweli Udom kwa sasa wananitia moyo sana, ila ndio hivyo chadema wanasingiziwa wapo nyuma yao kwa muv wanazofanya
 
Na bado,
Sasa watahangaika kupangua kashfa ngapi? Dowans anatumwa ngeleja, sijui kashfa ya arusha Tambwe hiza, kufanya vibaya kwenye uchaguzi mkuu mchawi Tido mhando. Kila siku ni kutafuta namna ya kupangua kashfa, shughuli za maendeleo watafanya lini?
Hiyo ni ishara kuwa 2015 ni chadema dolani.
 
ndg yangu ni kweli udom kwa sasa wananitia moyo sana, ila ndio hivyo chadema wanasingiziwa wapo nyuma yao kwa muv wanazofanya

kama umekomaa haungalii wanachokufanyia wale wasio upande wako ni vita vya msituni type."ambaye hayupo upande wako ni adui"

nashangaa sana ndugu dr.nyaoro wa udasa umekaa kimya mbona kwenye xenophobia/chauvinism ya south africa udasa mlitoa tamko fasta
 
Hayo madai ni madai gani? Kwa nini hao wanataaluma hawafungui kesi mahakamani ? Au wanalengo ya kuchafua jina la UDOM na mafanikio ya serikali kujenga Chuo Kikuu kizuri kwa muda mfupi tu ?
Naushauri uongozi wa UDOM uchukue hatua za kisheria dhidi ya hao wanataaluma wa UDOM wanaleta "migomo-siasa" ambayo haifuati sheria za kazi za Tanzania. Mfanyakazi ana haki ya kugoma, lakini utaratibu unaeleweka kisheria. Ninavyofahamu chama cha wanataaluma sio chama cha wafanyakazi (Trade Union) kinachoweza kuitisha mgomo. Hata kama wanataaluma wamefikia uamuzi wa kugoma lazima wafuate sheria za kazi.
Huu utamaduni wamigomo isiyofuata sheria ni kansa mbaya sana inayotafuna utawala wa sheria. Imefikia wakati sheria za kazi zitumike dhidi ya migomo-siasa na hao wanataaluma watakuwa ni mfano mzuri sana wa utawala wa sheria.
 
ccm Vilaza wengi bado nasisitiza jamani fanyeni kazi ya kusolve hayo matatizo acheni kuingiza chadema hata kwenye mambo ya msingi hapo ndo mnaonekana akili zenu ndogo ccm! mnakamatika padooogo TATIZO AKILI ZENU ZOOTE ZIMELALA KWENYE UFISADI DABALA YA KUENDELEZA CHAMA NA NCHI! kweli nyinyi ni sikio la kufa.
 
craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap
 
na nyinyi si mnaua basi tuuueni wooote wabaki wanenu tu! SIKILIZENI MATATIZO YA WATU KABLA YA KUFIKA KWENYE MIGOMO! HAKUNA MGOMO UNAOKUJA KAMA RADI, MIGOMO HUFANYIKA KAMA IMESHINDIKANA MAZUNGUMZO! JAMANI CCM AMKENI!!!
 
CHADEMA wasichafuliwe na migogoro ya UDOM, tatizo UDOM wamekasirika, wamekimbiza fomu za mkulu nchi nzima kipindi cha kupata wadhamini, leo mkulu kawashiti, zile ahadi zote hazijatekelezwa, mara atawapa uwakilishi kwenye NEC mara atahudumia vizuri chuo, waaaapi? ile ilikuwa danganya toto. Nao wasomi lakini hawakutafakari kuwa wanaingizwa mjini na kuachwa kwenye mataa. Nani anawajali UDOM sasa, CCM wamepata nchi, wanakula nchi yao, acha wagawane za DOWANS, za epa, kigoda, meremeta, zilishakwisha zote.
 

nashukuru sana kwa mchango wako mzuri ndg yangu, ni kweli Udasa inabidi watoe tamko kupinga kabisa unyanyasaji huu wa serikali.
 

udom haiwezi kuchafua chama chochote cha siasa ila inavyoonekana udom ndio inachafuliwa.
Ukweli wa mambo unazidi kudhihirika.
Ukificha moto moshi utakuumbua.
 

naamini unaupungufu wa kufikiria ndg yangu, kwa taarifa yako wanataaluma wana haki kabisa ya kugoma kwa kufuata utaratibu wa kisheria.

kabla ya kugoma wahadhiri wa Udom walitafuta ushauri wa kisheria kudai haki zao. Kwa hiyo wewe unashabikia dhuluma? Unataka watu wawe wananyonywa na wakae kimya? Acha ushabiki ndg yangu, kama serikali imejenga chuo kizuri kwa gharama nyingi mbona haiwajali watumishi wake?

kama wewe unamaisha mazuri kwa kupata haki zako zote, waache wenzako watafute haki zao kama njia za kawaida zimeshindikana, mgomo ni alternatives, na hawa ni wasomi wamefuata sheria zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…