Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

na nyinyi si mnaua basi tuuueni wooote wabaki wanenu tu! SIKILIZENI MATATIZO YA WATU KABLA YA KUFIKA KWENYE MIGOMO! HAKUNA MGOMO UNAOKUJA KAMA RADI, MIGOMO HUFANYIKA KAMA IMESHINDIKANA MAZUNGUMZO! JAMANI CCM AMKENI!!!

hapo umenena mkuu, wanatakiwa kushugulikia matatizo mapema sio mpaka yaharibike mambo
 
Namsubiri Tambwe Hiza atoe tamko kulaani mgomo!
 
CHADEMA wasichafuliwe na migogoro ya UDOM, tatizo UDOM wamekasirika, wamekimbiza fomu za mkulu nchi nzima kipindi cha kupata wadhamini, leo mkulu kawashiti, zile ahadi zote hazijatekelezwa, mara atawapa uwakilishi kwenye NEC mara atahudumia vizuri chuo, waaaapi? ile ilikuwa danganya toto. Nao wasomi lakini hawakutafakari kuwa wanaingizwa mjini na kuachwa kwenye mataa. Nani anawajali UDOM sasa, CCM wamepata nchi, wanakula nchi yao, acha wagawane za DOWANS, za epa, kigoda, meremeta, zilishakwisha zote.

hapana ndg yangu, usiwahukumu kwa past, angalia wanayoyafanya sasa. Kwa taarifa za uhakika, uongozi wa juu wa Udom umechaguliwa ki ccm lakini wanataaluma na wafanyakazi wake wengi hawana mlengo wowote wa kisiasa zaidi ni wanamageuzi.

nadhani itakuwa busara kuwaunga mkono kuliko kuwashambulia sana kwa mambo ya zamani na ndg yao Mkwere, sasa wamepevuka na wanahitaji changes.

mbona Udsm mkuu wake Prof. Mkandala na wengine ni washabiki sana wa ccm lakini hatukibrand kama chuo cha chama? Udom ndio mageuzi yanaanza kwani hakina hata miaka mitano, tuwape mawazo positive ya kuwafanya wawe na mtazamo chanya daima kama wasomi wanavyopasa kuwa.
 
Hakuna mgomo wa wahadhiri UDOM. Ila kuna extended meeting,ambapo wahadhiri wamedhamiria kuwa na mikutano endelevu mpaka pale madai yao yatakapotekelezwa.
 
Mtanganyika licha ya kujaliwaa uvumilivu pia amejaliwa uzembe wa kutenda,sasa anapo amua kujitahidi kutenda ndipo wanyonyaji wanapoanza kutafuta wakumlaumu.
CCM na serikali yao hawaamini kama UDOM wanaweza kudai haki zao bila kushawishiwa.
 
Kama chadema ndo wanachochea mgomo wa UDOM basi ndo hao hao watakua wametafuna pesa za waalimu na wanafunzi wa udom. Naiomba serikali iunde tume ya kuwachunguza chadema kwa ufisadi walioufanya.
 
Hakuna mgomo wa wahadhiri UDOM. Ila kuna extended meeting,ambapo wahadhiri wamedhamiria kuwa na mikutano endelevu mpaka pale madai yao yatakapotekelezwa.

sasa ndg yangu, huo si ndio mgomo wenyewe wameupa jina hilo ili kujiepusha na mabomu ya machozi. Kama mgomo haupo mbona darasani hawaingii kufundisha? Mi naona waendelee kuipa presha serikali mpaka madai yao yatimizwe
 
Kama chadema ndo wanachochea mgomo wa UDOM basi ndo hao hao watakua wametafuna pesa za waalimu na wanafunzi wa udom. Naiomba serikali iunde tume ya kuwachunguza chadema kwa ufisadi walioufanya.

hahahahaa! Hii nimeipenda mkuu, kweli wamechanganyikiwa hawa. Badala ya kuwatatulia matatizo wanabaki kulaumu vyama vingine,. Sasa wameshikwa pabaya hawa
 
Wanachama wa udasa wengi wao wamepikwa na kuiva vizuri. Lakini kuna baadhi ya wanakidharau Udom, wakiwa wanafundisha utasikia wakisema ukitaka A nenda Udom, watakukumbembeleza na kukufaulisha. Nafkr hayo siyo ya kushkamana nayo, maana wengi wa wanataaluma udom ni product ya mlimani. Hivyo ikiwa mtoto anagawa maksi na kubembeleza basi ni wazi kuwa ndivyo baba alivyomlelea.

Pia kwa upande mwingne kulaumu vyama kuwa ndivyo chanzo cha migomo na migogoro sio kweli. Dukuduku, adha, umaskn, shda za watanzania zimeshkamanishwa na chadema pale anapoibuka mtu au kundi la watu kudai na kutetea haki na maslahi yao. Hivyo, sio vema kukituhumu chama kisa tu kina sera zinazofanana na madai ya wanyonge wanaonyongwa na kundi la wevi wasio na huruma. Ni vema kuusimamia ukweli, mkifanya madudu yakubalini na kutafuta namna ya kuyaondoa.
CCM kama chama na sera zake hakina shida, sera zimenyooka tena saaafi na zinamtetea mwananchi wa kawaida. Hivyo tatizo sio chama bali ni baadhi ya watu ndani ya chama waliogeuza kuwa mtaji wao binafsi. Hawa watu, miungu watu, makachero, nondo mla watu, mazimwi na mafsadi (ashakhumu si matusi) ndio wanaofanya chama kionekane jangwa lisilo maji wala aina yeyote ya uhai. Kundi hili la watu limewafanya watanzania hasa vijana kuhisi kichefuchefu pale wanapoona rangi ya kijani na njano au wanapomsikia Kapteni Komba akiimba CCM eee yajenga nchi%. Hasira zinawaka ndani yao maana nchi haijengwi bali maisha ya watu binafsi na familia zao ndiyo yanayojengwa.
Ccm ilikubalika sana enzi za nyerere na wenzake, hata ndani ya chama kwa sasa wako watu wanaokubalika sana. Hivyo basi chama ka chama havina tatizo bali wanachama wachache ndani ya chama ndio chanzo cha shda na umaskn tz.
Mungu ibariki tanzania, tuokoe na ufisadi na umaskini wa fikra na kipato.
nashukuru sana kwa mchango wako mzuri ndg yangu, ni kweli Udasa inabidi watoe tamko kupinga kabisa unyanyasaji huu wa serikali.
 
Kutoka dodoma mjini:tayari wauwaji wameshawanyunyizia upupu na mabomu ya machoz wanachuo,hali si shwari.
 
Kutoka dodoma mjini:tayari wauwaji wameshawanyunyizia upupu na mabomu ya machoz wanachuo,hali si shwari.
 
Namsubiri Tambwe Hiza atoe tamko kulaani mgomo!

anaweza huyu kuja kukurupuka na kulaani mgomo, tena umemsahau babu Makamba, sijui safari hii atalaani kwa kutumia mitishamba ya kipagani mana maandiko matakatifu kesha maliza yote.
nahisi hata Marry Chatanda atakuja kulaumu viongozi wa dini hata huu mgomo, hawachelewi hawa.
 
Kutoka dodoma mjini:tayari wauwaji wameshawanyunyizia upupu na mabomu ya machoz wanachuo,hali si shwari.

Watatumaliza mwaka huu. Mpaka kikwete aondoke madarakni tumekwisha.

Dawa yao inakuja washenzi hawa
 
Salaam wana JF,
kweli nimekubali mfamaji haachi kutapata, sasa watawala wa Udom na serikali wanaitaja na kuisingizia CHADEMA kwamba ndio wanachochea migomo chuoni Udom na hususani mgomo huu wa wanataaluma wa chuoni hapo.

makamu mwenyekiti wa UDOMASA (chama cha wanataaluma Udom) ametumiwa jumbe mbali mbali za kuonyesha kwamba wanatumiwa na Chadema na kwamba hawana madai ya msingi (uongo uliokithiri). Na mwanataaluma huyo alisoma hiyo sms mbele ya wantaaluma wenzake.

soma moja ya sms hii . " tunajua mnatumiwa na Chadema kufanya hayo mnayofanya". Hii ni ajabu kabisa kutapatapa badala ya kushughulikia madai yao ya msingi. M/mweyekiti huyo alisema atawapeleka mahakamani wote waliomtumia jumbe hizo na atawashitaki wathibitishe madai yao kama yanaukweli.

Sasa kila muv ya kudai haki tanzania chadema wanahusishwa hata kama hawapo kabisa kwa nini? Bt nafurahi sana kwa sababu ccm bila kujua wanaipa umaarufu Chadema kwamba hakuna haki tanzania bila Chadema.

my take,
uongozi na serikali acheni zengwe shughulikieni madai ya msingi ya wananchi acheni kuisingizia upinzani hususani Chadema.
hii safi kama haki is equated to CHADEMA.....ni sawa wanaipa CHADEMA hadhi yake mahsusi!
 
Hayo madai ni madai gani? Kwa nini hao wanataaluma hawafungui kesi mahakamani ? Au wanalengo ya kuchafua jina la UDOM na mafanikio ya serikali kujenga Chuo Kikuu kizuri kwa muda mfupi tu ?
Naushauri uongozi wa UDOM uchukue hatua za kisheria dhidi ya hao wanataaluma wa UDOM wanaleta “migomo-siasa” ambayo haifuati sheria za kazi za Tanzania. Mfanyakazi ana haki ya kugoma, lakini utaratibu unaeleweka kisheria. Ninavyofahamu chama cha wanataaluma sio chama cha wafanyakazi (Trade Union) kinachoweza kuitisha mgomo. Hata kama wanataaluma wamefikia uamuzi wa kugoma lazima wafuate sheria za kazi.
Huu utamaduni wamigomo isiyofuata sheria ni kansa mbaya sana inayotafuna utawala wa sheria. Imefikia wakati sheria za kazi zitumike dhidi ya migomo-siasa na hao wanataaluma watakuwa ni mfano mzuri sana wa utawala wa sheria.

we wawapi?mwaka jana UDASA waligoma pale UDSM,hadi warioba akaenda kuwasikilza,na hawakugoma cku1,so unataka sheria gani?hadi wanapofikia hatua ya kugoma,ujue wameshafata taratibu,pale kuna ma-loya wanajua nin wanafanya.
Pili usizungumze lyk bar-maid,hawa watu ni kweli madai yao wameyasotea na hayatekelezwi,wakat watu wa kada nyngne kama politicianza mambo yao huenda smooth,lakini pia utambue kuwa hawa ndio wanaowazalisha wataalam,je wakiwapa makasa itakuaje?je wahadhri hawana mahtaji yao,kwanini serikal inawazngua,ACHA KUHOROJOKA AZ IF UNAVUTA GOZO,ina maana m2 akidai haki yake,siasa,eh mbona hzo difence mekanizm mbovu
 
Mwaka huu CHADEMA tutasingiziwa mengi sana maana kila baya kwa CCM hutupiwa kwetu. Sasa kwa nini wasitendee tu haki wananchi maana wakulima nao watakapogoma kwa kunyimwa mbolea shauri ya itikadi zao kisiasa nacho tutasukumiwa tu huku.

UDOM kudai kwenu kile kilicho cha haki wala msifanyiwe ghiliba. Kuhenya mhenye madarasani na good-time wale wengi tu, nani kasema hivyo??
 
Salaam wana JF,
kweli nimekubali mfamaji haachi kutapata, sasa watawala wa Udom na serikali wanaitaja na kuisingizia CHADEMA kwamba ndio wanachochea migomo chuoni Udom na hususani mgomo huu wa wanataaluma wa chuoni hapo.

makamu mwenyekiti wa UDOMASA (chama cha wanataaluma Udom) ametumiwa jumbe mbali mbali za kuonyesha kwamba wanatumiwa na Chadema na kwamba hawana madai ya msingi (uongo uliokithiri). Na mwanataaluma huyo alisoma hiyo sms mbele ya wantaaluma wenzake.

soma moja ya sms hii . " tunajua mnatumiwa na Chadema kufanya hayo mnayofanya". Hii ni ajabu kabisa kutapatapa badala ya kushughulikia madai yao ya msingi. M/mweyekiti huyo alisema atawapeleka mahakamani wote waliomtumia jumbe hizo na atawashitaki wathibitishe madai yao kama yanaukweli.

Sasa kila muv ya kudai haki tanzania chadema wanahusishwa hata kama hawapo kabisa kwa nini? Bt nafurahi sana kwa sababu ccm bila kujua wanaipa umaarufu Chadema kwamba hakuna haki tanzania bila Chadema.

my take,
uongozi na serikali acheni zengwe shughulikieni madai ya msingi ya wananchi acheni kuisingizia upinzani hususani Chadema.

Hakika; CCM na Serikali yake inayoporomoka kila kukicha wanajua kuwa CHADEMA ni sauti ya Umma na chechote umma unachoamua ni kauli isiyo na utata kwa maslahi ya Taifa. Kama hao CCM wapo ili kukidhi maslahi ya mafisadi na ndio maana wanashindwa kushughulikia Maslahi na shida za wanajamii, inabidi wajue kuwa uadui wanaoujenga hautajionyesha ktk majukwaa ya siasa pekee bali ktk nyanja zote za kijamii katika taifa hili maana Umma wa watanzania upo kila mahali. Na pia watanzania wote wanazidi kufumbuka macho kila kukicha maana Chadema imeshafichua kila kitu kuwa ni kwanini nchi ni maskini, inaongozwa vibaya na inazidi kudidimia kutokana na mafisadi wachache!

Hivyo kimsingi, CCM na Serikali yake wanapominya na kudhoofisha haki ya wananchi walioko ktk fani yoyote, wajue kuwa watajutia matokeo yake, iwe haki na madai yanaanzishwa na CHADEMA kama mwanga kwa Taifa au taasisi au idara zenyewe. Yote hii ndio nguvu ya Umma, na umma unaanza kujitambua kila kukicha. Iwe inatokea UDOM, UDSM, au taasisi nyingine yoyote! Wote wameshaamua, Hakuna tena kudanganywa!

Ni wale tu waliokwishakata tamaa, ndio watakubali kuendelea na uozo na usanii uanoonekana kwa viongozi karibu wote ndani ya serikali na taasisi zake.

My Take:
Chadema ni chama cha Umma, na nguvu ya umma. Kwa hivyo umma unapotekeleza au kupigania haki zake toka ktk nyanja au taasisi zozote, hata kama wapo nje ya Chadema, lazima CCM na serikali yake wahangaike na kutapatapa maana wanajua ukombozi unapatikana na hawana tena nguvu ya kuziba au kuzuia lolote. Ndio kwanza kunapambazuka!
 
naamini unaupungufu wa kufikiria ndg yangu, kwa taarifa yako wanataaluma wana haki kabisa ya kugoma kwa kufuata utaratibu wa kisheria.

kabla ya kugoma wahadhiri wa Udom walitafuta ushauri wa kisheria kudai haki zao. Kwa hiyo wewe unashabikia dhuluma? Unataka watu wawe wananyonywa na wakae kimya? Acha ushabiki ndg yangu, kama serikali imejenga chuo kizuri kwa gharama nyingi mbona haiwajali watumishi wake?

kama wewe unamaisha mazuri kwa kupata haki zako zote, waache wenzako watafute haki zao kama njia za kawaida zimeshindikana, mgomo ni alternatives, na hawa ni wasomi wamefuata sheria zote.

Naona hata wewe hujui taratibu za kugoma kwa mujibu wa sheria. Kwanza walioitisha mgomo ni chama cha walimu kinachoitwa UDOMASA. Kisheria hii si Trade Union, ni pressure group tu. Jana waliwafukuza viongozi wa RAAWU ambao ni Trade Union inayotambulika kisheria. Hawa jamaa ni kama watoto wadogo. Inatia aibu sana kuona wanataaluma wanafanya mambo hovyo hovyo. Huko UDOM kumejaa ushabiki tu. Na wasipoangalia hao viongozi wao ndio watakaoishia kuburutwa mahakamani na kufukuzwa kazi.

Wanataaluma wanashindwa hata na wafanyakazi wa reli ambao wengi wao elimu yao ama ya shule ya msingi, ngumbaru na wachache sekondari. Inaudhi sana kuona wanaojiita wanataaluma wanahemukwa tuu bila kujua mustakabali wao. Waambieni ndugu zenu waache utoto.
 
King Suleiman said:
huo si ndio mgomo wenyewe wameupa jina hilo ili kujiepusha na mabomu ya machozi. Kama mgomo haupo mbona darasani hawaingii kufundisha!
Hiyo ni term iliyokaa kiteknikali. Na term inaweza badilika kadiri siku za kudai madai zinazopoongezeka. Mfano kesho wanaeza kutumia terms ka academic seminar au workshop. Kijuujuu unaeza kuuita mgomo,ila kitaalamu zaidi huo sio mgomo,kwani hauna features za mgomo.
 
Back
Top Bottom