Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

Hana hoja ana majibu ya kisiasa tu huyo solidality iko palepale hasa kwa wahadhiri.
 
Issue ya kutokuwepo kwa semina kwa baadhi ya kozi siyo issue ya msingi. Mwalimu anweza kuvunja semina akazigawa marks kwenye assignment nyingine kufuatana na mazingira yenyewe labda hayo madai mengine yatakua ya msingi.
 
LICHA ya kuwepo kwa taarifa kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakutana na wadhahiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, wahadhiri hao wameendelea kuchachamaa wakisisitiza kwamba subira yao imefikia ukingoni sasa wanajiandaa kwenda mahakamani kutafuta haki yao.


Wahadhiri wa chuo hicho wamekuwa katika mgomo kuingia madarasani kufundisha kwa kile wanachodai kuwa wanadhulumiwa viwango vya mishahara wanavyolipwa na serikali.

Akizungumza na Mwananchi, Naibu Katibu mkuu wa chama cha wahadhiri hao (Udomosa), Peter Kokeli alisema juhudi zao kubwa wamezielekeza katika kuhakikisha wanapata haki zao.Kokeli alisema wamekuwa na mategemea kuwa Rais Jakaya Kikwete atalitatua suala hilo lakini tayari wameanza hatua za kwenda mahakamamani.

Licha ya kuahidi kwamba wako tayari kuzungumza na Pinda, alisema suala hilo ni kosa la jinai kwa sababu wamegunduia kwamba kumekuwa na tabia ya kughushi slipu zao za mishahara."Wahadhiri wamesikitishwa sana na taarifa hizi za uongo.

Tunapenda kuweka wazi kuwa mishahara mipya iliyoletwa chuoni ni sawa na ngazi ya mishahara iliyolipwa pia kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kwa mfano Tutorial Assistant (PUTS 12), kwenye vyuo vyote viwili imekuwa Tsh 1,248,070/=, lakini menejimenti ya UDOM imekata mishahara hiyo.

"Wahadhiri wamebaini nyaraka za ndani ya chuo Kikuu cha Dodoma zikionyesha kuwa mishahara mipya imeletwa na kimsingi hazina makosa yoyote kwa wanataaluma," alisema Kokeli.

Alieleza pia kusikitishwa na kauli ya Makamu mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula, aliposema kuwa wahadhiri wamekosa uelewa na madai yao si ya msingi, akisema kuwa kauli hiyo imelenga kuwadhalilisha, hivyo wamemtaka aiombe radhi jumuiya hii ya wanataaluma wa UDOM.

"Tunapenda kuweka wazi kuwa madai yetu ni ya msingi sana na pia ni stahiki za msingi na za kisheria. Makamu Mkuu wa Chuo ajibu hoja na si kueneza propaganda zisizo na msingi wowote" alisema KokeliLakini kwa upande wake, Profesa Kikula alisisitiza kuwa taarifa zake ni za kweli na kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda chuoni hapo leo ili kutoa maelezo kamili ya madai hayo. "Kesho (leo) Waziri mkuu atakuja hapa chuoni kueleza mambo yote wanayolalamikia.

Lakini pia kuna mkaguzi wa serikali anayefanya ‘special auditing' (ukaguzi maalum) kuanzia wizarani, atakuja hapa Jumatatu kutoa maelezo yake. Ukweli wote utajulikana," alisema Profesa Kikula. Akizungumzia hatua ya wahadhiri hao kufungua kesi mahakamani, Profesa Kikula alionyesha kutokutishwa na hatua hiyo.

"Mahakama zipo waache waende tu. Jana nimetoa matangazo ya ujio wa Waziri Mkuu. Nimetoa pia tangazo la mkaguzi wa hesabu za serikali. Sasa kama wao wanakwenda mahakamani, mimi siwezi kuwazuia.

Taarifa zote tunazo, mimi sizungumzi tu, natumia takwimu" alisisitiza Profesa Kikula. Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kwamba Pinda akiwasili leo anatarajia kukutana na wahadhiri hao na kutoa msimamo wa serikali.Akizungumza kwa niaba ya Wahadhri hao, Peter Kokeli ambaye ni kaimu katibu wa umoja huo alisema kuwa moja ya mambo ambayo wangependa Waziri Mkuu afahamu maelezo ya ufasaha kuhusu madai yao.

Alisema kuwa wako tayari kupokea maelekezo yoyote kuhusiana na kazi yao kutoka kwa Pinda kwa kuwa wanamtambua kuwa ni kiongozi wao tena mwenye heshima lakini si katika suala la kudanganywa kuhusu malipo.
Ujio wa Waziri MKuu unaweza kuwa neema kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakimhitaji kwa muda mrefu lakini kwa upande wa wahadhiri itakuwa bado ni kilio kwani wao wanamhitaji rais mwenyewe.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Profesa Kikula, Pinda pamoja na mambo mengine anatarajia kuzungumza na wanafunzi wa UDOM pia pamoja na kukagua miradi ya chuoni hapo ikiwemo majengo pamoja na mifumo ya maji.

Kokeli alisema kuwa Wahadhiri wana mashaka kuwa suala lao ni kama moja ya vitu ambavyo Waziri Mkuu atakuwa akivijadili lakini halitiliwi uzito mkubwa kutokana na ukweli kuwa hata katika mlolongo wa mambo ya kufanya liko katika ajenda ya nne.

"Unaweza kuona ni namna gani kuwa Waziri Mkuu hakupanga kuzungumza na sisi kwani hata katika ajenda sisi tumewekwa nafasi ya nne ni kama yaliyomo, lakini tumekubaliana kwa pamoja kuwa lazima tutakutana na kiongozi wetu huenda akawa na maagizo kutoka ngazi ya juu yake lakini tutapenda atuambie lini tunalipwa pesa zetu na si vinginevyo" alisema Kokeli.

Kiongozi huyo alisema katika maombi na malengo yao wanatarajia kumuona Rais Jakaya Kikwete akiingia katika viwanja hivyo na kukaa meza moja na wahadhiri hao ili kilio chao kiweze kufika mahali panapotakiwa na kwamba uwepo wa Pinda inawezekana ukawa ni kwa ajili ya wanafunzi.

Katibu huyo alisema wamekubaliana kuiburuza menejimenti ya Chuo mahakamani kama wataona haki yao haiipatikani na wanaiomba serikali ikubali kumtuma mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Ili afanye ukaguzi wa mali za Udom ikiwemo masuala ya fedha.

Katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja kumekuwa na mfululizo wa migomo na maandamano ya wanachuo wa Chuo hicho wakishinikiza kuonana na Waziri Mkuu huku wahadhiri wao walioanza mgomo mwanzoni mwa wiki wakitaka kuonana na Mkuu wa nchi.

Dai kubwa la walimu hao ni kupunjwa kwa mishahara yao kunakofanywa na uongozi wa Udom kwa kile walichokiita kuwa ni uchakachuaji mkubwa ndani ya menejimenti ya utawala na fedha chuoni hapo.

Wahadhiri hao walisema kuwa hawana shida na Hazina kwani mishahara yao inaonyesha kuwa imekuwa ikitumwa vizuri lakini tatizo lipo ndani ya uongozi wa chuo wenyewe ambao wanashindwa kulipa mishahara kama ilivyotumwa na Hazina.

Tatizo lingine ni pamoja na kutolipwa kwa fedha za kujikimu tangu walipoajiliwa ambao wengine wanazaidi ya miaka mitatu lakini hawajui ni lini watalipwa fedha za kujikimu kama wahadhiri wa vyuo vingine.Mwisho


hapo kwenye red kikula anaongea tu lakini anajua wazi hakuna pa kutokea wahadhiri wamewashika pabaya hiyo ni kauli ya mfa maji.....
 
Nilisoma taarifa ya UDOMASA,hapahapa jf,inaonyesha watumish wa udom ni vibarua,halaf ni taasis inayoendshwa kibabe haswa,msomi mwenye taaluma amegeuka m2mwa?ah!WHO Z MLACHA?yani ye ndo anasumbua vjana wasisome,kama chuo hakikua tayari mlikianzishia nini,kama c vherehere?
 
hapo kwenye red kikula anaongea tu lakini anajua wazi hakuna pa kutokea wahadhiri wamewashika pabaya hiyo ni kauli ya mfa maji.....

Hivi inawezekana kweli kikula ameshiriki kwenye kula hizo fedha?
 
Mi binafsi ctegemei solution kutoka kwa mzee pinda. Jamaa ni mwoga kufanya maamuzi na kama atathubutu basi yatakuwa kipolitics zaidi. Mtoto wa mkulima ana uzalendo WENye kutiliwa mashaka coz usalendo sio kuöngea2 na kulia michozi. Vitendo vinahusika sana! 2mckilizie lakn..,
 
Hapana kaka cha kukueleza ni kwamba pinda kweli kaja na muda wa saa nane alikuwa hapa social science na kuelekea medicine kukagua majengo huku akiwasaliti college ya education na kuwapita barabarani lakini nikueleze kuwa wanafunzi hao waliweka mawe makubwa njiani katika kuhakikisha kuwa wanampata pinda lakini akala kona na wakafanikiwa kumteka mkuu wa wilaya na vigogo wengine ambao hadi sasa wapo wanawaimbia na kusisitiza kuwa hawataachiwa had pinda je kuwanusuru.mkuu wa mkoa dr,engineee msekela ambaye anachukiwa sana na wanafunzi wa udom kwa kuamuru wapigwe mabomu katika mgomo wao wa hivi karibuni alionja joto ya jiwe baada ya wananfunzi kulala mbele ya gari yake hapa social science na kumzomea akiwa karibu kabisa na mlacha ambaye wanafuzi wameendelea kumwimbia waziri mkuu kuwa lazima aondoke na mlacha ampelekee kikwete akamwajiri kukaa mapokezi ikulu ndogo ya chamwino.
 
Hapana kaka cha kukueleza ni kwamba pinda kweli kaja na muda wa saa nane alikuwa hapa social science na kuelekea medicine kukagua majengo huku akiwasaliti college ya education na kuwapita barabarani lakini nikueleze kuwa wanafunzi hao waliweka mawe makubwa njiani katika kuhakikisha kuwa wanampata pinda lakini akala kona na wakafanikiwa kumteka mkuu wa wilaya na vigogo wengine ambao hadi sasa wapo wanawaimbia na kusisitiza kuwa hawataachiwa had pinda je kuwanusuru.mkuu wa mkoa dr,engineee msekela ambaye anachukiwa sana na wanafunzi wa udom kwa kuamuru wapigwe mabomu katika mgomo wao wa hivi karibuni alionja joto ya jiwe baada ya wananfunzi kulala mbele ya gari yake hapa social science na kumzomea akiwa karibu kabisa na mlacha ambaye wanafuzi wameendelea kumwimbia waziri mkuu kuwa lazima aondoke na mlacha ampelekee kikwete akamwajiri kukaa mapokezi ikulu ndogo ya chamwino.

Hili tatizo linakuwa ni la kifamilia sasa itabidi kikwete amuondoe tu huyo jamaa mie nadhani ndio solution hali itatulia kidogo then suala la waalimu nadhani wakikaa nao linasolvika ila hawa wahusika ingekuwa vizuri sana wangetangazwa kwenye vyombo vya habari tukawajua ili wasiweze kuajiliwa tena mahala popote pale sababu ni wezi wameiba mishahara ya waalimu kweli inauma ila mkuu wa nchi nae amekaa kimya sana tunashangaa kwanini kawa kimya hivi?
 
Wewe Teroburu kwanza unajua maana ya neno Pathetic au umekurupuka kutoka kwa mlacha saiv kakutuma uje uandike hizi crap?
Ngoja nikupe darasa kidogo.

Meaning of Pathetic:
(a.) Affecting or moving the tender emotions, esp. pity or grief; full of pathos; as, a pathetic song or story.

(a.) Expressing or showing anger; passionate.


Watu wamekuja na hoja zao nzito unasema Pathetic reason? Unasema uliwaona wahadhiri, then unasema 'kama wale niliowaona ni wahadhiri', huna uhakika hata na unachokiongea, wewe ni kilaza, na nakushauri ujiunge na mwaka wa kwanza next september, crap!

Hili jamvi nahisi limeingiliwa. Great thinkers are no more thinking. Ni Matusi kwenda mbele
 
Mi binafsi ctegemei solution kutoka kwa mzee pinda. Jamaa ni mwoga kufanya maamuzi na kama atathubutu basi yatakuwa kipolitics zaidi. Mtoto wa mkulima ana uzalendo WENye kutiliwa mashaka coz usalendo sio kuöngea2 na kulia michozi. Vitendo vinahusika sana! 2mckilizie lakn..,


Hii ni ukweli kabisa.
Mie binafsi sioni kama kuna hatua au hata tamko lolote la maana kutoka kwa Pinda. Huyu mheshimiwa yupo tu kama picha ya ukutani. Sijui ni nani amemwambia asitumie mamlaka yake.

Wasomi wa UDOM, nafikiri hatua ya kumleta Pinda mnaweza kuijutia. Ikumbukwe yeye ni top top authority. akiwaambia mrudi kazini msubiri uchunguzi sijui mtafanyaje...??
 
Wadau mpaka sasa hali ni tete toka alivyokuja Pinda, haijulikani nini kinaendela, ila bado watu wanamsubiri hapa chimwaga
 
Kwa upande wa CoED wameshapindua uongozi wao wa UDOSO na hawako tayari kusitisha mgomo.
 
kama sinema vile pinda amefika udom na ving'ora vyake kwenye ukumbi ili aongee na wahadhiri wa udom kuhausu mgomo wao wahadhiri wamegoma kuingia kuongea naye wanamtaka rais sio pm kuona hivyo pinda akajinda kwenda kuongea na serikali ya wanachuo hali wanachuo waliisha kubaliana kuwa aongee na wanachuo wote basi wakati pinda anaongea na viongozi huku wanachuo wakakutana na kuwang'oa madarakani haraka wakasimika serikali mpya wakamwapisha rais mpya na mawaziri wapya hapo patamu serikali yetu imechanganyikiwa huku makamba yuko arusha,mbeya kunafukuta.kila kona ya nchi yetu wananchi wameivimbia serikali naona ya tunisia yanakaribia DOWANS,ARUSHA,UDOM.KATIBA.UDSM nasikia j3 wanaanza kugoma,IRINGA,KIU sasa wameelemewa
 
tunashukuru kuja ila isitumike siasa katika kutatua matatizo yetu sisi wanafunzi.
 
Waliomba wenyewe kuwa viongozi na wanalipwa mshahara. ach wapate shida. usanii umewazidi.
 
Tupe yaliyojiri UDOM baada ya pinda kukataliwa kuongea nao.....nini kimejiri zaidi??
 
Mbona thread nyingine inasema wahadhiri walimsubiri chimwaga lakini pinda akachelewa na kuomba radhi na kuwataka wakutane kesho sa tano?????? wewe unasema wamegoma kuongea nae sasa tuamini lipi?????????????
 
Mtoa mada naona hayuko kwenye eneo la tukio, au anatoa mada hii makusudi kuchanganya watu, itapendeza kama atarudi hapa kufafanua zaidi
 
Back
Top Bottom