Habari nilizozipata sasa hivi kuhusiana na ishu ya Serikali na Mwanahalisi:-
1. Serikali yaani wizara ya habari ilimtumia barua leo asubuhi Kubenea, # ISC/N/100/1/Vol.11 ikitaka awajibu haraka sana, kuhusiana na habari ilizoziita ni za uchochezi against viongozi wakuu, hasa rais, Lowassa, na Rostam na pia mtoto wa rais.
2. Kubenea aliwajibu saa moja baada ya kupata ujumbe huo wa serikali katika barua namba M/http/MC/001/15, kwamba wanaiomba serikali kuwapa muda zaidi hadi Jumatatu, kutokana na Kubenea leo kutingwa sana na kesi mahakamani ile ya Tindikali, lakini serikali ilikataa katika barua # ISC/N/100/1/Vol.12 na kumpa hadi saa tisa na nusu mchana kujibu, Kubenea ikabidi akaamua kuwajibu haraka kuwahi hiyo time.
3. Majibu ya Kubenea yamewafikia serikali saa tisa mchana, ikiwa ni only nusu saa kabla ya muda ulitolewa na serikali kama a dealine. Briefly the dataz ni kwamba:-
Kubenea amejibu kwamba Mwanahalisi, hawajui ni lini serikali iliwahi kuweka wazi kisheria mahali ambapo uhuru wa media unapoanzia na kuishia, na kwamba gazeti hilo halijawahi kujaribu kuwagombanisha rais na mtoto wake, isipokuwa ukweli uko wazi kwamba huyu kijana amekuwa akitumiwa na kina Lowassa na Rostam na kwamba kitendo cha Mwanahalisi kujaribu kulinganisha hali ya siasa ya Tanzania na ile ya Mbeki kule SA, ni suala la mtizamo tu wa kisasa na hakuna uvunjwaji wa sheria at all. Pia Kubenea amewakumbusha wizara hiyo kwamba Mwanahalisi watakua more than happy kukutana na serikali on hii ishu kwenye sheria, ambako ndipo pekee wanapotakia kisheria, kutoa ushahidi walionao kulingana na habari walizoziandika, ambazo wanazo.
My Take:
Hapa the sagga inaelekea kuzuri, according to the dataz ni kwamba Ridhiwani amekua akimnadi kwa nguvu sana huko behind the scene, mgombea wa Lowassa na Rostam, anayeitwa Beno hili halijawahi kwua siri na limesemwa sana na magazeti, sasa kama Ridhiwani anamanadi mgombea wa Lowassa si ndio maana yenyewe ya kutumwia nao, au?
According to more dataz ni kwamba Muungwana alishashituka na hili la kutumiwa kwa mtoto wake, kwa hiyo last two weeks amemhamishia huyu mtoto wake kwenye nchi moja huko majuu kwa excuse ya kwenda kusoma ingawa the goal ni kumficha kabsia to the public,
Leo umoja wa wanawake, walijaribu kumtishia Kubenea, lakini the dataz ni muungwana kuingilia kati na kuwakaripia kwua wakae pembeni, sasa sisi wananchi tumekaa mkao wa kula tunasubiri kuona kama serikali itaenda kwenye sheria ili ukweli owte uwekwe wazi. Huko Tarime mambo ni magumu sana kitendo cha katibu wa Tanga kuingia Chadema kimezidi kum-depress muungwana, hasa kutokana na the fact kwamba kimtokea kwa sababu ya kijana kukataa kukumbatia ufisadi ndani ya CCM,
Kwa kweli tunampongeza sana huyu kijana, viongozi wengi wakuu wa CCM, leo wamekua wakitabiri mwisho wa Makamba na ukatibu.
Ahsante Wakuu, Mods Iki-exipre naomba iunganishwe mara moja. Tutaendeela kuhabarishana maana sasa hivi kuna movemmentnyingi sana ambazo tunazi-monitor na tutaleta dataz hapa as soon as zikipatikana.