Mgongo,kiuno nyonga vinanitesa

Mgongo,kiuno nyonga vinanitesa

Showme

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
1,251
Reaction score
498
Wanajf nisiwapotezee muda,nasumbuliwa na hivyo vitu tajwa hapo juu,mwenye kujua chanzo cha matatizo kama hayo aje aeleze hapa,mbarikiwe wote.
 
Umri wako?una Watoto as Umewahi kuzaa?
 
Jambo la msingi nakushauri uende Hospitali ili ukaonane na Daktari na ufanyiwe vipimo sahihi kwa wakati muafaka kabla ugonjwa haujawa sugu.
 
Nimeenda sana lakini nafuu napata kwa siku chache,labda niende hospitali kubwa.
 
Pole sana Dada Zamda Geuka. Hilo ni tatizo Dogo sana, kama hutojali nakukalibisha PM nikuelekeze nn cha kufanya.
 
Last edited by a moderator:
Nunua boga, kisha likate vipande vidogo vidogo pamoja na mbegu zake, vianike juani hadi vikauke. Vikikauka visage au vitwange hadi viwe unga laini. Tafuta bakuli au chupa ya kuhifadhia.

Nunua asali, kisha chukua kijiko kimoja cha unga wa boga changanya na maji ya uvuguvugu, kisha ongeza vijiko viwili vya asali koroga na furahia juisi ya boga, pata juisi mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni, kwa wiki mbili.

Kama hali haikubadilika nenda hospitali wakufanyie vipimo, mara nyingi tatizo lako linasababishwa na kupungua kwa ute kwenye pingili za uti wa mgogo, kwenye magoti na kenye maungio ya kiuno. Boga hurejesha ute kwa haraka kuliko aina nyingine za tiba.
 
Pole Dada. Kama walivyoshauri wana JF nenda hospital ukapime na utapata majibu. Lakini ni matatizo sugu kwa watu wenye umri mkubwa kwa umri wako itabidi waone wataalamu zaidi wakueleze sababu. Lakini kama huko hospital umeshindwa njoo tukuonyehe njia au tiba mbadala.itakusaidia.tumewasaidi na wengine pia. unaweza wasiliana nasi. +255 689 417 472
 
Pole sana Dada Zamda Geuka. Hilo ni tatizo Dogo sana, kama hutojali nakukalibisha PM nikuelekeze nn cha kufanya.

Nawashukuru wote kwa ushauri,nilipewa barua ya rufaa kuja muhimbili MOI-Orthopaedic department nimepewa vipimo vingi kesho ndo nitapata majibu.
 
Last edited by a moderator:
Nunua boga, kisha likate vipande vidogo vidogo pamoja na mbegu zake, vianike juani hadi vikauke. Vikikauka visage au vitwange hadi viwe unga laini. Tafuta bakuli au chupa ya kuhifadhia.

Nunua asali, kisha chukua kijiko kimoja cha unga wa boga changanya na maji ya uvuguvugu, kisha ongeza vijiko viwili vya asali koroga na furahia juisi ya boga, pata juisi mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni, kwa wiki mbili.

Kama hali haikubadilika nenda hospitali wakufanyie vipimo, mara nyingi tatizo lako linasababishwa na kupungua kwa ute kwenye pingili za uti wa mgogo, kwenye magoti na kenye maungio ya kiuno. Boga hurejesha ute kwa haraka kuliko aina nyingine za tiba.

Asante sana majimoto nikirudi nyumbani nitaufanyia kazi ushauri wako,napenda sana matibabu ya asili,asante.
 
Back
Top Bottom