Mgongo unaniuma sana toka nijifungue.

Mgongo unaniuma sana toka nijifungue.

Machuchu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2017
Posts
1,260
Reaction score
965
za leo.

Ni miaka mitano (5) sasa mgongo unaniuma sana tena mno. Wengi waliniambia kwa kua umetoka kujifungua, na nilijifungua kwa njia ya kawaida. kuna miaka mi2 nyuma uliacha sasaiv umeludia tena wengi walisema ni godoro, kuna siku nilienda kwa wifi yangu nikakaa siku4 nikasema ngoja nione kama ni godoro ila hali ikawa ni vilevile.

Je, dawa nini nikandwe tena na maji ya moto? Kuna mama mtu mzima aliniambia ata panadol nisiwe nameza wenyew utatulia ila alinishauli niwe naoga maji ya vuguvugu mda wowote.

NB: Nina mtoto mmoja tu.
 
Pole mwaya! Nenda Kwa daktari umuone, ufanye vipimo, Kisha atakupa Dawa na huenda ukatakuwa kufanya Mazoezi Kwa muda mrefu! Zaidi ya miaka 5 umekaa bila kwenda hospitali [emoji87][emoji87] sasa hivi ungeshapona zamani ingebaki unahadithia tu Watu kuwa uliwahi umwa mgongo! Usipuuze kwenda kumwona daktari!
 
Wengine wanasema ukianza mapenzi mapema baada ya kajifungua inaweza kuwa chanzo cha mgongo kuuma! Nikisema mapema namaanisha ndani ya mwezi mmoja! Wengine husema ukianza kufanya kazi mapema baada ya kajifungua pia husababisha maumivu hayo! Yaani hata wiki haiishi umeanza kufua, kufagia, kudeki nk.

Je haya yote hukufanya? Kama hukufanya au hata kama ulifanya muone daktari kwa msaada wa kitabibu. Unaweza kuta ni tatizo la uti wa mgongo

Sent from Moto G
 
Mapenzi nilianza kufanya baada ya 40 jioni....ila swala la kufanya kazi nilianza baada ya 40 pia nilikua sina msaidizi baada ya 40 waliondoka.
 
za leo.

Ni miaka mitano (5) sasa mgongo unaniuma sana tena mno. Wengi waliniambia kwa kua umetoka kujifungua, na nilijifungua kwa njia ya kawaida. kuna miaka mi2 nyuma uliacha sasaiv umeludia tena wengi walisema ni godoro, kuna siku nilienda kwa wifi yangu nikakaa siku4 nikasema ngoja nione kama ni godoro ila hali ikawa ni vilevile.

Je, dawa nini nikandwe tena na maji ya moto? Kuna mama mtu mzima aliniambia ata panadol nisiwe nameza wenyew utatulia ila alinishauli niwe naoga maji ya vuguvugu mda wowote.

NB: Nina mtoto mmoja tu.
Shemeji pole sana kwa maumivu.Jaribu yafuatayo
1.Epuka godoro lenye kubonyea katikati.Tumia godoro gumu au jembamba ili mwili ulale umenyooka.
2.Uwe unafanya mazoezi ya kujinyoosha nyumbani ili misuli yako ya mgongo iimarike
3.Kama unaweza kwenda kufanya physiotherapy kama Muhimbili ni vema
4.Maumivu yakiwa makali sana unaweza kutumia dawa za maumivu kama panado na diclofenac
5.Epuka kuinua vitu vizito wakati umeinama.
6.Iwapo maumivu yatazdid kuongezeka ni vema ukamuone daktari akufanyie kipimo cha xray au CT Scan.
 
Mapenzi nilianza kufanya baada ya 40 jioni....ila swala la kufanya kazi nilianza baada ya 40 pia nilikua sina msaidizi baada ya 40 waliondoka.
Pole Dada, kwa ratiba hiyo naona ni matatizo tu ya mgongo.. Waone madaktari kwa ushauri na matibabu.

Sent from Moto G
 
Hio hata mie inanitokea nikikaa sana sehemu akati wa kuinuka au nikiinama sana hioilitikana nanilipojifungua kabla sijapona nikaanza na kazi za kuinama hilo mwanzo huoni tatizo ila miaka inavyoenda ndo unaona shida yake ninamiaka 5 tokea nimejifungua ila mgongo unaniuma hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mwaya. Nenda hospital upate uhakika wa unachoumwa na nini ufanye. Kukisia kisia haitakusaidia. Onyo: usibebe mimba kabla ya kupona. Utaongeza tatizo juu ya tatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom