Mgonjwa aliyelazwa kwa miezi mitano atoa Tuzo kwa Wauguzi wa Wodi Namba 6 katika Taasisi ya MOI

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mgonjwa aliyekuwa amelazwa wodi namba 6 “A” katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ametoa tuzo maalum ya kuwapongeza wahudumu wa wodi hiyo kwa huduma bora wanazotoa kwa wagonjwa.


Mgonjwa huyo Godfrey Mushy alilazwa wodini hapo kwa miezi Mitano kuanzia Oktoba, 15, 2022 kutokana na kupata mivunjiko ya mifupa sehemu mbalimbali za mwili (Polytrauma) na kuruhusiwa Februari 2023 baada ya afya yake kutengamaa.

Katika tuzo yake hiyo, Mushy ameandika "WAPENDWA WAUGUZI WA WODI NAMBA SITA ‘A”

“Nataka kuelezea kuguswa kwangu na huduma zenu bora mlizonipa katika kipindi chote nilichokaa hapo. Upendo wenu wa hali ya juu kwa kuiona kila hatua ya maisha ni muhimu.

Nawashukuru kwa huduma zenu! Asanteni kwa kujitoa katika safari hii ya pamoja.

Kwa pamoja tunawapongeza nyie wote! Mikono yenu ya kuponya na mionyo yenu ya kujali ni baraka za kweli kwa mnaowahudumia.

Asanteni kwa juhudi zenu za bila kuchoka na jitihada zenu za kutoa huduma kwa upendo wa hali ya juu.

Kutoka ndani ya mioyo yetu Bwana na Bibi G. Mushy”

Wauguzi wa wodi hiyo wamemshukuru mteja wao na kwamba tuzo hiyo imewafariji na kuwaongezea hari ya kutoa huduma bora zaidi.
 
Familia hii imeonyesha mfano wa kuigwa dhidi ya kina sisi tuliojawa kibri na malalamiko yasiyokwisha kwa kada hii iliyotelekezwa kimaslahi.

Tujiulize wapo kada ya afya wenye kujishasha kama wale wajiitao wasomi kwenye mambo ya siasa?

Wapo kada ya afya wenye kujimwambafy na majumba, magari mazito mazito au mali kama wanasiasa au zile kada nyingine?

Si kuwa kada hii inafahamu kwa vitendo kuwa kama binadamu tu vulnerable kiasi gani?

Tuweni na subira ndugu zangu. Tuweni humble. Tuweni wacha Mungu. Tuweni wenye hofu na Mola. Tuweni wenye shukurani.

Duniani hapa tu wasafiri tu. Kwa Mola hakika tutarejea. Wala hatuna muda mrefu.
 
kama kumbkumbu ziko vizuri ward no 6 MOI ni VIP.....!!! Kuna huduma zote muhimu na nurse wako.
Ila wauguzi wa MOI wanajitahidi piaa pongezi kwao
 
Aisee huu ujumbe na huu moyo wa familia ya bwana na bibi Mushi umenifanya machozi yanilengelenge.
 
Pongezi kwake kwa kuonyesha njia, kuliko kuendelea kutoa 'tips' bar na kwingineko, sasa ni muda muafaka kwa wengine kutoa 'tips' kwenye hii kada inayopigania uhai wetu.
Utakuta mtu kafanyiwa upasuaji wa moyo na akapona, ata ile tu kusema asante ni shida; tuwaheshimu sana hawa wataalamu, na kwa kazi wanazofanya hawatakiwi kulalamika shida; kwao nyumba na magari vinatakiwa viwe ni vitu vya kawaida.​
 
Ni miongoni mwa watanzania wachache ambao wapo positive na kua na mwoyo wa kuappriciate wengine.........
Sijaribu kuwa negative ila ukichunguza kwa undani zaidi ni lazima mgonjwa yupo vizuri kiuchumi. Ithibati ipo hapo kwenye hiyo tuzo. Si kwamba ni ghali sana ila uwepo wa akili ya kutoa/kutengeneza tuzo kunaendana na hali ya kipato pia.

Sio kwamba Tanzania kuna huduma mbovu, ni kwamba Tanzania kuna huduma kulingana na uwezo wako wa kifedha na influence yako ama ya wale unaowajua. Kinyume na hapo utafanywa kama tambara la deki.

Nilichoandika hapo juu hakiondoi utu wake wa kushukuru pale aliporidhishwa japo kipato/influence yake nina yakini vilikuwa na mchango mkubwa katika huduma aliyopata.
 
Usiwe pessimistic mkuu mimi nawewe hatujui kipato chake, huwezi kumuhukumu kwamba ni pesa, watanzania wengi hata masikini hata kuseme thank you sir/madam hatuna kabisa tunaona ni haki kuhudumiwa vizuri.......kazi yetu ni lawama kukosoa kutukana kukejeli.
 
Kama tuzo hiyo haiwezi kubadilishwa kuwa hela wauguzi wakagawana. Basi huo ni ush.uzi tu.
 
Call it pessimism, I call it facts. Sijaondoa credit ya mtoa shukrani wala ufanisi wa walioshukuriwa but I had to look at it on a reality point of view and the probable factors that might have facilitated the good care.

Ignoring a problem doesn't magically make it inexistent. We have one of the messed up and biased healthcare system in the world, that is a fact especially in Government facilities. Deep down inside your heart you know what I'm talking about. But for the sake of seeming right you will refuse.
 
Call it pessimism, I call it facts. Sijaondoa credit ya mtoa shukrani wala ufanisi wa walioshukuruwa but I had to look at it on a reality point of view.

Ignoring a problem doesn't magically make it inexistent.
Being appreciative its heart not wealth, mkuu, neenda hotel kubwa uone wateja wa kitanzania kama wana toa tips hata ahudumiwe je hawatowi chochote, wageni hata wenye uwezo wa kawaida ata muambia muhudumu to keep change........kwa hiyo my stand is wealth of some one has nothing to do with being appreciative to good service.
 
Let's agree to disagree and we both remain with our opinions/views.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…