Majestic wolf
JF-Expert Member
- Feb 10, 2015
- 1,248
- 1,851
Katika hali isiyo ya kawaida na ya kutisha sana mgonjwa mmoja nchini Kenya afanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya "non-invasive treatment for swelling".
Uzembe huu wa ajabu uliofanywa na madaktari bingwa nchini humo umepelekea kusimamishwa kazi kwa wafanyakazi wanne wa hospitali hiyo ya "TAIFA".
Uzembe huo uligundulika masaa kadhaa ndani ya chumba cha upasuaji baada ya kumpasua mgonjwa wa watu kisha kukuta hana "blood clot" walioitegemea kuikuta. Katika hali ya kushangaza madaktari wenza wamepinga uamuzi wa kuwasimamisha kazi "wazembe hao" wakitetea maslahi yao.
Ikumbukwe kuwa hospitali hii ndio iliyokumbwa na kashfa ya mtoto mchanga "kutekwa" pia na kashfa chafu ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wamama wajawazito.
Uzembe kama huu ulishawahi kutokea miaka mingi huko nyuma Muhimbili na ni ajabu kwa uzembe huu kujitokeza miaka hii ya karibuni katika nchi iliyo na uchumi mkubwa zaidi East Africa
I saw this on the BBC and thought you should see it:
Kenya doctors 'perform brain surgery on wrong patient' - Wrong patient given brain surgery