Nehemia Kilave
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 1,414
- 3,118
Haya ni maendeleo makubwa katika sekta ya Afya.
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imemuaga Faith Mwinula (9), ambaye ni mtoto wa kumi na nne kupona ugonjwa wa selimundu baada ya kupandikizwa uloto.
Ugonjwa wa Selimundu ni ugonjwa wa kuzaliwa nao kutokana na kuurithi kutoka kwa wazazi wa mtoto kupitia vinasaba.
Akiongea na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma cha Hospitali, Mama mzazi wa mtoto, Pendo Luteja, amesema alipata taarifa kuwa BMH wanatoa huduma hiyo kupitia chombo Cha habari Cha televisheni (TV).
"Niliona kwenye TV wakati Mhe. Ummy (Waziri wa zamani wa Afya) anamtambulisha mtoto wa kwanza kupona sikoseli Bungeni baada ya kupata matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa," amesema mama mzazi wa Faith, ambaye ni mkazi wa Musoma, mkoani Mara.
Pendo amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, madaktari na wauguzi kwa kuanzisha huduma hiyo, kwani imesaidia kuokoa uhai wa binti yake.
Soma Pia: Rais Dkt. Samia ametoa fedha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kutibu watoto 20 wenye ugonjwa wa Selimundu
"Namshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali kwa kufikiri na hatimaye kuanzisha huduma. Kwa kweli, imesaidia kuok