Mgunda ailalamikia Bodi ya Ligi

Mgunda ailalamikia Bodi ya Ligi

Mbigirikavu

Senior Member
Joined
Aug 19, 2022
Posts
101
Reaction score
118
Mechi ya Simba na Yanga imechezwa tarehe 23-10-2022, Chama na Azizi walifanya makosa yaliyopelekea kufungiwa mechi tatu. Bodi ya Ligi imetoa hukumu jana tarehe 8-11-2022 takribani siku 17 baada ya mechi.

Mgunda anasema uamuzi wa kuwaadhibu wachezaji ulipitishwa tangu tarehe 4-11-2022, bodi ikaweka kabatini uamuzi huo mpaka jana ambapo Simba inakabiliwa na mechi ya ushindani leo tarehe 9-11-2022.

Juma Mgunda kama kocha ameshaandaa kikosi chake akimuhusisha Chama mpaka kufikia jana. Kwa hiyo analazimika kufanya mabadiliko ya dharura ili kuziba pengo la Chama.

Hii imemwathiri yeye kama kocha. Mgunda anakubaliana na adhabu aliyopewa mchezaji wake kuwa ni sahihi kwa mujibu wa kanuni. Lakini analaumu bodi kwa kuchelewesha taarifa ya maamuzi yaliyofanyika tarehe 4 na kuyatoa jana tarehe 8 siku moja kabla ya mechi dhidi ya Singida Big Stars.

Kwa nini wasitoe mapema?
 
Naona mlikuwa mnaicheka Yanga eti "wanalalamika.......",mkazani labda Yanga watakuwa kwenye hali mbaya.

Mgunda lazima alalamike kwanza wamechelewa kumwambia wakati tayari kishaplan,pili adhabu ni ya kipuuzi na kipumbavu sabau kupeana mikono ni fair play sio lazima.
So Mgunda lazima awe mkali sababu ,Chama ndio Key player wa Simba,unapo msimamisha kwa sababu za kipuuzi unaharibu game plan nzima ya kocha.

Kwa Yanga wataumia ila Aziz K kuna replacement yake ila kwa Chama hamna replacement.

Ila tusiwalaumu TFF kwani hizi sheria zimepitishwa na viongozi wa club zetu wasiojua nini maana ya fair play na leo zinawacost kwenye club zao.Mgunda ana haki ya kulalamika, wewe tokea mechi ya Yanga na Simba mpaka leo ni kama wiki tatu,siku zote walikuwa wapi kufanya haya maamuzi.
 
Ndio nafasi ya Muzamiri kuonesha uwezo
 
Michezo ya kibahasha hii
 
Lzm Leo kwa mwigulu akalie live live analiwaa vzr tu

Chondechonde sbs hakikisheni mgunda asichomoke
 
Hebu Okwa nae aanze kulipa bill
 
Mbona hamkuongea kipindi Bm3 alivyo ikosa Kariakoo Derby,hebu kausheni bhana kila kitu si lazima mkiletee uzi humu ilitakiwa mzoee na muone ya kawaida kama YANGA ilivyo watokea.
 
Back
Top Bottom