Mgunda ailalamikia Bodi ya Ligi

Mgunda ailalamikia Bodi ya Ligi

Mbona hamkuongea kipindi Bm3 alivyo ikosa Kariakoo Derby,hebu kausheni bhana kila kitu si lazima mkiletee uzi humu ilitakiwa mzoee na muone ya kawaida kama YANGA ilivyo watokea.
Yanga, (wala mihogo) ni tofauti na Simba sports club. Ukiona simba wanaongea fahamu kuwa lipo la kujifunza. Elewa kwanza kilichosemwa.
Taarifa ya chama imefika jana wakati timu ina game leo.

Vipi hapo linafanana na lile la chokoraa wenu? Taarifa yake ilitoka siku moja kabla ya game?
 
Mechi ya Simba na Yanga imechezwa tarehe 23-10-2022, Chama na Azizi walifanya makosa yaliyopelekea kufungiwa mechi tatu. Bodi ya Ligi imetoa hukumu jana tarehe 8-11-2022 takribani siku 17 baada ya mechi.

Mgunda anasema uamuzi wa kuwaadhibu wachezaji ulipitishwa tangu tarehe 4-11-2022, bodi ikaweka kabatini uamuzi huo mpaka jana ambapo Simba inakabiliwa na mechi ya ushindani leo tarehe 9-11-2022.

Juma Mgunda kama kocha ameshaandaa kikosi chake akimuhusisha Chama mpaka kufikia jana. Kwa hiyo analazimika kufanya mabadiliko ya dharura ili kuziba pengo la Chama.

Hii imemwathiri yeye kama kocha. Mgunda anakubaliana na adhabu aliyopewa mchezaji wake kuwa ni sahihi kwa mujibu wa kanuni. Lakini analaumu bodi kwa kuchelewesha taarifa ya maamuzi yaliyofanyika tarehe 4 na kuyatoa jana tarehe 8 siku moja kabla ya mechi dhidi ya Singida Big Stars.


Kwa nini wasitoe mapema?
Watu wanatoa adhabu Kwa kuviziana. Utadhani Polisi wanakukamata Ijumaa ili ukose dhamana Hadi Jumatatu.
 
Back
Top Bottom