ToniXrated
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 1,134
- 2,993
Nimeiangalia Simba toka Kocha Mgunda anakabidhiwa timu msimu huu nikagundua kuwa ni muhamasishaji mzuri ila sio kocha mzuri. Tuwe wakweli, Simba inabebwa sana na uwezo binafsi wa wachezaji watatu kupata matokeo msimu huu, nao si wengine bali ni Chama, Phiri na Okra.
Mgunda amekuwa akihusika na kupanga kikosi cha timu kishikaji huku akiendekeza kitu kinachoitwa "Uzawa". Kwamba lazima wachezaji wazawa wacheze huku wale wenye viwango vya kimataifa tena waliosajiliwa kwa pesa nyingi kama kina Sakho, Banda, Okwa, Ouatara wakiendelea kulitumikia benchi wakati huo huo wachezaji ma-flopp kama kina Mkude, Nyoni na Bocco wakiendelea kupata namba.
Amekuwa akichezesha wachezaji nje ya position zao halisi. Hivi Phiri ni wa kumchezesha kama winga? Mgunda anahusika katika kufanya subs za ovyo kabisa. Anaona timu imezidiwa kati anamuingiza Bocco, anamuacha Mkude amalize dakika 90, ili hali hata kukimbia hawezi. anamuanzisha Nyoni mchezaji ambae hastahili kabisa kuvaa uzi wa Simba.
Wito wangu kwa uongozi wa Simba ni kuwa tutafute kocha wa maana, mwenye ujuzi na uzoefu wa kutosha tena atoke nje ya Tanzania, pia aje na benchi lake zima la ufundi ili kuja kuepusha upendeleo na yoendelea kwa jina la "Uzawa".