Mguu wangu masikini!

Mguu wangu masikini!

yaelekea ni nzuri ila ndefu sana..nimeshindwa kuimaliza..hebu mtu anisummarizie fasta fasta! nina hamu ya kujua contents

okay....
Mtambuzi (sio yeye) na Waridi.....Mtambuzi akawa anamkula Waridi....mke wa Mtambuzi akajua, Mtambuzi akakataa......Waridi na Mtambuzi wakasafiri....ajali ilipotokea Waridi akafa......Mtambuzi akakatika mguu (hapa ukumbuke sio yeye)...mke wa Mtambuzi akaolewa na mume wa Waridi.......
umeelewa sasa........

 
Asante Mkuu Mtambuzi kwa maandishi yako ambayo hayaishi utamu.
 
Duh! Kweli mshahara wa dhambi ni kufa!
Tunajifunza kutoka kwa wengine, kama tumeamua kujifunza. Kwa wale ambao wameamua kujifunza kupitia habari hii, ni wazi watakuwa wamejifunza kitu kikubwa na cha maana sana. Wataalamu wa uhusiano wanadai kwamba, mtu anapotoka nje ni lazima atafumaniwa. Kama hatafumaniwa mwaka wa tatu tangu uhusiano wake na huyo mpenzi wake kuanza, basi ni lazima atafumaniwa kabla ya mwaka wa sita wa uhusiano huo haramu.

Kinachofanya mtu afumaniwe ni ule ukweli kwamba, baada ya kuzoea, mtu hujisahau na kuweka ngao yake ya kujikingia chini. Badala ya kwenda mbali kufanya mapenzi, watu watafanyia karibu, badala ya kuwaficha watu, ataambiwa mmoja ambaye anaitwa rafiki yangu wa kufa na kuzikana na hisia za umiliki badala ya wizi hujijenga. Kufumwa kunaweza kusababishwa na chochote kati ya hayo au mangine. Kwa mfano, ajali ambayo imewatoa hadharani marehemu Waridi na msimulizi wa stori hii, inatokana na kuzoeana ambako kumeondoa hofu ya wizi wa mali ya mtu na kuwafanya wote, kila mmoja kuamini kwamba, huyo mwenzake ni mali yake.

Unaweza ukaamini kwamba , wewe ni mjanja na una maarifa mengi sana katika kukanusha, katika kuteleza, usifumaniwe. Lakini kwa sababu ni nguvu mbovu unazozipanda ni lazima utazilipia, kwani zitakurudia tu, utake usitake. Unapotoka nje, jiandae kunaswa siku isiyo na jina. Kama utaacha kabla hujanaswa, siyo kwa sababu ni mjanja, bali ni kwa sababu, hiyo nguvu uliyopanda ilikuwa haijakamilishwa mzunguko wake.

Unapoonywa na mpenzi wako, unapooneshwa wasiwasi kwamba, unatoka nje, kama ni kweli, inabidi uache. Kama utaendelea, jua tu kwamba, utapata shida utaumia baadaye.
 
Mzee mwenzangu Rejao, unajua hii stori ilikuwa na kurasa nane! hapo nime-summarize sana
Hapa ngoja niendelee tu kusoma comments za watu...kupitia hizo nitapata picha nzima!
najiuliza ,mkono wako umeweza kuchapa vipi story yote hii, au tayari umeshapona kabisa?
 
Imetulia ila sina uhakikia mtu aliyekwishaanza kazi mwaka 1977 kama ana uwezo wa kutumia computer
 
Daaa pole yake huyo kaka, ila kila siku huwa nahubiri humu; Jamani Ma-infed ... wa humu, mke wa mtu sumu, acheni kabla hamjakamatwa wala habari kuvuja!
 
Hapa ngoja niendelee tu kusoma comments za watu...kupitia hizo nitapata picha nzima!
najiuliza ,mkono wako umeweza kuchapa vipi story yote hii, au tayari umeshapona kabisa?

Kazi hiyo kaifanya shemejio Mama Ngina, mie bado naumwa mkuu................
 
hii story iko juu! kwa movie inafaa sana, tena itauzika. tatizo movie za kibongo wanalipua mno, hasa hapo kwenye kutengeneza tukio la ajali.
 
Back
Top Bottom