Mh, dhambi ya Uroda.....

There is no god, and Kiranga is his prophet. --Hii inamanisha nini kwa kiswahili Ndg Kiranga?.

Hii inamaanisha Kiranga ni kuhani asiyeamini mungu, anaeneza ukweli kwamba mungu hayupo.Na siyo kwamba amenda likizo au kalala uingizi au kafa, hajawahi kuwepo, hayupo na hatakuja kuwepo.
 
Ukishaongea imani unaweza kuongea chochote kile, mi nataka facts, testable tangible observable facts.

Imani uanweza kuamini mungu anakaa misitu ya Kongo, poa tu kivyako.Ukitaka kuleta kama fact that is another matter.

Umekuja nilipopataka, na nilijua utakuja hapo ndo maana nikaanza kusema I can prove to you through facts, and the following are among the facts regarding your questions( tangible, observable, n.k.)
First of all be informed that not all non tangible, testless, and un-observable things do not exist. I am sure every one is aware about force, and if ask one will tell you there is a force thus why a flight take off, but if ask him can you observe, touch the force no one will tell you that he see/saw it by his/her eyes , no one had touch it or test it through five organs, but it is a force, which implies that, there are other organ that can prove existance of the force!!!!!!!! Like wise other organs are week to prove existance of the force. Similarly, the existence of god can be proved by organs other than what you forementioned as facts to prove his existence.

This is just one example to demostrate you that God do exist mzeeeee.
 
Hii inamaanisha Kiranga ni kuhani asiyeamini mungu, anaeneza ukweli kwamba mungu hayupo.Na siyo kwamba amenda likizo au kalala uingizi au kafa, hajawahi kuwepo, hayupo na hatakuja kuwepo.


UNA MAANISHA Kiranga ni "kuhani" au ...." KIRANGA Ni Kuhani wake......(..)???" kwa maana ya kwamba "his prophet? kama ulivyoandika mwenyewe kwenye signature yako?

"...Wan'changanya tena hapa!

WHICHEVER THE CASE, kama wewe ni "Prophet", tafadhali soma hapa chini tafsiri yake na utaona unavyopotoka kutumia neno hilo kwa kuwa "prophet" au "Kuhani "/Nabii" siku zote huwa ametumwa kufundusha yale anayoongozwa na mtu fulani aliyemtuma.

Na hapa unaonekana kuwa wewe una kana uwepo wa Mungu kwa upande mmoja lakini unakiri uwepo wa huyo Mungu kwake kwa upande mwingine !. How these two different facts apply simultaneously?. Unless otherwise utuambie sie huyo Mungu tunayemfikirai sie wengine ni wako!.

 

Huwezi kunielewa kwa sababu pembetatu yako ina nyuzi 180, mimi naingia kwenye pembetatu yenye nyuzi zaidi ya au chini ya 180 lakini kamwe si 180. Wewe unatumia Euclidean geometry wakati mimi nipo kwenye non euclidean geometry, why, you even quote the old testament or some antiquated ancient jewish books, how laughable..

Unatumia common sense wakati mimi naingia kwenye counter-intuitive uncommon common sense ya quantum physics za kina Wolfgang Pauli huko.

Ninaposema thre is no god, nafanya "no god" kuwa ndiyo godhead entity yangu.

Ninaposema and Kiranga is his prophet, namanisha Kiranga is the prophet of godlessness.Ndiyo maana nipo hapa naongea kwamba hakuna mungu, natumia sayansi kueleza phenomena as best as possible na pale sayansi isipoweza kutoa jibu sioni haya kusema hapa hatujajua bado, unlike theistambao kila kitu wasichojua wanamlundikia mungu.

Sijui kama utaelewa hili.Halafu mambo mengine ni dramatic effect, obviously nikikwambia there is no god halafu nikakwambia and Kiranga is his prophet hutakiwi kushangaa kwa nini nimetumia his, it is a quantum physics weirdness thing, counterintuitive picturization that does not to necessarily make sense in the large scale universe, ni kama Einstein alivyo coin phrase ya "in my mind's eye" hutakiwi kushangaa sana kwamba huyu bwana ana jicho katika mawazo yake.

Otherwise watu watakuona slow tu, huelewi artistic language.
 
...sasa nimekubali kwamba..there is no god,..but there is God and Kiranga can not be his prophet unless he admit His existance.
 
...sasa nimekubali kwamba..there is no god,..but there is God and Kiranga can not be his prophet unless he admit His existance.

Like I said, we can't see eye to eye and therefore we can't relate.

Katika ulimwengu wako parallel lines kamwe hazigusani, katika ulimwengu wangu parallel lines zinagusana, tutaelewanaje?
 
Kiranga, you appear to be almost acrobatic guy, acha sarakasi za maneno ambayo huwezi kuyajengea hoja!.

Usijaribu kucheza na maneno ya lugha ya kigeni, kumbuka hata hizo "uncommon sense ya quantum physics za kina Wolfgang Pauli" na akina Einstein unao warejea kama msingi wa mawzao na imani yako kuwa mungu hayupo, zina chimbuko lake na wewe yawezakuwa hao sasa ndo "miungu wako" kwani waonyeshwa wazi unavyo waamini kwenye nadharia zao. Kama ndo unaanza kuingia kwenye hiyo fani ya kupingana na ukweli, jaribu usichanganye sanyansi, lugha na dini.

"Science" is all about "theories" and "proofs" therefore, it has never worked "on common sense". "common sense is always men perceptions of what is applied in the realy world and can not be simply ignored (note: common sense is what people in common would agree on, : that which they "sense" as their common natural understanding!., without reliance on esoteric knowledge or study or research, but based upon what they see as knowledge held by people "in common". .) while "Uncommon sense" is the opposite of "common sense" and always based on the individual's perceptions, counterintuitive views which are undistiguishable to theories of the "common sense".

Kumbuka kuwa kwenye sayansi "common sense" is always applicable when there is a "point of return and failure of man's mind/brain to reach to the truth" kwa maana nyingine ni kuwa unapaswa kuanza na uhalisia na ili kuthibitisha "uwepo au kutokuwepo kwa uhalisi" na pale unaposhindwa kuthibitisha yale uliyotaka watu wayaamini kuwepo au kutokuwepo, usitumie vigezo vya wengine kuthibitisha ambavyo wao wamenshindwa pia kuyathibitisha vinginevyo utakuwa unakubaliana nami kuwa unachokifikiria unatumia "common sense" na sio "uncommon sense"!.
 
Probably,this is my last comment tonight,..Kama utapata muda ukasome Zaburi 53:1..mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu,wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza,hakuna atendaye mema........ninaamini kuanzia utaamini kwamba Mungu yupo maana siamini kwamba unataka kuwa mmoja wa wapumbavu watendao uovu,ufisadi na machukiza eti kwa kufikiri tu kwamba mungu hayupo.
 

Nnai kakwambia namuamini mtu? Umelitoa wapi hilo? Unaweza kunionyesha hapa? Au unajisemea tu?
 

That is where you arewrong, hujaonyesha kama mungu ana exist, umeonyesha unavyoshindwa kuonyesha mungu ana exist.

Force is a measurable entity,

Force = Mass X Acceleration

Kitu kingine ukikiita force, sijui roho mtakatifu na makorokoro mengine mizimu siju ambayo hayapimiki kisayansi hizo si forces za kisayansi, labda kwenye voodoo kuna force nyingine lakini haitambuliki kiayansi

Hii ni elementary physics

Ona hii website ya Chuo Kikuu cha Illinois inaweza kukusaidia kuhusu force ni nini.

Ndiyo maana nasema mnaoamini mungu mnajitungia vitu visivyoonekana wala kupimika na kuharibu haya majina kama force, kuchanganya watu

http://van.physics.illinois.edu/qa/listing.php?id=268

Measuring forces and speeds

Q: How can you measure the force on an object? Is there any way to measure the speed of an object without using a radar gun?

-Anonymous

A: There are lots of ways to measure the force on an object and the speed of an object. Which way you might use depends on the details of what you're doing. I'll give some examples of how to measure force and speed -- perhaps you can think of some more!

Measuring force:

1) A scale will directly read the force applied to it. A bathroom scale usually has a spring inside attached to a dial which reads how much the spring has either compressed or stretched, depending on how the scale is constructed. Scales read forces in units of pounds in the United States.

2) You can hook up a spring directly to the object you would like to measure the force on, and pull on the other end of the spring. The amount by which the spring stretches is directly proportional to the force applied. The constant of proportionality depends on the spring and should be calibrated with a known force, like a known weight.

3) You can use Newton's law F=mA. If you know the mass of an object and can measure its acceleration, the force is the product of these two. But be careful -- this force is the sum of all forces on the object. Be careful with friction! Measuring the acceleration just means measuring the speed at different times and seeing how it changes. Acceleration is the change in speed divided by the change in time.
 

Don,

sijui kama atakuelewa hapa yeye yupo kwenye kundi la "uncommon sense thinkers". Lakini uzuri wa hawa watu ni kuwa nadharia zao zikifeli huwa wanatabia ya kuamini MUNGU yupo kwa kuwa huwa wanatehgemeana kwenye hilo hilo kundi la "uncommon sense thinkers" badae wanakuja kulingana kimawazo na hapo ndipo tunaposema wote ni "common sense" ambayo Kiarnga anajaribu pasipo utafiti wa kina kuikwepa hapa.

Kwa kuwa dini ni nyingi, imani tofauti, kwa miungu tofauti, yawezekana kabisa huyu ndugu yetu Kiranga ana waamini wana sayansi wenzie kuliko mtu mwingine yeyote. Anaweza kukuambia pengine hata yeye hakuzaliwa na yupo kwa sababu yupo tu. Sikujui ana kanushaje, kwa nini anapumua,amelala sasa, anasikia njaa, anakwenda haja, ana simama, ana kaa, analia, ana chukia, ana cheka, ana waza nk.

Anajua kuwa yaliyomo ndani yake sio sayansi imeyaweka na sayansi haiwezi kuyafanya yaendelee kuwepo ndani yake milele (ndo maana hata mashine za hewa ya oksijeni zilizotengenezwa na mwana damu uwekwe mtu pale ambapo anakuwa kwenye hali ya ambayo hawezi kuishi na hewa hiyo ikishindwa, sayansi haiwezi kumrudishia uhai). Hawezi pia kutuambia hapa ni nani aliyemfanya awe hivi allivyo leo.....na ametokea wapi kabla ya kuwepo hapo, na kwa nini yupo hivyo halivyo na asiwe vile anavyotaka!.

Sayansi pia bado haijathibitisha kwa uhalisi asili ya binadamu wala hatima yake baada ya hapa mbali na nadharia tu zinazotolewa ambazo zinapingania. Hata hao wanasayansi maarufu waliokufa hawajaelezewa na wenzao walipo mpaka sasa!.

Lakini napata faraja kuwa kama sayansi na dini vingekuwa na mustakabali sawa, pasingekuwa na ugunduzi wowote duniani,

Watu kama hawa wawepo duniani kwa ajili ya mafanikio katika maisha ya binadamu.

Alaamsiki sasa!
 

Na mimi nitakwambia, mjanja kwa kutumia saikolojia amemfunga mpumbavu wa kweli kwa kumuogopesha kuitwa mpumbavu kwa kumwambia "mpumbavu amesema moyoni hakuna mungu"

Biblia hiyo hiyo unayo i quote imejaa contradictions, sehemu nyingine inakwmbia kila kitu ubatili mtupu.Contrdiction lukuki, ukiangalia unaona biblia imeandikwa na kuwa compiled na watu tu, wame i edit mara kibao, wameitumia kisiasa tangu enzi za kina Constantine na council of Nicea mpaka George W Bush, wengine wameitumia ku justify kuwafanya watu weusi watumwa na uchafu kibao, then unataka niiamini kichwa kichwa tu?
 

Huyu anonymous ni nani? na kwa nini unadhani rejea imefanyika kwa "Newton Law" kama sio hiyo "Common sense" unayojaribu kupingana nayo hapa??. Kumbe huna msimamo wako binafsi, hao akina Newton ndo Miungu wako tunaosema vinginevyo huwezi kuja na hoja binafsi ya kuthibitisha kutokuwepo kwa Mungu pasipo kuwarejea marehemu kama akina Newton?..
 
Nnai kakwambia namuamini mtu? Umelitoa wapi hilo? Unaweza kunionyesha hapa? Au unajisemea tu?




Haya sio maandiko yako unayojaribu kuyakwepa?...ua ulimaanisha nini, unakuwa na "uncommon sense" hata penye "Common sense"??
 

Are you anti science? unapinga ukweli wa Newtons Law?

Wewe una msimamo wako binafsi? Kati ya mimi ninayequestion vitu katika sayansi (sayansi msingi wake ni ku question) na wewe unayeamini dini (dini msingi wake ni imani bila kuuliza, Augustine alipoulizwa mungu alikuwa anafanya nini kabla ya kutengeneza dunia alijibu kwamba alikuwa anatengeneza moto kuwaweka watu wanaouliza maswali kama hayo, go figure) nani ana independence zaidi? Hivi dini na sayansi kipi kinaruhusu independent thinking zaidi? Unaweza kusema kitu kuhusu "msimamo wako?" naona unanifanya nisitafute weakness zako, maana unazisema mwenyewe kwa niaba yangu.

Halafu tofautisha msimamo wa mtu na established fact.Huwezi kukataa kutumia a wheel kwa sababu eti si wewe uliyeligundua na kwa hiyo si lako, si msimamo wako, inakubidi uvumbue kitu kingine sawa na wheel.Utakuwa babu jinga.

Hizi established scientific facts and formulas ni kama the already invented wheel, siwezi ku shy away from using these tools eti kwa sababu si "msimamo wangu" ninachoweza kufanya ni ku verify kama vinaweza ku stand logical scientific tests.

Unavyozidi kuandika ndvyo unazidi kuanika ignorance yako.
 

Jifunze netiquette kwanza, una bold post nzima.Kama unaandika barua ya kuomba kazi inaenda straight kapuni.
 

Kur'an

17. SURA AL ISRAAI (BANI ISRAIL) 32. Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.

24. SURATUN NUR
(Imeteremka Madina)

Sura hii ni ya Madina, na Aya zake ni 64. Mwenyezi Mungu amebainisha ndani yake waajibu wa kusafisha umma na uchafu wa zina na kutangaza fedheha kwa vitendo na maneno kati ya Waumini. Na akaleta sharia ya adhabu kuzuia hayo, kama alivyo leta sharia makhsusi katika uzinzi wa mume au mke ili kujenga imani baina ya mtu na mkewe. Kutoka uzinzi masimulizi yakaingilia kutaja hukumu ya uwongo katika hali hizi, na yawapasayo Waumini kwa min tarafu ya neno ovu lisio kuwa na dalili. Tena yakafuatia masimulizi ya adabu za kuingia majumbani. Na nani mwenye haki ya kuona pambo la mwanamke. Na baada ya wito wa jumla ikafuatiliza kutakiwa mwendo safi usio na towa. Kisha imekuja Nuru ya Mwenyezi Mungu, na inatajwa misikiti, na vinatangazwa vitendo vya makafiri na hali za wenye inadi. Na upande mwengine zinaelezwa hali za Waumini. Baada ya hayo Sura inaeleza adabu za watu wa nyumbani, watu walio khusiana, watoto na wakubwa, katika hali ya kuingiliana na kuchanganyika. Na nani mwenye haki ya kula naye mtu. Na khatimaye zimetajwa sifa za Waumini wanapo itwa na Mtume kwa jambo lilio wakhusu wote, na Sura ikambainisha Mwenye Ukuu wa Ufalme wake ulio tukuka, na Mwenye kuenea ujuzi wake.

2. Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini

3. Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo yameharimishwa kwa Waumini.

Na wanao wasingizia wanawake mahashumu, kisha wasilete mashahidi wane, basi watandikeni bakora thamanini, na msiwakubalie ushahidi wao tena. Na hao ndio wapotovu.

5. Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu.

6. Na wale wanao wasingizia wake zao na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika yeye ni katika wasema kweli.

7. Na mara ya tano kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo

8. Na mke itamwondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba huyu mume ni miongoni mwa waongo.

9. Na mara ya tano ya kwamba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake kama mumewe yu miongoni mwa wanao sema kweli

10. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na ya kuwa Mwenyezi Mungu ni Mpokeaji toba..



Biblia Kumbukumbu la Torati/ Chapter 5 18. Wala usizini.

Mathayo/ Chapter 5 27. Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28. lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
30. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…