Jamii01, fuatilia thread za Lowassa humu utaziona mpaka mali zake zimeorodheshwa!. Lowassa ni tajiri wa ukweli aliyepata mali zake zote kihalali na ndio maana amezisajili zote kwa jina lake na la mkewe Rejina!.
Ila hakuna ubishi CCM imegubikwa na ufisadi hali inayopelekea kila yeyete mwenye chochote kitu kuonekana fisadi.
Lowassa ni miongoni mwa wanaitwa mafisadi wakuu kufuatia kukubali kulibeba lile zigo kubwa la Richmond ili kumnusuru best wake na chama chake na aibu ya mwaka, hivyo yeye kuchafuka kwa kukubali kujitwisha msalaba wa ukombozi na salama ya CCM!.
Anachokifanya huko makanisani na kwenye michango mbalimbali ni kuonyesha uwezo wake kwenye kitu kinachoitwa mass mobilization kwa ajili ya kujiletea maendeleo, kitu ambacho JK ameshindwa kabisa!.
Hilo la kuandikwa magazetini, na kwenye vyombo vya habari, ni kufuatia EL kuwa na mvuto wa ajabu uliotoka kwa Mungu. Kila asemalo linamantik kwa hali ilivyo sasa!. Lowassa ni photo genic!, akipigwa picha anapendezea!, akiongea anavutia kumsikiliza!, na kikubwa zaidi yeye sio mtu wa maneno maneno na vitendo sifuri kama JK, yeye ni mtu wa maneno mafupi na vitendo virefu.
Wakuu wengi waliopo wakisikia JK atatembelea mahali, huandaa taarifa safi, mkuu akifika, akishasomewa taarifa, hupiga makofi na kuendelea na ziara!. Enzi za Lowassa akishasomewa taarifa huipokea na kuelekea physically kuyaangalia hayo yaliyozungumziwa!. Hivyo watu wakisikia JK anakuja, hukaa miguu juu, ila wakisikia ni Lowassa!, kijasho huwa kinawatoka maana jamaa hakubali kabisa longo longo yoyote!.
Ni kufuatia utendaji huu ndio maana mimi na wenzangu wachache humu jukwaani, tumeamua kujitolea kumsafisha Lowassa na ule uchafu wa Richmond, tunamtaka alitue hilo zigo amkabidhi mwenyewe, na yeye ndie ateuliwe kuwa mgombea wa CCM tumpigie debe, aingie Ikulu!.