Published on 14 Aug 2017
Mh. James Mbatia asifu uchaguzi wa Kenya
Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi James Mbatia (Mbunge) link-for-bio: Parliament of Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa UKAWA (Umoja wa Katiba wa Watanzania), ameusifu uchaguzi wa Kenya uliofanyika Agosti 8, 2017, wakati alipoalikwa kwenye kipindi cha Mizani ya wiki kilichorushwa na kituo cha Azam TV ya Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Katika kipindi hicho maalum pia Mh. Balozi Boniface Muhia wa Kenya anayewakiliwa nchi yake Tanzania pia aligusia katiba mpya ya mwaka 2010 ya Kenya na zoezi zima la kusajili wapiga kura na wakati wa kupiga bila kusahau Idara ya Mahakama Kenya kufanya kazi nzuri ya kutafsiri sheria za uchaguzi na vipengele vya katiba vinavyolenga uchaguzi kuwa huru.
Mh. James Mbatia kwa kina achambua makuzi ya demokrasia nchini Kenya toka mwaka 1992, 2007, 2012 kutokana na uzoefu wake kama mwenyekiti wa TCD (Link: Tanzania Centre for Democracy ), midahalo, vyombo vya habari kuwa na uhuru. Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC Link: Independent Electoral and Boundaries Commission ) katika kutumia teknolojia na kujaribu kutoa ufafanuzi wa maswali magumu n.k
Mh. James Mbatia pia anaangalia hotuba za viongozi wa JUBILEE na Umoja wa NASA baada ya matangazo ya matokeo ya ushindi wa uchaguzi wa Rais. Na mahusiano kati ya chama tawala Tanzania cha CCM(Chama Cha Mapinduzi) na umoja wa NASA chini ya Raila Odinga kwa upande moja. Na upande wa Upinzani Tanzania kuwa karibu na JUBILEE iliyomsimamisha Uhuru Kenyatta katika kampeni zilizofanyika kuelekea uchaguzi wa Kenya uliohitimishwa tarehe 08/08/ 2017.
Source: Azam TV