Mh. James Mbatia asifu uchaguzi wa Kenya

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Published on 14 Aug 2017

Mh. James Mbatia asifu uchaguzi wa Kenya
Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi James Mbatia (Mbunge) link-for-bio: Parliament of Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa UKAWA (Umoja wa Katiba wa Watanzania), ameusifu uchaguzi wa Kenya uliofanyika Agosti 8, 2017, wakati alipoalikwa kwenye kipindi cha Mizani ya wiki kilichorushwa na kituo cha Azam TV ya Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Katika kipindi hicho maalum pia Mh. Balozi Boniface Muhia wa Kenya anayewakiliwa nchi yake Tanzania pia aligusia katiba mpya ya mwaka 2010 ya Kenya na zoezi zima la kusajili wapiga kura na wakati wa kupiga bila kusahau Idara ya Mahakama Kenya kufanya kazi nzuri ya kutafsiri sheria za uchaguzi na vipengele vya katiba vinavyolenga uchaguzi kuwa huru.

Mh. James Mbatia kwa kina achambua makuzi ya demokrasia nchini Kenya toka mwaka 1992, 2007, 2012 kutokana na uzoefu wake kama mwenyekiti wa TCD (Link: Tanzania Centre for Democracy ), midahalo, vyombo vya habari kuwa na uhuru. Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC Link: Independent Electoral and Boundaries Commission ) katika kutumia teknolojia na kujaribu kutoa ufafanuzi wa maswali magumu n.k

Mh. James Mbatia pia anaangalia hotuba za viongozi wa JUBILEE na Umoja wa NASA baada ya matangazo ya matokeo ya ushindi wa uchaguzi wa Rais. Na mahusiano kati ya chama tawala Tanzania cha CCM(Chama Cha Mapinduzi) na umoja wa NASA chini ya Raila Odinga kwa upande moja. Na upande wa Upinzani Tanzania kuwa karibu na JUBILEE iliyomsimamisha Uhuru Kenyatta katika kampeni zilizofanyika kuelekea uchaguzi wa Kenya uliohitimishwa tarehe 08/08/ 2017.

Source: Azam TV
 
Halafu hilo jina 'Mbatia' mbona kama tumemuazima maana la Kikenya hilo.
Anyway uchaguzi wetu ulikua wa haki, tulidhihirisha demokrasia isiyo ya kawaida Afrika. Hata kama angeshinda Raila, mwisho wa siku ukweli ungekua huo kwamba uchaguzi ulikua wa kipekee, tume yetu ya IEBC walijiandaa ipasavyo.

Kuna tuhuma za kila aina lakini hazina mantiki, eti kwamba password ya bwana Msando ilitumika kudukua mfumo, watu wanachukulia mifumo kuwa jambo la kawaida sana. Kama angeuawa usiku wa kuamkia uchaguzi, labda hapo ningekubali, lakini sio pale mtu anauawa siku kadhaa kabla halafu eti password yake bado inakua hewani tayari kwa matumizi. Ikumbukwe huo mfumo hakuutengeneza yeye, ulitegenezwa na kampuni ya Ulaya ambayo ilikua na dhamana ya kuulinda hadi mwisho.

Vongozi wa NASA walionyesha logs za MS server 2008, mfumo uliopitwa na wakati sana, IEBC wanatumia Oracle solutions. Hapa wakubali walishindwa kabisa yaani herufi kwa herufi, namba kwa namba, leo hii viongozi wao mikoani na kwenye gatuzi zote wanapokea vyeti vya ushindi huku wakilalamika kwamba uchaguzi haukua wa haki, huo ni unafiki. Ikumbukwe pia Jubilee wamezoa idadi kubwa ya magavana, maseneta, wabunge yaani huu ulikua ushindi wa kichapo.

Uhuru aliuza sera zake kweli kweli, sikutegemea ataungwa mkono kiasi hiki hadi hata maeneo ambayo ni ngome kabisa ya NASA. Ana dhamana kubwa hatamu hii, ajaribu kila jinsi ya kutuunganisha Wakenya.

Kenya tukirekebisha ukabila, tutakua kwenye ligi ya nje ya Afrika, japo pia ndio demokrasia yenyewe hiyo, pamoja na kwamba nachukia vigezo vya ukabila, lakini ikumbukwe demokrasia inampa kila Mkenya wa kutumia kutumia kigezo akipendacho kwenye uchaguzi, akiamua kutumia ukabila, huo ni uhuru wake kidemokrasia.
 
Hivi huu ukabila mnafundishwa shuleni au? Huwa sielewi inakuwaje? Mimi binafsi nimezaliwa mkoa ambao sio wa asili ya wazazi wangu kabisa nimesoma huko na kukua huko Sikuwahi sikia watu wale wakiniuliza kabila langu hata Mimi mwenyewe Sikujua kabila langu, Neno kabila nimekuja kulifahamu nikiwa University nilipolazimishwa kwenda kumsalimia Babu yangu mzaa Baba, Babu Yeye alijaribu kunisalimia kwa hiyo lugha nikashindwa kujibu tukaishia kucheka, Sasa Kenya watu wenyewe mna sura mgumu na Dada zenu bado mnabaguana, Hivi kuna wakenya weupe Kweli wengi naona shapeless
 
Kutokujua kabila lako na asili yako na lugha yako ya asili ina maana umekua ukiishi kama mtumwa asiyekua na asili.
Ukabila ni tabia ya mtu binafsi lakini kuwa na asili ni maumbile.
 
Kama na wewe una mawazo basi nyie ni suala la muda tu kuna siku mtachinjana tu, mnaweka vizazi vyenu rehani, Sisi lugha yetu ni moja tu kiswahili nchi nzima, lugha ya kikabila ongelea chumbani na mke wako, Hivi unawezaje kuanza kuongea kikabila mbele ya jamii
 
Kumbe alisha pona...[emoji45] [emoji45]
 
Kwani huyu mbunge James Mbatia wa Tz ana la ukoo wa waKikuyu ? Amezaliwa wapi na anatoka jamii gani sababu waKikuyu wako na watu wanaitwa Mbatia wengi sana.
Kama na wewe una mawazo basi nyie ni suala la muda tu kuna siku mtachinjana tu, mnaweka vizazi vyenu rehani, Sisi lugha yetu ni moja tu kiswahili nchi nzima, lugha ya kikabila ongelea chumbani na mke wako, Hivi unawezaje kuanza kuongea kikabila mbele ya jamii
Kabila sio lugha pekee yake .Kunayo vyakula ,mila na tamaduni na vinginevyo ikiwemo utamaduni na mavazi wa waMaasai ambayo umenufaisha nyinyi wote kwa utalii.Sasa tuache ukabila wa manufaa pia?
 
Halafu hilo jina 'Mbatia' mbona kama tumemuazima maana la Kikenya hilo.
Anyway uchaguzi wetu ulikua wa haki, tulidhihirisha demokrasia isiyo ya kawaida Afrika. Hata kama angeshinda Raila, mwisho wa siku ukweli ungekua huo kwamba uchaguzi ulikua wa kipekee, tume yetu ya IEBC walijiandaa ipasavyo.

Kuna tuhuma za kila aina lakini hazina mantiki, eti kwamba password ya bwana Msando ilitumika kudukua mfumo, watu wanachukulia mifumo kuwa jambo la kawaida sana. Kama angeuawa usiku wa kuamkia uchaguzi, labda hapo ningekubali, lakini sio pale mtu anauawa siku kadhaa kabla halafu eti password yake bado inakua hewani tayari kwa matumizi. Ikumbukwe huo mfumo hakuutengeneza yeye, ulitegenezwa na kampuni ya Ulaya ambayo ilikua na dhamana ya kuulinda hadi mwisho.

Vongozi wa NASA walionyesha logs za MS server 2008, mfumo uliopitwa na wakati sana, IEBC wanatumia Oracle solutions. Hapa wakubali walishindwa kabisa yaani herufi kwa herufi, namba kwa namba, leo hii viongozi wao mikoani na kwenye gatuzi zote wanapokea vyeti vya ushindi huku wakilalamika kwamba uchaguzi haukua wa haki, huo ni unafiki. Ikumbukwe pia Jubilee wamezoa idadi kubwa ya magavana, maseneta, wabunge yaani huu ulikua ushindi wa kichapo.

Uhuru aliuza sera zake kweli kweli, sikutegemea ataungwa mkono kiasi hiki hadi hata maeneo ambayo ni ngome kabisa ya NASA. Ana dhamana kubwa hatamu hii, ajaribu kila jinsi ya kutuunganisha Wakenya.

Kenya tukirekebisha ukabila, tutakua kwenye ligi ya nje ya Afrika, japo pia ndio demokrasia yenyewe hiyo, pamoja na kwamba nachukia vigezo vya ukabila, lakini ikumbukwe demokrasia inampa kila Mkenya wa kutumia kutumia kigezo akipendacho kwenye uchaguzi, akiamua kutumia ukabila, huo ni uhuru wake kidemokrasia.
Raila asingeshinda 101% baada ya Msando kuuwawa. Kuuliwa kwa Msando kunahusishwa moja kwa moja na uchaguzi wenu, rejea his past statements concerning riggings in 2013 and how he was going to solve the problem this year's election. I know utatetea hadi mwisho wa dunia ila kuna wa Kenya wengi wanaamini hivyo na hutowa convince vinginevyo.
 
Sipo katika biashara ya ku-convince yeyote, humu tunajadili na kila mtu yupo radhi kutoa maoni au kuamini anachokitaka.
Cha msingi facts ndio muhimu, Msando kusema kwenye runinga kwamba yeye ndiye mwenye password pekee yake nchi nzima hilo sikuliamini maana si yeye aliyetengeneza huo mfumo. Am a software engineer by profession, hamna jinsi user mmoja ambaye sio developer atakua na password ya mfumo wa kihivyo ambao upo sensitive nchi nzima. Huo mfumo umetengenezwa na Wafaransa (kama sijakosea), wao mwisho wa siku ndio walikua na dhamana ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa mfumo.

Haiwezekani mtu mmoja aseme yeye ndiye mwenye password halafu achinjwe na siku kadhaa baadaye watu wawe wanasubiri hawajabadilisha hiyo password au access level, kwamba ipo tu hapo hewani ili itumike. Halafu mifumo haidukuliwi kwa kutumia passwords, the moment umetumia password kuingia basi huo sio udukuzi, ni kama mtu amekupa ufunguo uingie, udukuzi ni pale mtu ametumia mbinu na jinsi za kuingia kwenye mfumo wako bila access au password rasmi.

Ninashuku aliyemchinja Msando (may he RIP) alikusudia kutibua mjadala fulani ili kila mmoja aone kwamba mfumo umedukuliwa, siasa na wanasiasa wana undugu na shetwan, pande zote mbili wana uwezo wa kufanya chochote hata kutoa kafara wanao waliowazaa.

Wanaosema mfumo ulidukuliwa wameonyesha kile waliita ushahidi na wataalam tukiangalia hizo logs ni za server za zamani jameni 2008, halafu teknolojia tofauti kabisa ya Microsoft ilhali IEBC wanatumia teknolojia za Oracle.

Ninashangaa sana kila mtu amejitoa ufahamu na kusema sema eti password ya Msando ilitumika, hata wataalam ambao wanafaa kutoa taarifa za kueleweka kwa jamii.
 
Halafu hilo jina 'Mbatia' mbona kama tumemuazima maana la Kikenya hilo.
Anyway uchaguzi wetu ulikua wa haki, tulidhihirisha demokrasia isiyo ya kawaida Afrika. Hata kama angeshinda Raila, mwisho wa siku ukweli ungekua huo kwamba uchaguzi ulikua wa kipekee, tume yetu ya IEBC walijiandaa ipasavyo.

Kuna tuhuma za kila aina lakini hazina mantiki, eti kwamba password ya bwana Msando ilitumika kudukua mfumo, watu wanachukulia mifumo kuwa jambo la kawaida sana. Kama angeuawa usiku wa kuamkia uchaguzi, labda hapo ningekubali, lakini sio pale mtu anauawa siku kadhaa kabla halafu eti password yake bado inakua hewani tayari kwa matumizi. Ikumbukwe huo mfumo hakuutengeneza yeye, ulitegenezwa na kampuni ya Ulaya ambayo ilikua na dhamana ya kuulinda hadi mwisho.

Vongozi wa NASA walionyesha logs za MS server 2008, mfumo uliopitwa na wakati sana, IEBC wanatumia Oracle solutions. Hapa wakubali walishindwa kabisa yaani herufi kwa herufi, namba kwa namba, leo hii viongozi wao mikoani na kwenye gatuzi zote wanapokea vyeti vya ushindi huku wakilalamika kwamba uchaguzi haukua wa haki, huo ni unafiki. Ikumbukwe pia Jubilee wamezoa idadi kubwa ya magavana, maseneta, wabunge yaani huu ulikua ushindi wa kichapo.

Uhuru aliuza sera zake kweli kweli, sikutegemea ataungwa mkono kiasi hiki hadi hata maeneo ambayo ni ngome kabisa ya NASA. Ana dhamana kubwa hatamu hii, ajaribu kila jinsi ya kutuunganisha Wakenya.

Kenya tukirekebisha ukabila, tutakua kwenye ligi ya nje ya Afrika, japo pia ndio demokrasia yenyewe hiyo, pamoja na kwamba nachukia vigezo vya ukabila, lakini ikumbukwe demokrasia inampa kila Mkenya wa kutumia kutumia kigezo akipendacho kwenye uchaguzi, akiamua kutumia ukabila, huo ni uhuru wake kidemokrasia.
RIP Msando.
 
Usitufanye mafala humu. Yes Uhuru katangazwa mshindi lakini wizi ulikuwa wa hari ya juu. Nasijawahi hona wizi wakipumbavu namna hii. Matokeo yote yalikuwa computer generated.
Haiwezekani matokeo yatangazwe alafu yapande nakushuka kwa wakati mmoja huku yakiachana at the same level kati ya male na female.Pia matokeo kutoka kwenye form na yalio tangazwa yalitofautiana.Peleka huo uwongo Niger forum.
IMG_20170809_222513.png
IMG_20170809_222129.jpg
 
Attachments

  • ad814ae0a0cbdad33c0e2d28ea40db07.jpg
    ad814ae0a0cbdad33c0e2d28ea40db07.jpg
    34.4 KB · Views: 24
Usitufanye mafala humu. Yes Uhuru katangazwa mshindi lakini wizi ulikuwa wa hari ya juu. Nasijawahi hona wizi wakipumbavu namna hii. Matokeo yote yalikuwa computer generated.
Haiwezekani matokeo yatangazwe alafu yapande nakushuka kwa wakati mmoja huku yakiachana at the same level kati ya male na female.Pia matokeo kutoka kwenye form na yalio tangazwa yalitofautiana.Peleka huo uwongo Niger forum.View attachment 566962View attachment 566963

Hamna neno, basi sasa NASA wapeleke hii stakabadhi kotini. Lakini sasa wamekataa kwenda kotini so sijui kutakuwaje. Najuwa pia walileta stakabadhi zingine kwa IEBC lakini hizo stakabadhi zao IEBC ilisema ni fake na wakaonyesha tofauti ya original na fake. Ushauri wangu mimi kwa NASA ni wajaribu kufuatilia mpango wa kwenda kotini kama walivyofanya mara ya mwisho na walisikizwa.
 
Hii ndo original unayo ongelea?? Kuwa IEBC walionyesha. Next time don't play with our mind. Sio kila mtu nimpumbavu. Msije hata sikumoja mkasema kuna nchi hapa Africa yenye democrasy. Never say that. Nahakuna chakujifunza hapo Kenya. Mimi huyo Mbatia nisingependa kumchana sana. Ila muulize ile ofisi yake pale vunjo ina nini cha maana kama isingekuwa yeye kujiunga na Ukawa. Asijidanganye na gorofa aliyo jenga huko vunjo.Abaki na tenzi zake.

FRAUD DETECTED a handwritten Form 34A is discovered on the official IEBC portal for ElWak South polling centre, Bulla Dadacha polling station 02, Mandera Constituency. Cooked results.
IMG_20170815_181812.jpg
 
Hamna neno, basi sasa NASA wapeleke hii stakabadhi kotini. Lakini sasa wamekataa kwenda kotini so sijui kutakuwaje. Najuwa pia walileta stakabadhi zingine kwa IEBC lakini hizo stakabadhi zao IEBC ilisema ni fake na wakaonyesha tofauti ya original na fake. Ushauri wangu mimi kwa NASA ni wajaribu kufuatilia mpango wa kwenda kotini kama walivyofanya mara ya mwisho na walisikizwa.
Move by NASA team not to contest presidential elections will deny IEBC lawyers over Sh2 bn hefty payout. No wonder they want NASA to go to court It is a cartel nation
IMG_20170815_183550.jpg
 
Halafu hilo jina 'Mbatia' mbona kama tumemuazima maana la Kikenya hilo.
Anyway uchaguzi wetu ulikua wa haki, tulidhihirisha demokrasia isiyo ya kawaida Afrika. Hata kama angeshinda Raila, mwisho wa siku ukweli ungekua huo kwamba uchaguzi ulikua wa kipekee, tume yetu ya IEBC walijiandaa ipasavyo.

Kuna tuhuma za kila aina lakini hazina mantiki, eti kwamba password ya bwana Msando ilitumika kudukua mfumo, watu wanachukulia mifumo kuwa jambo la kawaida sana. Kama angeuawa usiku wa kuamkia uchaguzi, labda hapo ningekubali, lakini sio pale mtu anauawa siku kadhaa kabla halafu eti password yake bado inakua hewani tayari kwa matumizi. Ikumbukwe huo mfumo hakuutengeneza yeye, ulitegenezwa na kampuni ya Ulaya ambayo ilikua na dhamana ya kuulinda hadi mwisho.

Vongozi wa NASA walionyesha logs za MS server 2008, mfumo uliopitwa na wakati sana, IEBC wanatumia Oracle solutions. Hapa wakubali walishindwa kabisa yaani herufi kwa herufi, namba kwa namba, leo hii viongozi wao mikoani na kwenye gatuzi zote wanapokea vyeti vya ushindi huku wakilalamika kwamba uchaguzi haukua wa haki, huo ni unafiki. Ikumbukwe pia Jubilee wamezoa idadi kubwa ya magavana, maseneta, wabunge yaani huu ulikua ushindi wa kichapo.

Uhuru aliuza sera zake kweli kweli, sikutegemea ataungwa mkono kiasi hiki hadi hata maeneo ambayo ni ngome kabisa ya NASA. Ana dhamana kubwa hatamu hii, ajaribu kila jinsi ya kutuunganisha Wakenya.

Kenya tukirekebisha ukabila, tutakua kwenye ligi ya nje ya Afrika, japo pia ndio demokrasia yenyewe hiyo, pamoja na kwamba nachukia vigezo vya ukabila, lakini ikumbukwe demokrasia inampa kila Mkenya wa kutumia kutumia kigezo akipendacho kwenye uchaguzi, akiamua kutumia ukabila, huo ni uhuru wake kidemokrasia.
You should never ever ever ever and ever write this kind of words to us, we are not fools or not everyone is a Kikuyu or Kalenjini.
(Anyway uchaguzi wetu ulikua wa haki, tulidhihirisha demokrasia isiyo ya kawaida Afrika. Hata kama angeshinda Raila, mwisho wa siku ukweli ungekua huo kwamba uchaguzi ulikua wa kipekee, tume yetu ya IEBC walijiandaa ipasavyo.) Never ever. Am evil but i don't lie when I kill I say I have killed. My brain is usually affected by people who lie and we have killed many because of that. Unataka tuseme uchaguzi ulikuwa wa haki kwa huu upumbavu.
IMG_20170812_223600.jpg
IMG_20170812_222123.jpg
 
Kama na wewe una mawazo basi nyie ni suala la muda tu kuna siku mtachinjana tu, mnaweka vizazi vyenu rehani, Sisi lugha yetu ni moja tu kiswahili nchi nzima, lugha ya kikabila ongelea chumbani na mke wako, Hivi unawezaje kuanza kuongea kikabila mbele ya jamii
Huyu MK mtu waajabu sana. Jamaa analeta hoja akizani sisi ni wakabila. Mimi hapa nikianza kushusha hadi video zinazo onyesha wizi ukifanyika live sijui atasemaje. Huyo Mbatia najua hadi ndani ya nyumba yake. Huruma ya Kikwete na Ukawa isimfanye awe mtu wa kulopoka. He was part of the system.
 
Wizi uliofanyika Kenya hakuna nchi Africa Mashariki imewahi ufikia. Pia walikua wanagawa karatasi za kura zilizopigwa rejected kwa nyuma kwenye strong hold za NASA ilikuaribu kura zake.
IMG_20170815_181534.jpg
 
Shirika la wanawake lamtaka Raila kutuliza wafuasi wake
Imepakiwa - Monday, August 14 2017 at 17:14
Kwa Mukhtasari
SHIRIKA moja la kukuza wanawake kuwa viongozi Jumanne lilimtaka kiongozi wa NASA Raila Odinga kuwatuliza wafuasi wake wakome kuzua ghasia.

Wakiongea jijini Nairobi viongozi wa kundi la Women Empowerment Kenya (WEK) walisema Raila anapasa kuwaeleza wafuasi wake wasijihusishe na visa vya ghasia.

“Tunamhimiza kiongozi wa NASA Raila Odinga kutuliza hasira za wafuasi wake. Tunaamini kwamba kuna njia za kisheria za kutatua mizozo ya kisiasa kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya kura ya urais,” alisema mwenyekiti wa kundi hilo Bi Truphena Moraa.

Alisema ni jukumu la viongozi wa kisiasa kuwatuliza wafuasi wao ili kuepuka umwagikaji wa damu. Aidha, waliwataka polisi kutotumia nguvu kupita kiasi katika harakati za kukabiliana na waandamanaji.

“Ninaamini kwamba baada ya ghasia zilizoshuhudiwa, Wakenya wataendelea kupendana na kupenda nchi yao,” alieleza Bi Moraa.

Aliwataka wabunge waliochaguliwa kupitisha sheria ya usawa ya jinsia ili wanawake zaidi waweze kuteuliwa bungeni na katika nyadhifa za uongozi.

“Ninamuomba Rais Uhuru Kenyatta kuongoza juhudi za kupitisha na kutekelezwa kwa sheria inayohakikisha kuwa thuluthi moja ya wabunge sio wa jinsia moja,” aliongeza Bi Moraa.

Alisema ili Kenya ipate ustawi, wanawake wanapasa kupewa nafasi ya kuchangia katika maamuzi.

Source: Shirika la wanawake lamtaka Raila kutuliza wafuasi wake
 
Raila aahirisha kutoa dukuduku lake kuhusu uchaguzi

Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga akihutubu awali. Picha/KEVIN ODIT
Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Tuesday, August 15 2017 at 14:08
Kwa Mukhtasari
Muungano wa National Super Alliance (Nasa) umeahirisha hotuba ya kinara wake Raila Odinga kwa taifa iliyotarajiwa kwa hamu na ghamu leo Jumanne kutokana na uamuzi na mwelekeo wake wa kauli ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo Jumanne, Agosti 8, 2017

Kufuatia uchaguzi huo uliofanyika kote nchini, Rais Uhuru Kenyatta wa Jubilee Party alitangazwa kuwa mshindi mnamo Ijumaa Agosti 11 na mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Bw Wafula Chebukati kwa kuzoa kura 8,203,290 ikiwakilisha asilimia 54.24 naye kinara wa Nasa Raila akipata kura 6,762,224 ikiwa ni asilimia 44.72, ya kura zote zilizopigwa.

Hotuba yake imeratibiwa hadi kesho (Jumatano) majira ya asubuhi, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya kinara mwenza Bw Musalia Mudavadi ambaye pia ni mkurugenzi na ajenti mkuu wa Nasa.

Duru zimearifu Swahilihub kwamba muungano wa Nasa ungali kwenye mazungumzo ya faragha kuhusiana na maswala tata waliyosema yalisababisha shughuli ya uchaguzi kutokuwa wa halali.

Hata hivyo tume ya IEBC ilishikilia iliendesha uchaguzi kwa njia ya huru, haki na wazi, kauli iliyoungwa mkono na wachunguzi wa kimataifa.

Licha ya kinara wa Nasa Raila mnamo Jumapili Agosti 13 kuwaeleza wananchi wasiende kazini siku iliyofuata ya Jumatatu na Jumanne, wengi wamekaidi amri yake na kuenda gangeni kama kawaida kuzimbua riziki.

Kutokana na maamuzi ya IEBC, wafuasi wa Nasa walizua ghasia katika mitaa kama vile; Mathare, Kibera, Kawangware Kaunti ya Nairobi na baadhi ya maeneo Kaunti ya Kisumu.

Kinara huyu aidha alieleza wananchi wasiende kazini mnamo Jumatatu, akiahidi kutoa mwelekeo na msimamo wake leo Jumanne.

Jijini Nairobi wananchi wanaendelea na kazi zao kama kawaida, huku kila mmoja akionekana kuwa kwenye harakati zake za kusaka riziki.

Bi Rispah Gichohi, mmiliki wa Uvazi Couture, duka la kushona mavazi Nairobi alifungua biashara yake kama ilivyo desturi na anaendelea vyema. "Nina familia inayonitegemea, nikikosa kufanya kazi watakula kwa nani?" ametaka kujua Bi Gichohi kwenye mahojiano ya kipekee na Swahilihub.

Akaongeza: "Usalama umeimarishwa, na sioni haja ya mtu kukosa kufanya kazi."

Mnamo Jumamosi Agosti 12, Kaimu Waziri wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang'i alihakikishia taifa kuwa liko salama.

Hata hivyo idadi kamili ya waliofariki kutokana na ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi, inakinzana.

Kaunti ya Kiambu, inayoaminika kuwa ngome kuu ya Rais Kenyatta taswira ni ile ile, kila Mkenya akiwa kazini.

Hata hivyo usalama umeimarishwa kaunti hii huku maafisa wa kukabiliana na ghasia GSU wakishika doria, ingawa wanatangamana na wananchi kwa furaha kwa kuwa amani imeshamiri.

"Huku kazi ni kama kawaida, hata nyinyi wenyewe mnajionea. Nina mtoto ambaye akirejelea shuleni atahitaji karo," akaeleza Bw John Ngugi, mekanika wa Tuk Tuk Mumbi, Kiambu, akiendelea kuhudumia wateja wake.

"Kwa nini nikose kufanya kazi ilhali majukumu ya familia yananiongoja? Wakenya tufanye kazi, uchaguzi umeisha sharti gurudumu la maisha tulisukume," akaongeza Bw Kevin Ochieng, mekanika mwenza Ngugi.

Maeneo mengine nchini kama vile; Kaunti ya Mombasa, Nyeri, Meru, Nakuru, Uasin-Gishu, Bungoma, na kaunti zingine shughuli za kutafuta riziki zinaendelea kama kawaida.

Mnamo Jumapili Gavana wa Kisumu aliyechaguliwa, Profesa Anyang' Nyong'o alishauri wananchi kurejea kazini wakuze nchi.

Rais Kenyatta aliwania kuhifadhi kiti chake kwa awamu ya pili na ya mwisho akisaidiwa na mgombea mwenza Bw William Ruto, ambaye pia ni Naibu Rais.

Aidha Raila (ODM), alisaidiwa na mgombea mwenza Kalonzo Musyoka (Wiper Party)
Source: Raila aahirisha kutoa dukuduku lake kuhusu uchaguzi
 
Back
Top Bottom