MH KAWAMBWA live on TBC mada kuu Elimu/Matokeo

 
Last edited by a moderator:
Kamishna wa elimu Prof Bhalalusesa alihitimisha kwa kuomba wadau tuchangie kwenye elimu, ni vema tufanye hivyo kuliko kulaumiana
 
Kawambwa: Matokeo ni mabaya kwa sababu shule za serikali ni nyingi.
Mwaka wetu sisi tuliosoma shule serikali hiyo hiyo wanafunzi walikuwa zaidi ya mia nne zero zilikuwa 26 tu wani 78 tatu za kumwaga usiulize mbili. Ukiangalia shule hiyo hiyo sasa hivi ni kichefuchefu, This Guy is RUBBISH he is no Phd kabisa
 
Mwaka wetu sisi tuliosoma shule serikali hiyo hiyo wanafunzi walikuwa zaidi ya mia nne zero zilikuwa 26 tu wani 78 tatu za kumwaga usiulize mbili. Ukiangalia shule hiyo hiyo sasa hivi ni kichefuchefu, This Guy is RUBBISH he is no Phd kabisa
vipi paper haikuvuja?
 

Mh Kawambwa hajajiuzulu tu anangoja nini!
 

Huyo kawambwa hajajiyxuru tu?anaanza tena kuzungukia vitui vyavtv kutudangany'a juu ya sababu ya kufeli wanafunzi. Yeye si alifikiri tv na radii ndio waalimu akawa anajadiliana na hivyo vituo badala ya kuongea na walimu wakati wa mgomo? kweli hatuna viongozi
 
Ili Tanzania iweze kupata maendeleo ni lazima makosa kama haya ya wazi wazi yaondoke ya kuwa na viongozi kwa maslahi yao binafsi na wasio kuwa na aibu hata punje moja. Mtu asiye na aibu kama inavyoonekana kwa Kawambwa ni hatari kwa taifa kwa kuwa malengo yake ni tofauti kabisa na matarajio ya wengi. Kinachoonekana hapa ni kwamba malengo la kawambwa siyo haya ambyo sisi wananchi wengi tunayatarajia na ndiyo maana anaweza kujitokeza hadharani kutetea matarajio yake kwa kuwa amefanikiwa kuhakikisha ameliangamiza taifa la Tanzania.

Haiwezekani katika hali ya kawaida Waziri, unatokea uharibifu mkubwa (janga) halafu yeye anenda kwenye media kuongea ujinga na hata dhamira yake haionyeshe kwamba kuna kitu kimeharibika. Huenda anataka kusikia wanafunzi wote waliomaliza kidato cha nne wamekufa wote ndiyo aweze kuona sasa hii ni hatari.

Hauwezi kwenda kwenye media kuongea kuwa wanafunzi wanafeli kwa sababu kuna shule nyingi za Serikali. Wakati sisi tuliposoma shule za Serikali zilikuwa bora kuliko hata Seminary, ajiulize what went wrong and why? siyo kwenda kuongea ujinga mtu na akili yake.

Kuna haja ya kuangalia uhalisia wa hiyo PhD yake maana pia anaidhalilisha.

Siku zote ninaamini, kiongozi mzuri ni yule anayeangalia nje ya dirisha na kutoa credits kwa watu/vitu vingine vinavyowezesha mambo kwenda vizuri na kujiangalia kwenye kioo na kujipa lawama pale mambo yanapokuwa hayaendi vizuri ili kuweza kujisahihisha kuliko kutumia lawama watu na wewe kutaka sifa tu. Kawambwa anataka sifa tu siyo kuwajibika. Eti watoto hawasomi ndiyo maana wanafeli, je amejiuliza kwa nini hawasomi. Wameandika kwenye karatasi za mitihani kuwa kuna masomo hawajawahi kuona mwalimu kwa miaka 4, hakuna vitabu hakuna maabara, walimu hawalipwi n.k yeye hayo hayaoni. Bajeti ya Wizara ya elimu imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, lakini maendeleo ya elimu yamekuwa hakididimia mwaka hadi mwaka yeye haoni hilo.

Siku za karibuni hapa ilisemekana walimu wapo kwenye mgomo baridi yeye hataki kutumia elimu yake na muda kuangalia undani ili kupata ukweli na kutafuta suluhisho badala yake analaumi vitu ambavyo havina kabisa uhusiano wa moja kwa moja na elimu ya mtoto shuleni.

Jamani tupige kelele Kawambwa ajiuzulu kabla hayafanikisha kuliangamiza taifa kabisa. Mimi ninaamini hilo ndilo lengo lake.
 
Ndugu, hakuna mwaka ambao pepa haivuji, wakikwambia leo pepa haijavuja jiulize mara mbili... mara nyingi pepa zote za practical zinavuja kwa wanaosoma sayansi .. huo ni mfano.

Ni mwaka 1998 ambapo form four ilivunja rekodi hadi mtihani uliahirishwa

lakini kama ukitaka kujua kama product ni nzuri angalia performances zao wakienda form six na vyuo... subiri two years from now ndipo utajua pepa inavuja au la
 
Kamishna wa elimu Prof Bhalalusesa alihitimisha kwa kuomba wadau tuchangie kwenye elimu, ni vema tufanye hivyo kuliko kulaumiana

Tuchangie Elimu mara ngapi sasa?
1. Tumeshachangia vya kutosha kupitia kodi zetu ambazo ni P.A.Y.E, VAT, Custom duty, Excise duty, corporate tax.
2. Tumeshachangia vya kutosha kwenye asilimia za means test za loan board kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
3. Tumeshachangia vya kutosha kupitia ujenzi wa Shule za kata.
4. Tumeshachangia vya kutosha kupitia kuanzisha shule binafsi ili kuipa support serikali ktk kutoa elimu.

Sasa huyu jamaa anataka tuchangie nini tena zaidi ya tulivyokwishachangia?
Hapa issue sio kuchangia, issue ni Sera mbovu, mipango mibovu na Usimamizi mbovu wa serikali hii dhaifu katika Elimu.
 
Huyu Kawambwa sijui anataka kutuwamba utando wa ujinga vile!
Kwa hiyo 37% ambayo hata nusu haijafika ndiyo kufaulu?
Faraja gani hiyo anayotughiribu! Hivi wewe Kawambwa ukilipwa 37% ya mshahara wako wa mwezi utaelewa kweli! Nina wasiwasi na U dokta (PhD) wako!
 
Tumefika hapa kwa sabab ya system ya udugunaizeshi,waziri huyo kila wizara anavurunda badala ya kuengulia anabadilishwa wizara,usiposimamia vema suala ulilopangiwa jitoe bila shinikizo
 
hahahaa walio zoea kuchachua mitihani wamepigwa chenga mbaya. wamewakaririsha mitihani wanafunzi wao kumbe ni mitihani fake..
 


Hahahaha! Hapa nimezidi kuamini kuwa, "Mlango mmoja ukifungwa, Mlango mwingine hufinguliwa!"
 
Kasahau 1,shule za Jeshi.kama airwing,jitegemee,...................malizia zingine
 
kwa iyo kawambwa atakosa wateja kwenye cafeteria zake za UDOM hasa za social and humanities
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…