Hivi mnavyo wakejeri wawekezaji wa mpira kwa kiasi hiki mnataka mpira wetu uendeshweje ?
Hamwoni kuwa mnawakatisha tamaa wenye nia ya kuwekeza katika mpira wa Tanzania ?
Hata kama mwekezaji anakosea basi aulizwe kwa staha.
Kuuliza kwa kejeri, dharau, vijembe, na hata matusi ndivyo mnavyotaka ?
Mbona wawekezaji wa maeneo mengine hamuwa ulizi kwa mtindo huu.
MO katika mpango wa kuwekeza Simba amefuata taratibu zote na akapewa baraka na Serikali.
Hizi chuki zinatoka wapi ?
Kwanza MO hata akiweka hapo hiyo B20 bado inakuwa pesa yake tu.
Na anaweza kuiondoa kama hataridhishwa na uendeshwaji wa timu au vinginevyo, au akamwuzia mtu mwingine.
Mnataka kila mtu akiwa na dukuduku mda wowote kuhusu Simba basi amuulize MO popote na MO lazima awajibu wote wanaouliza kwenye Instagramu, Facebook, twitter, na popote pengine.
Viongozi wa Simba wapo, vikao vipo nashangaa huko hamwendi mnataka mjibiwe kwenye mitandao.
Wana michezo wanajua jinsi timu za ulaya kama Manchester United na City, na Chelsea, zinavyoendeshwa na wawekezaji tena watu binafsi.
Jifunzeni kuheshimu wawekezaji, hata kama mtu mmoja au kikundi hakitaki.
MO toka aingie Simba maelfu ya Watanzania wamepata Ajira. Na wanaendelea kuajiriwa kadri Simba inavyo kua.
Kila siku mnalialia humu kuwa nchi haina ajira hasa kwa vijana.
MO kaongeza fulsa ya ajira mnaishia kumtukana, au kumshangila anayemtukana wakati mamia ya watoto wenu wameajiriwa naye.
Kwanini hamwezi kumwelekeza kwa staha pale anapo kosea.
Afrika inakuwa nyuma ktk maendeleo kwa mambo kama haya.
Inavyo itwa Dark- Continent, Shit-Hole. Vinaangaliwa vitu kama hivi.
Poleni sana.