Kwa kawaida huwa kuna makosa madogo ya liufundi ambaye anapelekea hakim au Jaji kuhukumu vinginevyo shauri lililo mbele yake. Lakini kwa hukumu hii ya Godbless Lema nalazimika kumuuliza huyu mheshimiwa amejitathmini vipi? Kubwa zaidi ni jinsi gani mashariki ilivyo mbali na magharibi ambavyo ni sawa na hukumu ya Jaji Lwakibarila aliyoitoa Arusha ilivyo mbali na matokeo ya rafaa ya Lema. Hii ni aibu nyingine ya mwaka katika mahakama kuu. Kweli kuchelewa kufa ni kuona mengi. Ni wakati muafaka kwa mapilato wengine kujitunzia heshima ya uweledi wao badala ya kuendeshwa kwa amri za watu wengine and nguvu nyingine. Mh. Lissu, bado uko sahihi juu ya uteuzi wa hawa waheshimiwa, wengi wao wanaendesha kesi kwa maslahi ya aliyewateua.