Taswira
JF-Expert Member
- Sep 23, 2012
- 1,198
- 447
CHADEMA WAWEWESEKA,YEYE AAHIDI KUKAZA KAMBA MWANZO MWISHO NDANI NA NJE YA NCHI.
Ni kweli,ni uhakika,ni dalili za wazi kuwa Mh.Mwigulu Nchemba sasa hakamatiki,ni moto wa kuotea mbali katika siasa za nchi hii.Akabidhiwa beji ya kuimarisha chama kimataifa.Camera yetu imenasa habari za uhakika kuwa ,Mbunge wa Iramba Mgharibi na Naibu katibu Mkuu wa CCM-TANZANIA BARA Mh.Mwigulu Nchemba anaanza rasmi ziara yake ya kikazi,ziara ya kujenga na kuimarisha chama cha mapinduzi kimataifa,Ziara ya kuzungumza na vyama rafiki wa CCM ndani ya Marekani na Uingereza, ziara ya kuzungumza na watanzania kule kule waliko "MAREKANI NA UINGEREZA".
Mwigulu Nchemba anategema kuanza ziara yake siku ya kesho katika majimbo mbali mbali ndani ya Marekani na baadae kuelekea Uingereza katika miji ya West London,Birmigham,Reading Na Manchester kwa kazi maalum zifuatazo.
1.Mbunge huyo mwiba mkali kwa CHADEMA anategemea kuzunguka zaidi ya Mwezi Mzima Marekani na uingereza kufungua matawi mbalimbali na kuzungumza na wanachama wa CCM Katika Mataifa hayo makubwa mawili Duniani.
2.Pia Mh.Mwigulu Nchemba anategema kwenda kukutana na viongozi wa juu wa vyama vikubwa na vikongwe vya mataifa hayo mawili,Vyama rafiki vya CCM ndani ya Marekani na Uingereza.Hii ni fusa ambayo itatumika kujenga uimara wa CCM kidiplomasia hasa kwenye siasa za kimataifa.
3.Mbunge huyo anategemea kushiriki mkutano wa UN unaotegemea kufanyika mwishoni mwa Mwezi huu ndani ya WASHINGTON D.C (Hapa anategemea kupata uzoefu wa kukaa na kujadili mambo na mataifa makubwa duniani na viongozi wenye beji za heshima mbalimbali katika ulimwengu huu).
4.Pia Mh.Mwigulu Nchemba anategemea kuzungumza na watanzania karibia wote wanaoishi ndani ya nchi hizo mbili.Katika mambo muhimu anayokwenda kuzungumza ni pamoja na Katiba mpya,Maendeleo ya kiuchumi ndani ya Taifa letu,ajira,Amani na mwenendo wa siasa ndani na nje ya Tanzania.Pia anakwenda kujadiliana na watanzania maisha yao nje ya nchi na changamoto wanazokutana nazo.Kubwa zaidi anakwenda kuzungumza uimara wa CCM na uhakika wa kuendelea kuongoza nchi na namna watakavyobwaga upinzani kwenye uchaguzi ujao kwa sababu Upinzani Watanzania haujitambui,hawana malengo,ni vyama vyenye ubinafsi na ufamilia ndani yake hivyo havifai kupewa nchi.
KUWEWESEKA KWA CHADEMA,Paparazi wetu amenasa tetesi kuwa Viongozi wa juu wa CHADEMA wamesikia Taarifa za Mwigulu Nchemba kutua Marekani na Uingereza,jambo hilo linaonekana kuwapa wakati mgumu sana viongozi wa CHADEMA na kupelekea kufanya vikao vya ghafla vya hapa na pale na kufikia maamuzi ya kumwmbia Dr.slaa naye afunge ziara kwenda marekani siku tatu akajaribu kujibu mapigo ya Mh.Mwigulu Nchemba.
Kuweweseka huku kwa CHADEMA si mara ya kwanza,kila mmoja anakumbuka kuwa Mh.Mwigulu Nchemba aliporejea kutoka china baada ya kukutana na viongozi wa juu wa kikomunisti wa nchi ile,CHADEMA waliloa jasho,wamekuwa wakilia kila siku kuwa Mwigulu anawadhoofisha kisiasa na wamekuwa wakisema alikwenda china kwa lengo maalumu la kujifunza siasa za kisayansi.JE MWIGULU NCHEMBA AKIREJEA KUTOKA MAREKANI NA UINGEREZA CHADEMA MTAPONA KWELI???Mziki wa China tu imewafanya chadema wachuje kiasi kwamba inaonekana sio chama cha upinzani tena.Hii yote ni kazi ya mikono ya Mh.Mwigulu NChemba kuhakikisha upinzani hawafui dafu mbele ya CCM na kweli imewezekana.
Je ikirejea kutoka ziara ya Marekani tutegemee nini kama sio kifo cha chadema ama kusambaratika kabisa???
Duru za habari zainaonesha wazi kuwa Mh.Mwigulu Nchemba ndiye kijana anayeandaliwa na watu wakubwa wanchi hii kuchukua nafasi ya Urais,Rejea kauli ya JK kuwa nchi hii hatamuachi mtu Mzee.BASI kaaa ukijua kuwa Mh.Mwigulu Nchemba anaandaliwa kiti cha kugombea Urais,na vijana wa CCM wanasubiria kwa hamu sana kuona Mbunge huyo anatajwa kuwa ndiye atapeperusha bendera ya CCM kwenye kiti cha Urais.
Hii ya Urais inaonekana kuwa mwiba sana Kwa CHADEMA kutokana na namna wanavyomuogopa Mbunge huyu,iwapo yeye ni mbunge tu amewashinda kisiasa kiasi hiki,Je akiwa Rais wanchi tutegemee kuiona chadema tena??Tusubiri macho yetu tu kuona chadema na vyama vya upinzani vikitafuta njia mbalimbali za kukimbilia.
Nilipojaribu kumtafuta Mh.Mwigulu Nchemba kuhusiana na ziara hii kama ni kwelu au la!!akaniambia "Ni kweli naeleka kikazi zaidi huko Marekani na Uingereza,napeperusha bendera ya nchi yangu na chama changu kimataifa,Nakwenda kukutana na viongozi mbalimbali wa vyama rafiki na CCM,nakwenda kuzungumza na Watanzania wenzangu,nakwenda kuimarisha chama na kufungua matawi ya CCM huko nje ya nchi,Nimezaliwa kwaajili ya kulitumikia Taifa langu na chama change CCM,Na furaha yangu ni kuona wale ninaopambana nao kwenye siasa wanakasirika kila siku kwani ni ishara ya wazi kuwa nawapiga kisawasawa na nitaendelea kufanya hivyo bila kukata tamaa." alidokeza.
ASANTE.