Nakumbuka mwaka elfu mbili na kumi walimu walipogoma mh. rais Jakaya Mrisho Kikwete alitoa hotuba kali ikiwataka waalimu kuacha kugoma akasema "Atakayeendelea mgomo,kama hataki kazi aache akafanye kazi zingine serikali haina hela"
Mh. Hawa Ghasia akasema "mwalimu nae anagoma,je askari mwenye bunduki"
Nikiona kauli hizi na zingine za viongozi kwa mgomo wa waalimu siamini kama wajumbe wa bunge la katiba wanaweza kuitetemesha serikali kiasi cha kuundiwa tume!
Nataka kujua je,walimu na wabunge wa bunge la katiba ni nani muhimu zaidi kwa nchi yetu?
Nauliza kwa sababu waalimu wakidai viongozi wanawashangaa hawasikilizwi lakini bunge la katiba wanadai posho iongezwe serikali inatetemeka! Kilikoni!