Mh Rais anaweza kulivunja Bunge la Katiba ?

Mh Rais anaweza kulivunja Bunge la Katiba ?

The Fixer

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
1,365
Reaction score
594
Wana ndugu,
Naomba wale wenye maarifa ya upande wa sheria au wajuvi au wabobezi wa Sheria watuambie ikiwa tutapaza sauti zetu na Mh Rais kwakuwa ni mtu msikivu na akaamua kwa dhati kabisa kulivunja Bunge hili la Katiba na kutoa muda kwa wenye nia ya dhati kabisa ku apply walau Laki 1 kwa siku hapa Dodoma mpo tayari ?

Hii kuwa mjumbe tu ni heshima kubwa sana kwa nchi zingine unaweza mtu kuhudhiria kwa kujitolea tu, buree kabisa

Tumshinikize Rais alivunje tu kama ni mbwai ni mbwai tu
 
avunje bunge ili iweje kuzinguana ndio kupata katiba bora.
 
Mmeshindwa kumshinikiza kwenye mambo ya msingi ya gharama za umeme mnakomaa na mambo ya kifala. This country has poor quality citizens.
 
Kama BUNGE hili litaafikiana muundo wa SERIKALI moja ama KUVUNJA MUUNGANO, basi anaweza kulivunja. Maana hata kuwa na uhalali wa kuwa Rais maana katika kiapo chake cha URAIS aliapa kulinda MUUNGANO.
 
Nakumbuka mwaka elfu mbili na kumi walimu walipogoma mh. rais Jakaya Mrisho Kikwete alitoa hotuba kali ikiwataka waalimu kuacha kugoma akasema "Atakayeendelea mgomo,kama hataki kazi aache akafanye kazi zingine serikali haina hela"

Mh. Hawa Ghasia akasema "mwalimu nae anagoma,je askari mwenye bunduki"

Nikiona kauli hizi na zingine za viongozi kwa mgomo wa waalimu siamini kama wajumbe wa bunge la katiba wanaweza kuitetemesha serikali kiasi cha kuundiwa tume!

Nataka kujua je,walimu na wabunge wa bunge la katiba ni nani muhimu zaidi kwa nchi yetu?

Nauliza kwa sababu waalimu wakidai viongozi wanawashangaa hawasikilizwi lakini bunge la katiba wanadai posho iongezwe serikali inatetemeka! Kilikoni!
 
hii nchi imeshaoza... na katika hili ndipo ushahidi mmojawapo wa kuoza kwake unapothibitika
 
Back
Top Bottom