Hakika umezidi kudhihirisha ya kwamba wewe ni rais wa watu,rais wa Watanzania wote bila kujali makundi ya kisiasa yanayojaribu kutaka kuhodhi mchakato wa kupatikana katiba mpya.Umewapasha waziwazi baadhi ya makundi hasa ya vyama vya siasa kushinikiza katiba mpya iwe na matakwa yao ya kisiasa au kimakundi. Juhudi zako za kupatikana kwa katiba mpya ni jinsi gani unavyoguswa na mabadiliko ya kisiasa,kiuchumi,kijamii ktk nchi yetu kwa mustakabali wa Taifa letu.Watanzania wote tunaunga mkono na kutambua juhudi zako za kutuongoza ili tupate katiba mpya kwa faida ya Watanzania wote na Ulimwengu kwa ujumla.Vile vile uongozi wako wenye tija ni tunu kubwa kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla.MUNGU AZIDI KUKUBARIKI KTK JUHUDI ZAKO ZA KUWATUMIKIA WATANZANIA.