Unapaswa kumtetea mtu baada ya kumfahamu. Hata Wakili hawezi kumtetea mtuhumiwa katika kesi bila kupata undani wa tukio toka kwa mtuhumiwa au watu wa karibu au mwenendo wa kesi yenyewe. Tunaomfahamu tulisema mapema humu juu ya ukanda, ukabila na umimi lakini tulitukanwa sana.
Na hata Leo kuna watu watakuja kukushambulia kuonesha hakuna ukweli katika tuhuma zako. Lakini ni ukweli ulio wazi kuwa uliyosema yako wazi, mgawanyiko unaonekana wazi kikabila, kikanda, kisiasa na kujuana.
Kama uliwahi kufanya kazi naye mahali Fulani wewe ni mtakatifu mpaka mwisho hata kama una makandokando, kanda ya kwetu inapelekewa kila chema hata mbuga imehamishiwa huko ili Watalii wasiende kaskazini. Ni mengi ila mtayaona mkiamua kufumbua macho.