Mh. Rais wangu, naomba elekeza jicho lako kwny sector ya michezo

Mh. Rais wangu, naomba elekeza jicho lako kwny sector ya michezo

kluger

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
2,093
Reaction score
1,899
Nakupa heshima maridhawa Rais wangu wa awamu ya Tano, hakika unafanyakazi stahiki.

Naomba utazame sekta hii ya michezo yote nchini chini ya vyombo mbalimbali vya usimamizi wa serikali.

Eneo hili limeficha wababaishaji na wafujaji wengi wa raslimali za umma.
Wengi ni wababaishaji huku wakitumia vibaya kodi za wananchi bila kufuata kanuni za kiuendeshaji, kumeoza sana.

Badala ya michezo kuleta raha iliyokusudiwa imebakia karaha na kadhia kwetu sisi walipa kodi.
Inauma sana kila mwaka, kila michezo katika nchi hii timu za taifa zinafanya vibaya huku mamilioni ya fedha yakiteketea kwa safari na posho zisizo na tija.

Eneo hili linaweza kuzalisha ajira nyingi hasa kwa vijana, mapata makubwa kwa serikali na hata kutangaza jina la nchi.
Lakini hivi sasa ni kinyume chake, kuanzia ngazi za vilabu ni ubabaishaji tu, na vyombo vya kusimamia michezo hii vipo bila meno. Mfano haiingii akilini vilabu kushiriki ligi ya taifa bila viwanja vya mipira, hii ni ajabu sana yaani unakuwa mkulima bila kuwa na jembe!!, kweli??? Na Chama cha mpira wa miguu kipo, wakijilipa kila mwezi.
Pili, matokeo yamekubikwa na rushwa iliyokidhiri, kupanga matokeo kisha kuuaibika kimataifa.

Nashauri nchi ijitoe katika mashindano yote ya kimataifa kwa muda wa miaka mitatu na kufumua mifumo yote ya uongozi katika michezo na kuleta wataalamu toka nje ya nchi zilizopiga hatua.

Lakini pia waziri wako wa michezo si sahihi katika Eneo hili, hakusaiidii. Tunahitaji mtu makini asiyeendekeza siasa bali kazi tu.

Ahsante sana, nitashukuru sana kupokea maoni yangu.
 
Back
Top Bottom